Traffic police ni janga la kitaifa, wanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi

Traffic police ni janga la kitaifa, wanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi

Unakuta kibao ni 50KPH wewe ukitembea 51KPH unaambiwa umezidisha mwendo na aidha uwape kitu kdg au wakuandikie fini 30,000 badala ya kuonya kwa vikosa vidogo. Hwa jamaa hapana!
Ila kama ni 50 we ukapiga 51 unakuwa umezidisha mkuu
 
Kuna kipindi nilikuwa nasafirisha vitunguu kutoka Iringa kuja Dar. Gari ikakamatwa eti vitunguu vimezidi uzito kwa gunia.
Nikamwambia dereva ayashushe magunia hapo Mikese. Nikajua nikifika hapo baada ya siku tatu nikawaambia wapime uzito, watashangaa wenyewe na roho zao.
Bahati nzuri dereva 'aliyajenga' wakamruhusu kuendelea na safari...
Kitu kidogo kimepunguza uzito wa vitunguu safari ikaendelea.
 
Kinashangaza sana, gari Imeandikwa inapiga safari kutoka Dar kwenda Mkuranga...Sasa ajabu gari itasimamishwa vituo zaidi ya Saba inakaguliwa vitu vilevile kila kituo.

Mimi nafikiria Traffic waweze kufanya synchronization ya taarifa zao kuhusu gari husika ili wale wa mbele waone taarifa ya gari husika...hii kazi ya traffic ya kuwa na Mashine ya kukusanya mapata kwakweli inafikirisha sana.
Yaani njia nzima traffic ni yeye TU, wengine huko nyuma hawaaminik
 
Tena wanakuuliza kabisa tukuandikie au unamaliza...!!?. Mwingine juzikati kaniomba hela nikamwambia sina, akageuka kutaka leseni na kaniandikia makosa mawili 1. Gari bovu. 2. Failure to comply with road sijui nn daaah ... Hapa mkeka una siku 4 sijaulipa naugulia ndani ndani tuu maana elfu kumi imenitandikia keka LA 60..
Traffic anasahau kuwa maisha ni magumu hata kwa wengine.
 
Fedha zinakunjwa kunjwa ndani vipande vya karatasi ambayo ni uharibifu wa sarafu zenyewe,wanatupiwa nao wanaokota;Wanajidhalilisha.
Police waache kupokea RUSHWA na wanatakiwa kuwajibika.Hizo Rushwa ndiyo chanzo cha ajali za barabarani.
Traffic wa Gongo La Mboto wanakwambia pesa peleka pale kwa shoe shiner nitazikuta hapo.
 
Kwanza 51km/hr, hujazidisha. Kuna kitu kinaitwa instrument error. Kamera ya polisi,, kama inafanya kazi sawasawa, ina instrument error isiyozidi 10%.

Kwa hiyo instrument error ambayo mtengenezaji ameiruhusu ni kwamba camera inaposoma 55km/hr, inaweza kuwa ni 50km/hr au 60km/hr au soeed yoyote katika boundaries hizo. Ndiyo maana gari yoyote ambayo camera imeisoma inakwenda kwa speed ya 55km/hr, kiuhalisia haitakiwi kuadhibiwa.

Usikubali kulipa faini wala kuandikiwa ka speed yako haijazidi 55km/hr.
Badala yake ufanye nini? maana hawa jamaa wanakwambia lete leseni yako halafu wanaondoka nayo kwenda kibandani kwao ili uwafuate huko,
 
Back
Top Bottom