TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede amepokea orodha ya huduma za malazi iliyoboreshwa 2020 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki ili kuiwezesha TRA kukusanya tozo ya Kitanda Siku kutoka kwa Watalii wanaotumia huduma za malazi.

9DD4D73D-DDC2-42FF-8CDF-5130746B2893.jpeg


Hii ni katika harakati za kuongeza mapato
 
Shule ya St. JUDE wameifungia account zao kisa hawakupeleka watoto wao kwenye kampeni za CCM, kuimba mapambio kama shule nyingine.

Hii nchi kumpa huyu dereva lesseni ya kutuendesha, tumeingia chaka.

1) Mwenye kampuni ya kutembeza watalii, alipie kampuni yake kodi.

2) Na hayo magari yake ya kampuni ya watalii, alipie kodi.

3) Gari likiwekewa mafuta, unakutana na kodi.

4) Dereva nae, alipe kodi lesseni yake na ajira yake sambamba na kodi ya Trafic Police (Vijana wa kukusanya mapato TRA).

5) Mwenye hoteli wanaofikia watalii hao (Pengine mwenye kampuni ya utalii ndio hoteli yake pia), alipe kodi. Ndani ya hio hoteli yake anayoilipia kodi, chumbani kitanda nacho kikilaliwa, kilipiwe kodi.

Halafu serikali tunaambiwa haina hela. Shabaashi.

Wasisahau na KODI YA KUTUMIA VYOO KWA WATALII (Kama Vyoo Vya Kulipia Standi Za Bus).
 
Ni jambo la kheri kama wamepunguza PAYE kwenye mishahara ya wafanyakazi, na ikepelekwa sehemu nyingine. Ni kweli serikali inahitaji pesa kwa ajili ya maendeleo. Sasa wapunguze PAYE halafu wasiwachaji wageni?
 
Hi kodi ipo muda mrefu,Hoteli za mbugani ndio walikua wanalipa.Walikua wanaforce hoteli za mjini nao walipe.Ile ni kuongeza tu mzigo kwa wamiliki wa hoteli na kwa watalii.Hoteli industry ina kodi na tozo zaidi ya 12.
 
Back
Top Bottom