Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Polisi Trafiki watatu walikamtwa jana Alhamisi 30/11/2023 asubuhi eneo ambalo maafisa wa kupambana na rushwa walisema ni maarufu kwa kukusanyia rushwa kando ya Barabara ya Mai Mahiu katika makutano ya Karagita huko Naivasha, Kaunti ya Nakuru
Kulingana na Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa (EACC), afisa mwingine alikataa kujisalimisha na kukimbia huku akifyatua risasi kuzuia maafisa hao wa uchunguzi walokuwa wanamfuatilia. Hakuna majeruhi yaliyorekodiwa kutokana na majibizano hayo ya risasi, imesema shirika hilo.
Maafisa wa uchunguzi walipata ganda la risasi wakati wanawasafirisha matrafiki waliopokea rushwa kutoka Naivasha kwenye Kituo cha Polisi cha Tume hiyo kwaajili ya kutoa maelezo.
Afisa Trafiki watatu waliokamatawa wakipokea rushwa katika makao makuu ya EACC kwa ajili ya kuandikisha maelezo kabla ya kufikishwa mahakamani.
Citizens Digital