TRA yaweka rekodi ya kukusanya Trilioni 27.6 kwa mwaka 2023/2024

TRA yaweka rekodi ya kukusanya Trilioni 27.6 kwa mwaka 2023/2024

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Licha ya mgomo na Hujuma za wafanyabiashara waliochochewa Kisiasa ila TRA imeandika rekodi ya Kukusanya Shilingi Trilioni 7.3 robo ya mwisho wa mwaka (April-June) na pia imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 27.6 Kwa mwaka mzima kati ya lengo la kukusanya Trilioni 28.3.👇👇
---
Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi imesema katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/24, imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa 97.67% ya lengo la kukusanya Tsh. trilioni 28.30.

Taarifa iliyotolewa leo July 01,2024 na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidato imesema “Makusanyo haya ni ongezeko la 14.50% ikilinganishwa na makusanyo ya Tsh. trilioni 24.14 katika Mwaka wa Fedha uliopita, 2022/23”

“Katika kipindi cha robo mwaka ya nne yaani Aprili - Juni, 2024, TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 7.09, sawa na ufanisi wa 99.46% ya lengo la kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 7.13, makusanyo haya ni ongezeko la 24% ukilinganisha na kiasi cha Tsh. trilioni 5.72 kilichokusanywa katika kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha uliopita 2022/23”

Tunaendelea kuweka rekodi sawa za Rais Samia.Alikuta Mapato ya Juu kabisa Kwa mwezi ni 1.5T(2020/2021) na Sasa ameyafikisha 2.5T(2024/25) yaani ongezeko la Trilioni 1 ndani ya miaka 4.

Kuna Marais wakiongeza Bilioni 500 tuu Kwa miaka 5 ila Makelele waliyokuwa wakipinga Sasa hatukunywa maji.

Saizi Wana wimbo wao Mpya Utasikia watu wanapiga sana hela awamu hii ila ukiwaambia wakati hawapigi hela pesa ziliwmda wapi wataishia kutukana 😂😂😂😂😂.

My Take
Hongera TRA Kwa kazi nzuri, Hongera Samia Kwa kukusanya Kodi kubwa na hongera walipakodi wote.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C85cFw2tnIh/?igsh=YWhram1xcGY4cjli

Mambo ya Kugoma sio dili ,tunajichelewesha na kuchelewesha maendeleo ya Nchi.

Samia Mama wa Taifa ndio gwiji wa Uchumi wa Kisasa ,mama Anatosha na chenji inabaki.👇👇

View: https://twitter.com/TRATanzania/status/1808786525653475627?t=sDE6atWbVdaO8dQVKhnZKA&s=19

Pia soma Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu
 
Licha ya mgomo na Hujuma za wafanyabiashara waliochichewa Kisiasa ila TRA imeandikwa rekodi ya Kukusanya Shilingi Trilioni 7.3 robo ya mwisho wa mwaka (April-June) na pia imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 27.6 Kwa mwaka mzima kati ya lengo la kukusanya Trilioni 28.3.👇👇
---
Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi imesema katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/24, imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa 97.67% ya lengo la kukusanya Tsh. trilioni 28.30.

Taarifa iliyotolewa leo July 01,2024 na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidato imesema “Makusanyo haya ni ongezeko la 14.50% ikilinganishwa na makusanyo ya Tsh. trilioni 24.14 katika Mwaka wa Fedha uliopita, 2022/23”

“Katika kipindi cha robo mwaka ya nne yaani Aprili - Juni, 2024, TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 7.09, sawa na ufanisi wa 99.46% ya lengo la kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 7.13, makusanyo haya ni ongezeko la 24% ukilinganisha na kiasi cha Tsh. trilioni 5.72 kilichokusanywa katika kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha uliopita 2022/23”

My Take
Hongera TRA Kwa kazi nzuri, Hongera Samia Kwa kukusanya Kodi kubwa na hongera walipakodi wote.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C85cFw2tnIh/?igsh=YWhram1xcGY4cjli

Mambo ya Kugoma sio dili ,tunajichelewesha.

Huo ni usanii tu, hakuna kipya cha maana. Ngoja nikupe shule kidogo hapa.

1. Thamani ya shilingi yetu imeshuka sana, hivyo tarakimu kubwa za mapato kwa kutumia shilingi yetu haziakisi uhalisia.

2. Mfumuko wa bei ni mkubwa sana na hilo litaakisi pia kwenye makusanyo ya kodi kuwa na tarakimu kubwa, lakini ukija kwenye uhalisia hayo mapato sio chochote kwenye kutumika kulipia huduma au manunuzi ya bidhaa.

