Ngoja nichanganue hili sakata kwa nilivyoelewa mimi.
Mfanyabiashara Ameingiza bidhaa zake nchini kupitia kampuni ya tosh cargo
Tosh cargo amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha na kukabishi mzigo kwa mteja wake.
Shida inaanzia hapo kwenye (Amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha)
Wakati mfanyabiashara anapelekea mzigo wake huko unapotakiwa kwenda gari ikapata ajali na kusababisha uharibifu na upotevu wa mali.
Kwakua mfanyabiashara alikua na bima, akaanza mchakato kufatilia ili apate fidia ya mali yake iliyoharibiwa na tukio la ajali.
Kampuni ya bima inawajibika kumlipa mteja wake, lakini kabla hawajamlipa lazima wapate nyaraka zote muhimu kuhusu mali zilizopotea, ikiwa ni pamoja na nyaraka zote halali za kikodi na mengineyo ili wapate uhakika wa thamani na uhalali wa wanachoenda kulipa.
Sakata linaanzia hapa kwenye nyaraka.
TRA hawatambui mali ya mlalamikaji, kwanini hawaitambui na hawajaiona kwenye mfumo?
Kuna mawili hapa;
1. Tosh cargo wameingiza mzigo kama mali yao, hivyo mteja mwenye mzigo hatambuliki na mfumo mzima wa TRA.
2. Rejea namba moja 😂, kama mfumo haukusomi basi unamsoma aliekamilisha clearance ya mzigo.
Kama Nyaraka za TRA hazikutambui kampuni ya Bima itakufidia vipi na umeshindwa kutoa vielelezo vya uhalali wa mali iliyoharibika, vipi kama umekula njama na mtu baki utumie mgongo wa mali yake iliyoharibika kujipatia bima kwa njia ya udanganyifu?
Swali jingine la msingi kwa mfanyabiashara.
Asijekua anataka huruma ilhali nayeye anajua fika changamoto ambazo zingejitokeza.
Je kabla ya kupata matatizo yote ya ajali n.k, aliridhika na nyaraka zote alizokabidhiwa baada ya kupewa mizigo yake, au akili imekuja kukaa sawa baada ya matatizo?