Matumizi sahihi ya sheria yanahitaji mambo matatu.
1. Sheria lazima imtumikie binaadam sio binaadam aitumikie sheria (yaani sheria ilenge katika kupunguza au kuondoa matatizo ya binaadam)
2. Uelewa wa faida na hasara za matumizi ya sheria husika.
3. Mazingira husika.
Utekelezaji wa sheria wa polisi hapa kwetu hauzingatii mambo hayo.
Kwa mfano, unapita kwenye high way, unakutana na kijiji, hakuna alama yoyote kuhusu spidi kwenye Kijiji hicho, mbele trafiki anakukamata ume overspeed kea kwenda spidi 60 badala ya 50. Unamjibu sijaona alama yoyote inayoniambia nipitie eneo hili kwa spidi ngapi? Anakujibu huoni kama ni makazi ya watu? Anasisitiza makazi yote ya watu hutakiwi kwenda spidi zaidi ya 50! Vitu viwili vinakujia kichwani mwako, ni sheria ipo hiyo iliyosema hivyo na kama ipo je, maeneo yote ya mijini hakuna alama za spidi? (Maana ni makazi ya watu). Huu mfano wa kwanza; kuna shida kea jeshi la polisi Tanzania pamoja na hao trafiki.
Mfano, mwingine unapita kwenye high way, unakutana na alama inayooshesha magari yamezuiwa kulipita lingine (overtaking), lakini ukiwa unaendelea na hilo agizo, unaona alama za mstari zikiruhusu ku overtake. Kubwa kuliko yote, utaendesha ukitafuta hilo zuio linaishia wapi! Hautakuja kuona.
Unapita highway, unakuta huu upande unaondesha una shimo kubwa kiasi itakulazimu upite upande wa kulia kwako. Unfortunately, kwa kufanya hivyo unavuka mstari unaozuia ku-overtake eneo hilo. Kumbe mbele tu, Askari wamejibana kuvizia wanaofanya huo mchezo Ili wawapige fine. Mifano ni mingi inayoonyesha kuna shida kubwa kwa kikosi hicho. Kinafanya kazi kwa elements zote za kitumwa. Hawajali kumpotezea mtu muda hata kidogo.
Mfano mwingine. Siku moja (siku nyingi kidogo, kiasi miaka 10-15 nyuma) nilipata simu ya dharura so nikalazimika kutoka Dar saa 7 usiku kwenda Tanga kupitia chalinze. Nilipofika Ruvu, kuna askari amenisimamisha na kuniambia amejulishwa kwamba mi mine overtake kwenye zebra huko nilikotoka. Najaribu kufikiria, ule muda kwanza hakukuwa na magari ya ku-overtake kihivyo, lakini hizo zebra zenye wavukaji kwa saa 8 ile usiku wanataka wapi. Na for sure hakukuwa na kitu hicho. Nikamwambia nipe ushahidi wa usemacho na usiponipa nakushtaki wewe. Akasema sawa ngoja aje aliyekuona. Nikasubiri kama nusu saa, huyo askari mwingine asitokee. Akaja ukiniambia huyo jamaa yake anachelewa hivyo ananiomba niondoke tu amanisamehe. Nikamwambia umenisamehe kwani nilifanya kosa? Mimi siondoki Hadi huyo mtu aliyeniona nimetenda hayo makosa aje kama vipi nitakupeleka Mahakamani. Ikabidi aanze kuniomba niridhie kuondoka. Nikaondoka lakini ashaharibu ratiba zangu. Hawa watu ni hovyohovyo sana. They don't care na maisha wala uchumi wa nchi. Wanajali maatumbo yao tu.
So unapolinganisha nchi za Ulaya/America na nchi zetu, inabidi uwe makini kidogo. Mazingira ya barabara katika nchi hizo, hayakupi nafasi ya kufanya makosa ya kipuuzi, hiyo tofauti na kwetu. Lakini hata watu wenyewe waliopo barabarani na miundombinu yake ni tofauti.
Matatizo mengi katika jamii yanatatuliwa na mfumo, lakini mfumo wowote unahitaji watu wenye Elimu na uelewa wa kutosha. Hatua ya mwanzo ya kubadili jeshi la polisi na hasa usalama barabarani ni kuajiri vijana wenye Elimu nzuri sio hizi dhana za kuajiri waliofeli. Kinyume cha hivi, nothing tangible will be achieved.