Traffic police ni janga la kitaifa, wanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi

Traffic police ni janga la kitaifa, wanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi

Watu wamejawa na hofu ndani ya taifa lao, yaani dereva akiona mtu yeyote mbele kuleee kavaa nguo nyeupe/kanzu mapigo yake ya moyo yanabadilika akidhani ni traffic polisi, aandae pesa.
Hahahahha ni huyo mimi aisee😂😂😂
 
Wellcome to police state, katiba mpya ingetuletea kitu inaitwa IPID, hawa ni police wenye uwezo wa to arrest their own, wewe unapoona hujatendewa haki let's say mikumi check point, unalenga kituo cha police pale mikumi na kumfungulia mashitaka, IPID watachunguza even do arrest kwa suspect, kwa sasa bado sana....ILA nimeota kuwa Botswana 🇧🇼 police wote watakuja kufanya kazi Tanzania, na hawa wa kwetu wataenda Botswana!!no just kidding mkuu ila tuna safari ndefu na tusitegemee watu watupiganie mkuu
Nadhani unaongelea kujaribu serikali ya Chama kingine, au?
 
Bei ya mafuta imepanda sana, mishahara ni midogo sana na bidhaa zote sokoni zimepanda kwa kila mtu duniani wakiwemo hata polisi traffic.

Polisi wanazidisha ugumu wa hali hii kwa njia ya kutafuta makosa kwa wenye magari na wasafirishaji wa abiria na mizigo, hali inayosababisha gharama kubwa za usafiri na usafirishaji mijini na barabarani. Ukiendesha gari lazima uwe na hela ya askari barabarani, kwanini iwe hivi?

Wanatekeleza ukatili huu kwa njia zifuatazo.
1. Wanaanza msako wa magari yenye kasoro ndogondogo na madeni ya kubambikia ambayo hayalipwa kuanzia asubuhi kabisa wakati ule watu wanawahi kwenda kazini. Jambo hili linachelewesha watumishi, wafanyabiashara, wanafunzi, wasafiri wa mikoani na wagonjwa kufika kwa wakati waendako.
2. Kuwapiga fine madereva au kudai kitu kidogo ili kuwasamehe. Makosa yenyewe ni hata ukikosa triangle moja kati ya mbili, mkwaruzo kwenye gari.

3. Kujificha vichakani na kupiga picha kwa kificho magari yaendayo spidi na kurusha picha hizo kwa wenzao mbele ambao watakudai kitu wakuachie uendelee na safari yako, wanakuchelewesha njiani bila sababu za msingi. Yaani nililipishwa kitu kidogo kwa spidi ya mwendo wa km 54/hr. Njia zote za kwenda mikoani zimejaa viota vya kujifichia askari hawa wasioonekana njiani.

3. Pikipiki za maguta, bodaboda, kirikuu na gari za mizigo wanatembea roho juu kwenye nchi Yao wenyewe, askari wanaondoka na faida yote unayotarajia kuipata kwenye mzigo huo. Huu ni wizi sawa na wizi mwingine TU.

4. Watoto wanachanganyikiwa, shuleni wanafundishwa kuwa taa nyekundu simama, lakini wanapofika barabarani sio hivyo, traffic wanaruhusu magari kwenye taa nyekundu na kusimamisha kwenye taa ya njano na kijani, hadi inakuwa kero.

Ugumu wa maisha unazidishwa na hawa watu bila sababu za msingi. Wanaichonganisha serikali na raia wake, ili maisha ya mpiga kura wa kawaida yawe magumu sana.

Mama yetu tusaidie hili pia.
Hujafuatilia vizuri. KM wa Chama kakizungumzia Hilo suala na kutoa ushauri murua.
 
Kuwapiga fine madereva au kudai kitu kidogo ili kuwasamehe.
Kuna kipindi nilikuwa nasafirisha vitunguu kutoka Iringa kuja Dar. Gari ikakamatwa eti vitunguu vimezidi uzito kwa gunia.
Nikamwambia dereva ayashushe magunia hapo Mikese. Nikajua nikifika hapo baada ya siku tatu nikawaambia wapime uzito, watashangaa wenyewe na roho zao.
Bahati nzuri dereva 'aliyajenga' wakamruhusu kuendelea na safari...
 
