Avriel
JF-Expert Member
- Jun 25, 2017
- 4,950
- 5,378
Kuna familia za ajabu ndugu.Unasema atakuoa kwa siri.? Ina maana hata familia yako utaifanyia siri juu ya hilo swala?
Kwanini nimesema familia yako, kwasababu siku zote wazazi wetu wanatutakia yaliyo mema kwenye maisha yetu, sidhani kama familia yako itakubali uolewe nae endapo wakijua status ya huyu bwana.......Nachotaka kusema ni kwamba achana na hizo danganya toto za Mume wa mtu!!
Anyway wewe ndio muamuzi wa mwsho katika hili.
Wanasapoti hizi ndoa za Siri wao kikubwa binti yao aolewe na inawezekana binti akagharamia mchongo mzima wa harusi.
Nimeshuhudia kwa macho yangu.
Mdada kajigharamia kila kitu cha ndoa, huyu jamaa huwa namuuliza umeoa au umeolewa ananichukia kinyama. Na ndoa walishiriki upande wa mwanamke pekee japo mama wa jamaa alijua ila kuondoa Shari hakutokea eneo la tukio maana jamaa aliacha mke mwingine ndani akaaga anaenda kikazi kumbe anaenda kuoa sijui ndio kuolewa kisiri. Mpaka Sasa yuko ndoani huko alikoolewa, bahati nzuri akaolewa na wanae na ukoo mzima ukahamia kws huyo mwanamke.
Dunia ina mengi hii.