ukiona mtu anafanya biashara Tanzania, na biashara yake imedumu kwa zaidi ya miaka mitano (5) ujue huyo mtu ana roho ngumu sana. Bila hivyo ndani ya miaka mitano lazma uwe chali.
Ili uweze kufanya baishara Tanzania lazima uwe kama John Wick au Rocky Balboa. Uwe na roho ya paka, na uwe na vitu vifwatavyo
1. Focus
2. Commitment
3. Sheer will
4. Perserverance
Wengi wanakuwa na number 1 na 2 na hao ndio wengi wanaishia njiani. Tanzania bila sheer will and perseverance, hufanyi biashara. Angalia watu unaopambana nao ukiwa mfanyabiashara Tanzania
1. TRA
2. Fire
3. OSHA
4. Manispaa
5. Bwana afya
6. Serikali za mitaa na madiwani
7. TMDA
8. Polisi
9. Wafanyakazi wako (muda wote wanawaza kukuibia)
10. Majirani, ndugu, na marafiki zako
11. Wafanyabiashara ambao mko sekta moja na ni majirani.
12. Majambazi na vibaka
13. Mafuriko na majanga ya moto
14. Maagano ya ancestors wako
na mengineyo mengi mno. Hapo inabidi uwe mwamba ndio utoboe!