Kinashangaza sana, gari Imeandikwa inapiga safari kutoka Dar kwenda Mkuranga...Sasa ajabu gari itasimamishwa vituo zaidi ya Saba inakaguliwa vitu vilevile kila kituo.

Mimi nafikiria Traffic waweze kufanya synchronization ya taarifa zao kuhusu gari husika ili wale wa mbele waone taarifa ya gari husika...hii kazi ya traffic ya kuwa na Mashine ya kukusanya mapata kwakweli inafikirisha sana.
 
Nadhani unaongelea kujaribu serikali ya Chama kingine, au?
Nope mkuu, katiba mpya haina vyama, ipo kwa ajili ya watanzania na katiba hii pia itatupatia strong judiciary na bunge, means hii chop chop,hii ndio ndio haitokuwepo!
 
. Pikipiki za maguta, bodaboda, kirikuu na gari za mizigo wanatembea roho juu kwenye nchi Yao wenyewe, askari wanaondoka na faida yote unayotarajia kuipata kwenye mzigo huo. Huu ni wizi sawa na wizi mwingine TU.
Kinana amewasema juzi tu jana nimewakuta barabarani Dar to Iringa na yaleyale, kuna Rais miaka ya nyuma katika nchi moja aliwaambia askari mnalalamika maisha magumu wakati mna bunduki, hiki ndicho kipo anzania hivi sasa, traffic wanawapora wananchi fedha zao kwa kutumia sare zao
 
Unakuta kibao ni 50KPH wewe ukitembea 51KPH unaambiwa umezidisha mwendo na aidha uwape kitu kdg au wakuandikie fini 30,000 badala ya kuonya kwa vikosa vidogo. Hwa jamaa hapana!
Kwanza 51km/hr, hujazidisha. Kuna kitu kinaitwa instrument error. Kamera ya polisi,, kama inafanya kazi sawasawa, ina instrument error isiyozidi 10%.

Kwa hiyo instrument error ambayo mtengenezaji ameiruhusu ni kwamba camera inaposoma 55km/hr, inaweza kuwa ni 50km/hr au 60km/hr au soeed yoyote katika boundaries hizo. Ndiyo maana gari yoyote ambayo camera imeisoma inakwenda kwa speed ya 55km/hr, kiuhalisia haitakiwi kuadhibiwa.

Usikubali kulipa faini wala kuandikiwa ka speed yako haijazidi 55km/hr.
 
Bei ya mafuta imepanda sana, mishahara ni midogo sana na bidhaa zote sokoni zimepanda kwa kila mtu duniani wakiwemo hata polisi traffic.

Polisi wanazidisha ugumu wa hali hii kwa njia ya kutafuta makosa kwa wenye magari na wasafirishaji wa abiria na mizigo, hali inayosababisha gharama kubwa za usafiri na usafirishaji mijini na barabarani. Ukiendesha gari lazima uwe na hela ya askari barabarani, kwanini iwe hivi?

Wanatekeleza ukatili huu kwa njia zifuatazo.
1. Wanaanza msako wa magari yenye kasoro ndogondogo na madeni ya kubambikia ambayo hayalipwa kuanzia asubuhi kabisa wakati ule watu wanawahi kwenda kazini. Jambo hili linachelewesha watumishi, wafanyabiashara, wanafunzi, wasafiri wa mikoani na wagonjwa kufika kwa wakati waendako.
2. Kuwapiga fine madereva au kudai kitu kidogo ili kuwasamehe. Makosa yenyewe ni hata ukikosa triangle moja kati ya mbili, mkwaruzo kwenye gari.

