Trafiki wanafanya kazi kubwa, wapongezwe

Trafiki wanafanya kazi kubwa, wapongezwe

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Katika hali isiyo ya kawaida na ambayo haijawa kutokea toka tupate Uhuru Tanganyika na baadae Tanzania , Polisi wa Usalama Barabarani toka mwaka 2015 wamefanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu.

Mwaka 2017 Mpwendwa Wetu Rais JPM aliona mateso yao na kuruhusu kuchukua shekheli ya ku-futia viatu.
Mwaka 2017,2018 idara hii ya usalama barabarani ikaanza kutangaza mapato kwa mbwembwe na majigambo yasiyo ya kifani.

Sasa, idara hii IMEHAMIA BARABARANI KILA ASUBUHI, HASA VITUO VYA MABASI NA DALADALA, tunawapongeza sana, hongereni ASKARI WETU MNAOVAA NGUO NYEUPE kuashiria USAFI NA UTAKATIFU.

Askari hawa kila GARI LINASIMAMISHWA, anashuka utingo gari linapaki kwa mbele kidogo, konda anachukua ticketi yake (ya daladala yake) anachukua mfukoni mwake KITU KINACHOFANANA NA Tshs 2000 [elfu mbili] na kuifunga na ile ticketi, anampa yule malaika aliyevaa nguo nyeupe za "utakatifu"

Tunawapongeza sana ndugu zetu kikosi hiki, Watanzania wanauliza, wana maswali yafuatayo:-

1. Kwanini gari/daladala unaiacha ipite, utingo abaki na kukupa hicho ki-tiketi kilichofungiwa na kitu kinachofanana na 2000?
2. Kwanini hawakagui gari badala yake wanapokea vikaratasi?
3. Kwanini kila gari ambalo hawawapi vikaratasi wanaandika majina yao kwenye daftari lisilo la serikali na kupeana namba za simu?
4. Kwanini daladala zimeongeza "mabenchi ya mbao" kwenye ule uwazi katikati na "malaika hawa" hawasemi kitu?
5. Kwanini wanataka kuwabebesha watoto na fasmilia zao laana kwa kuwalisha haramu?
6. Kweli hizo zinazokusanywa, kama ni karatasi zinazofanana na 2000 ni wao wamejiamulia ama kuna mtu juu yao "msafi zaidi" kawatuma?
7. Kwanini trafiki kague gari badala ya vehicle inspector?
8. Kwanini baadhi ya magari hayakamatwi kabisa, tena wanapungiana na "hawa malaika" hata kama yafanye kosa la aina gani?
9. Kwani Waziri na Sirro hawa watu wanawahusu? Wana simamiwa kweli? Wako wapi akina Jerry Muro wa kuhoji hizo vitu vinavyofanana na fedha kila siku asubuhi kukusnywa nchi nzima?

Note: Kesho asubuhi kwa wale wanaoingia Stendi ya MAKUMBUSHO-DAR angalia kila kondakta akisimamishwa, anachukua tiketi, anatoa kitu kinachofanana na 2000, anachanganya na kumpa "malaika"

Mungu anasema "TOSHEKENI NA MISHAHARA YENU"
 
Kukaa kwenye jua kali siku nzima na hii vumbi sio jambo dogo mkuu.

Waache tu wakanywe maziwa. Ila wajichunge wasipate vitambi.
 
Ukweli wajasiriamali tuliowekeza kwenye usafirishaji watu na mizigo tunagawana faida na serikali (Kodi ya mapato) na hawa trafick police

Ukiwa na gari hizi wewe unalisha familia za traffic police
1.Daladala
2.canter
3.Fuso
4.lori zinazobeba containers
5. Suzuki Carry (hizi hazitoboi hasa ikiwa imebeba mzigo)
6.Basi zinazopiga ruti fupi
 
nawewe unazoficha kazini kwako nani anakuona[emoji16][emoji16][emoji16].

siku ya hukumu polisi na wafiraji watasamehewa sababu wanaowanyooshea vidore wamesahahu dhambi zao.
 
Back
Top Bottom