TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

Si kuna ndege lakini?
Ni jambo la kheri kama wamepunguza PAYE kwenye mishahara ya wafanyakazi, na ikepelekwa sehemu nyingine. Ni kweli serikali inahitaji pesa kwa ajili ya maendeleo. Sasa wapunguze PAYE halafu wasiwachaji wageni?
 
kodi ya BAO nayo wataleta, yaani mkiingia gesti unahesabiwa IDADI YA BAO unazilipia kodi# MATAGA
 
yani huyu dada hajawahi post eti "magufuli awanyoosha mabeberu...." mwikoooo yeye yale mabaya tu ,daah kuna watu wanaroho ngumu aisee 😂😂😂😂😂
Ukiona mtu anakusifiasifia kila wakati ogopa mkuu kuna kitu anakitaka toka kwako.
Maana kadri utavyokenua ndivyo anakuwinda uwe "off guard" amalize mchezo
 
Halafu Kuna mendawazimu yanamsifu mshamba na Limbukeni .
 
Hi kodi ipo muda mrefu,Hoteli za mbugani ndio walikua wanalipa.Walikua wanaforce hoteli za mjini nao walipe.Ile ni kuongeza tu mzigo kwa wamiliki wa hoteli na kwa watalii.Hoteli industry ina kodi na tozo zaidi ya 12.
Kwa mjini kuna changamoto ya kujua nani mtalii nani kaja kikazi. Na wengine wanakuja kikazi halafu wanapiga utalii kidogo.
TRA wanaamini kila mzungu ni mtalii.
Definition ya sheria haisaidii kuweka wazi nani mtalii nani siyo.
Ugumu mwingine unakuja anapokuja mgeni kikazi halafu weekend anaenda day tour mbugani au town tour, anarudi kulala hoteli ileile. Sasa mwenye hotel atajuaje kuwa jamaa alienda kutalii!
 
Utekelezaji wake utakuwa mgumu aidha kwa wenye mahoteli ama kwa watalii. Ni vigumu kumwambia mtalii alipe gharama za chumba halafu alipe kodi ya kitanda atakacho lalia. Na ukifanyika utaratibu wa mwenye hoteli/nyumba yoyote ya wageni aingize kodi hiyo katika malipo ya chumba gharama za malazi zitakuwa juu na hapo ndio itakuwa chanzo cha kuharibika kwa biashara hasa kwa hoteli kubwa.
Watalii wanaoingia nchini sio kwamba wote ni matajiri huko kwao, asilimia kubwa huwa anaweka pesa kidogo kidogo kwa miaka hata mitano ili apate uwezo wa kutembelea nchi flani.
Na wengi wanatafuta nchi zenye gharama nafuu. Hivyo ni vyema serikali kuweka viwango na taratibu nzuri zenye unafuu kwa mtalii ili iwe moja ya kivutio cha watalii kuja kwa wingi.
 
I wish all accomodation facilities be listed accordingly without an overlook to boost Government Income.
 
Kwama hii sheria itaishia bara tu, tujiandae watalii wote kuishia Zanzibar. Ngoja tusubiri tuone Mwinyi maamuzi atakayo chukua kwenye sekta ya utalii Zanzibar ndio mtajua mwenye akili na mwenye elimu ni watu wawili tofaut
 
Nimeisoma hii habar kwenye gazeti la the citizen la Jana jumamosi 5/12/2020 ikiwa na kichwa " TRA receives updated list of taxable hotel facilities " nikagundua kwamba hii.kitu ilikuwepo mda mrefu sema sisi tulikuwa hatujui .

Tulieni tulieni tujenge nchi.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Sure Ndio maana kwa hotel let say Sinza na Manzese ambazo wazungu wachache hawakazi ulipo labda Waanze sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…