TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

Kwani hili baya, kupeana taarifa kuwa kuna kodi ya Kitanda Siku nayo nongwa au ni wakala wa mabeberu? Jamani kuweni na akili hata kidogo basi.
unamfuatilia erthrocyte lakni au umejisikia kuropoka tu??
Eti kuweni na akili ata kidogo; wewe unaakili??, yani darasa la saba halafu unavimba eti unauelewa😐
 
Usishangae sana mkuu. Watu wana chuki, tena wana chuki hadi kwa wanaowapa ulinzi wanapokua wamelala.

Kuna dada wa bongomovie aliwahi sema kwenye media hana mama, akadadavua mamake alishakufa ilihali mamake mzazi yuko hai na anamsikiliza sembuse huyu

Dunia inaenda kasi sana hii
Kati ya watu wanaoishi kwa hasira kutokana na siasa za chadema, ni mleta mada
 

Kutii Mamlaka​

Warumi13 Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

6 Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. 7 Walipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.
Nukuu ya uongo mkubwa.
 
Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede amepokea orodha ya huduma za malazi iliyoboreshwa 2020 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki ili kuiwezesha TRA kukusanya tozo ya Kitanda Siku kutoka kwa Watalii wanaotumia huduma za malazi.

View attachment 1641829

Hii ni katika harakati za kuongeza mapato
Hii kodi ilikuwepo tunaita Government Leavy na kila Mtalii akilala usiku mmoja analipia USDollar 1.5 sasa sijui hawa viumbe wamepandisha tena au wameshusha kwa ajili ya kuvutia Watalii?
 
Hivi dhana ya kudhani watalii wana hela nyingi sana tutaacha lini?? Wengine wanapenda kutembea na kujifunza au kupumzika na sio kua wana hela sana......serekani inaturudisha kwenye fikra kua mzungu yeyote ana hela sana
 
Kwa mwendo huo,tutegemee hata na wananchi kuja kulipia kile kitanda anachokilalia nyumbani kwake,kama kodi ya ardhi tunalipia kama wenye mahoteli,kama wao watalipia kitanda kwa nini mwananchi wa kawaida naye asilipie?
 
Ushawastua na itakuwa kubwa sana ili wapunguze watumiaji wa mitandao wanaomtusi na kumkejeli huyo anayejiita mwendawazimu 😂😂
Nchi inaendeshwa tuu kama gari bovu, hakuna sheria wala taratibu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede amepokea orodha ya huduma za malazi iliyoboreshwa 2020 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki ili kuiwezesha TRA kukusanya tozo ya Kitanda Siku kutoka kwa Watalii wanaotumia huduma za malazi.

View attachment 1641829

Hii ni katika harakati za kuongeza mapato
Hiyo kodi ya kitanda itakuwa kwa watalii peke yao? Loji, Gesti hazitalipa? Mwenyeji akilala kwenye hoteli ya kitalii hatalipa? Au ni kodi inayoendana na vitanda ambavyo vipo kwenye hoteli na sio watu waliolalia vitanda hivyo?

Amandla...
 
Back
Top Bottom