Naomba nianze kwa masikitiko makubwa, kuwa askari wetu wamekuwa wanatumia hizi service roads kutengeneza pesa tena si pato la taifa bali maslahi yao maana wengi wanaowakamata wanaoshia kuwahonga.
TANROADS wamefanya vizuri sana kwenye hii Bagamoyo road, wanapanua kwa kuongeza service roads ambazo zingepunguza foleni lakini Askari wetu wanazitumia kama fursa kwao.
Tufike mahali watanzania tufanye kazi kizalendo na si kimaslahi,
Cha kuchekesha unakuta mainroads kuna foleni iliyojaa kweli halafu askari wetu wako mstari wa mbele kukamata wanaopita service roads, wakati kwa akili yangu ndogo tu, polisi wetu wangetumia service roads kama fursa ya kupunguza foleni.
Inasikitisha uzalendo uko wapi?