Trafiki kama kupita service road ni makosa basi muwaambie Tanroads wasizijenge

Trafiki kama kupita service road ni makosa basi muwaambie Tanroads wasizijenge

Nashangaa sana haya mambo wanayofanya hasa hapa Mbezi Beach Massana mpaka Tanki Bovu gari ikipita service road wanaikamata.

Nauliza ile barabara matumizi yake ni nini?
Matumizi yake ni kupiga madereva faini
 
Naomba nianze kwa masikitiko makubwa, kuwa askari wetu wamekuwa wanatumia hizi service roads kutengeneza pesa tena si pato la taifa bali maslahi yao maana wengi wanaowakamata wanaoshia kuwahonga.

TANROADS wamefanya vizuri sana kwenye hii Bagamoyo road, wanapanua kwa kuongeza service roads ambazo zingepunguza foleni lakini Askari wetu wanazitumia kama fursa kwao.

Tufike mahali watanzania tufanye kazi kizalendo na si kimaslahi,

Cha kuchekesha unakuta mainroads kuna foleni iliyojaa kweli halafu askari wetu wako mstari wa mbele kukamata wanaopita service roads, wakati kwa akili yangu ndogo tu, polisi wetu wangetumia service roads kama fursa ya kupunguza foleni.

Inasikitisha uzalendo uko wapi?
 
Katika idara ya polisi inayotakiwa kufumuliwa ni hii idara ya polisi wa usalama barabarani hawa ni donda sugu hasa katika kudai na kupokea ruswa.

Service Road zimekuwa kero hasa kwa madereva.

Morogoro road maeneo ya bucha na rombo ukipita salama basi mungu wako mkubwa.

Ifike mahala trafiki watumie akili tu maana wengi tunajua PGO zero lakini kupunguza msongamano wa magari pindi kunapotekea ajali.

Unaweza kukuta gari limeharibika main road na karibu tu kuna service road unajiuliza kwanini asingetumia njia hiyo.

Kumbe wanaogopa faini za kijinga. TRAFIKI NI TATIZO.

Wapo pale Shekilango karibu na kituo na wapo hapa Ubungo Tanesco.

Jana nilipanda daladala tumesimamishwa mara 5 tena asubuhi.
 
Fala sana hao jana wamenizingua nikamwambia naingia sheli Puma. Tukasumbuana na yule dada eti park gari nikamwambia nawai ofisini wewe chukua namba ya gari na namba nitakuja ofisini. Nikasepa
Umeona yaaan kama hawajielewi kabisa mimi mwenyewe nimekutana nao nikawaambia na haraka kama vipi niwaachie gari na ufunguo ntalikuta kituoni wakaogopa
 
Kuna ile ya Africana inayopita kwenye ghorofa la urithi la Mange Kimambi duh yule Awadh alitutesa sana!

Alishanikamata zaidi ya mara 10 baadae tukawa marafiki tu.

Hapo Shule kwa dogo janja huwa napita kama sijauona mkono vile!
He he heeee
 
Unajua maana ya service road? Au hujui kiingereza
AE65AC7D-D894-4B8D-B0E1-CDFD97BB6DEA.png
 
Katika idara ya polisi inayotakiwa kufumuliwa ni hii idara ya polisi wa usalama barabarani hawa ni donda sugu hasa katika kudai na kupokea ruswa. Service Road zimekuwa kero hasa kwa madereva. Morogoro road maeneo ya bucha na rombo ukipita salama basi mungu wako mkubwa.

Ifike mahala trafiki watumie akili tu maana wengi tunajua PGO zero lakini kupunguza msongamano wa magari pindi kunapotekea ajali. Unaweza kukuta gari limeharibika main road na karibu tu kuna service road unajiuliza kwanini asingetumia njia hiyo.

Kumbe wanaogopa faini za kijinga. TRAFIKI NI TATIZO. Wapo pale Shekilango karibu na kituo na wapo hapa Ubungo Tanesco. Jana nilipanda daladala tumesimamishwa mara 5 tena asubuhi.
Sirro alifumie tu jeshi lake
 
Nashangaa sana haya mambo wanayofanya hasa hapa Mbezi Beach Massana mpaka Tanki Bovu gari ikipita service road wanaikamata.

Nauliza ile barabara matumizi yake ni nini?
Ni mtego wa pesa ya kiwi
 
Back
Top Bottom