3. Mfumo wa ukusanyaji mapato kwa TRA umejikita kumnyonya mlaji wa mwisho, na kitakwimu idadi ya watanzania inaongezeka kwa zaidi ya watu milioni moja kwa mwaka, hivyo automatically mapato ya TRA yataongezeka kufuata hilo.
 
Ni vizuri sana, sasa wamepata bilioni 190 za kununulia VX V8 za TAMISEMI. Nchi ya hovyo sana hii
 
Attachments

  • 20240702_072327.jpg
    20240702_072327.jpg
    192.8 KB · Views: 5
Huo ni usanii tu, hakuna kipya cha maana. Ngoja nikupe shule kidogo hapa.

1. Thamani ya shilingi yetu imeshuka sana, hivyo tarakimu kubwa za mapato kwa kutumia shilingi yetu haziakisi uhalisia.

2. Mfumuko wa bei ni mkubwa sana na hilo litaakisi pia kwenye makusanyo ya kodi kuwa na tarakimu kubwa, lakini ukija kwenye uhalisia hayo mapato sio chochote kwenye kutumika kulipia huduma au manunuzi ya bidhaa.

3. Mfumo wa ukusanyaji mapato kwa TRA umejikita kumnyonya mlaji wa mwisho, na kitakwimu idadi ya watanzania inaongezeka kwa zaidi ya watu milioni moja kwa mwaka, hivyo automatically mapato ya TRA yataongezeka kufuata hilo.
Ni ujinga na umbumbumbu kulinganisha thamani yetu na Dola badala ya kuangalia inaweza kununua nini ndani ya Nchi.

Maendeleo na thamani ya Shilingi havihusiani.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C85MYDqi1Ui/?igsh=MTF0cjZtODAzdzhlMQ==
 
Ni vizuri sana, sasa wamepata bilioni 190 za kununulia VX V8 za TAMISEMI. Nchi ya hovyo sana hii
Ila mlio wengi ni nyumbu kabisa, Bajeti inayosemwa hapa ni ya 2023/24 na pesa zimeshatumika hapa ni reporting tuu wewe Kwa akili zako za kuku unajua labda wanakusanya ndio wanaanza kutumia 😆😆😆😆

Harafu majinga kama nyie ndio mnataka mpewe Nchi 🤣🤣
 
Nikiona post zako nahisi unaandikia ukiwa chooni unajisaidia aja kubwa ambayo Jana umekula mabungo na mbegu zake
Haijalishi naandika nikiwa nakupumulia au wapi ila Cha muhimu hapa ni content ya mada imekufikia na umeielewa Kwa Kasi nzuri ya Samia na TRA.
 
Zanzibar makusanyo Bilioni 700 bujeti ilikua trilioni 2.8.

Mwaka huu wa fedha ulioanza Zanzibar wameweka bajeti ya trilioni 5 na ushee.

Assume Zanzibar mwaka huu watakusanya trilioni 1 ingawa haitafika. Bado kuna pungufu ya trilioni 4., 80%

Unajiuliza hizi figures hua wachumi wetu wanazitoa wapi?
 
Zanzibar makusanyo Bilioni 700 buneti ilikua trilioni 2.3.

Mwaka huu wa fedha ulioanza Zanzibar wameweka bajeti ya trilioni 5 na ushee.

Assume Zanzibar mwaka huu watakusanya trilioni 1 ingawa haitafika. Bado kuna pungufu ya trilioni 4., 80%

Unajiuliza hizi figures hua wachumi wetu wanazitoa wapi?
60% ya Bajeti Yao watakopa,mada nilishaiweka hapa jukwaani,jisomee hapa Marais Museveni wa Uganda & Mwinyi wa Zanzibar Wamekataa Itikadi za Kijamaa, Bajeti zao kugharamiwa na Mikopo kwa 60%
 
Ila mlio wengi ni nyumbu kabisa, Bajeti inayosemwa hapa ni ya 202/24 na pesa zimeshatumika hapa ni reporting tuu wewe Kwa akili zako za kuku unajua labda wanakusanya ndio wanaanza kutumia 😆😆😆😆

Harafu majinga kama nyie ndio mnataka mpewe Nchi 🤣🤣
Kwa hiyo nchi inaanza mwaka mpya wa fedha za zero balance, ndezi sana wewe.
 
Back
Top Bottom