3. Kujificha vichakani na kupiga picha kwa kificho magari yaendayo spidi na kurusha picha hizo kwa wenzao mbele ambao watakudai kitu wakuachie uendelee na safari yako, wanakuchelewesha njiani bila sababu za msingi. Yaani nililipishwa kitu kidogo kwa spidi ya mwendo wa km 54/hr. Njia zote za kwenda mikoani zimejaa viota vya kujifichia askari hawa wasioonekana njiani.

3. Pikipiki za maguta, bodaboda, kirikuu na gari za mizigo wanatembea roho juu kwenye nchi Yao wenyewe, askari wanaondoka na faida yote unayotarajia kuipata kwenye mzigo huo. Huu ni wizi sawa na wizi mwingine TU.

4. Watoto wanachanganyikiwa, shuleni wanafundishwa kuwa taa nyekundu simama, lakini wanapofika barabarani sio hivyo, traffic wanaruhusu magari kwenye taa nyekundu na kusimamisha kwenye taa ya njano na kijani, hadi inakuwa kero.

Ugumu wa maisha unazidishwa na hawa watu bila sababu za msingi. Wanaichonganisha serikali na raia wake, ili maisha ya mpiga kura wa kawaida yawe magumu sana.

Mama yetu tusaidie hili pia.
Mh Rais anasema na kutenda!Alipoteta na polisi pale mwanzo kuhusu yeye kushikwa kwa kosa la taa tu,nilifurahi na kuamini kuwa sasa trafiki wangeenda kubadilika..wapi!
Mzee Kinana kajitosa kupasua jipu la trafiki...kongole!trafiki wanasema huu ni upepo tu.Tiss, Takukuru,n.k msaidieni mkuu wa nchi kuondoa aibu hii!
 
Kinashangaza sana, gari Imeandikwa inapiga safari kutoka Dar kwenda Mkuranga...Sasa ajabu gari itasimamishwa vituo zaidi ya Saba inakaguliwa vitu vilevile kila kituo.

Mimi nafikiria Traffic waweze kufanya synchronization ya taarifa zao kuhusu gari husika ili wale wa mbele waone taarifa ya gari husika...hii kazi ya traffic ya kuwa na Mashine ya kukusanya mapata kwakweli inafikirisha sana.
Tena wanakuuliza kabisa tukuandikie au unamaliza...!!?. Mwingine juzikati kaniomba hela nikamwambia sina, akageuka kutaka leseni na kaniandikia makosa mawili 1. Gari bovu. 2. Failure to comply with road sijui nn daaah ... Hapa mkeka una siku 4 sijaulipa naugulia ndani ndani tuu maana elfu kumi imenitandikia keka LA 60..
 
Vitendo hivi hakuna asiyevijua, watu Wana wasiwasi ya kuendesha magari Yao ndani ya taifa lao wenyewe. Eti utembee na hela ya kuwalipa polisi kipumbavu kabisa.
Fedha zinakunjwa kunjwa ndani vipande vya karatasi ambayo ni uharibifu wa sarafu zenyewe,wanatupiwa nao wanaokota; Wanajidhalilisha.

Police waache kupokea RUSHWA na wanatakiwa kuwajibika.Hizo Rushwa ndiyo chanzo cha ajali za barabarani.
 
Kipimo kikuu cha mafanikio ya mapambano dhidi ya rushwa ni kupungua au kwisha kwa rushwa ya traffic police!
Hivi nani hajui hawa jamaa ni wala rushwa?
 
Utafanya nini mkuu, hata Rais analifahamu hili? Hata jaji mkuu analifahamu hili? Hata IGP analijua. Utapeleka kwa nani?
wao wanajulia wapi angali zao spidi kuliko na saluti juu
 
Tena wanakuuliza kabisa tukuandikie au unamaliza...!!?. Mwingine juzikati kaniomba hela nikamwambia sina, akageuka kutaka leseni na kaniandikia makosa mawili 1. Gari bovu. 2. Failure to comply with road sijui nn daaah ... Hapa mkeka una siku 4 sijaulipa naugulia ndani ndani tuu maana elfu kumi imenitandikia keka LA 60..
Cha kushangaza nchi ina takukuru na wanakula salary kama kawa

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom