Shule ya St. JUDE wameifungia account zao kisa hawakupeleka watoto wao kwenye kampeni za CCM, kuimba mapambio kama shule nyingine.
Hii nchi kumpa huyu dereva lesseni ya kutuendesha, tumeingia chaka.
1) Mwenye kampuni ya kutembeza watalii, alipie kampuni yake kodi.
2) Na hayo magari yake ya kampuni ya watalii, alipie kodi.
3) Gari likiwekewa mafuta, unakutana na kodi.
4) Dereva nae, alipe kodi lesseni yake na ajira yake sambamba na kodi ya Trafic Police (Vijana wa kukusanya mapato TRA).
5) Mwenye hoteli wanaofikia watalii hao (Pengine mwenye kampuni ya utalii ndio hoteli yake pia), alipe kodi. Ndani ya hio hoteli yake anayoilipia kodi, chumbani kitanda nacho kikilaliwa, kilipiwe kodi.
Halafu serikali tunaambiwa haina hela. Shabaashi.
Wasisahau na KODI YA KUTUMIA VYOO KWA WATALII (Kama Vyoo Vya Kulipia Standi Za Bus).
Bora Mugalifu wao hana hayo mambo.
Mugafilu anazingatia haki za binadamu
Anazingatia utawala bora
Anazingatia utawala wa sheria
Hana upendeleo
Anazingatia usawa kwa kila mwananchi
Anazingatia ulaji sawa wa keki ya taifa.
Anawapenda sana wapinzani wake ikiwemo Tundu Lissu na Chadema kwa ujumla.
Anapenda sana kukubali kukosolewa
Ni msikivu wa kiwango cha rami.
Anazingatia misingi ya ukuzaji uchumi
Anazitumia vizuri pesa mabeberu(wanaume wachapakazi wa Uraya)
Anahakikisha afya za wananchi zinastawi
Ana ruhusu upatikana wa habari hata zile zinazomkosoa.
Anazingatia uwepo wa usalama wa kila mwananchi hata uwe wa Chadema.
Amekuwa kiongozi wa mfano ulimwenguni hata serikali za peponi zinajitahidi kumuiga yeye.
Anazingatia kutokuwepo kwa wasaliti duniani kwa kuwapa ulinzi(Tundu Lissu amiminiwa marisasi huko Dodoma)
Mambo ni mengi muda mchache
Kidumu chama chetu chakavu cha mapinduzi kisichojali tena matatizo ya wananchi.
Kigumu chama kinacho impoverish watanzania kwa speed ya mwanga.