TRC, Chukueni Ushauri Huu na Wenye Mabasi someni hapa

TRC, Chukueni Ushauri Huu na Wenye Mabasi someni hapa

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Kwanza ndugu Kadogosa na ofisi yako ya Tanzania Railways Corp hadi hapo hongereni kwa hatua hiyo japo no kwa kuchelewa sana.

20240613_184805.jpg
Nimepitia ratiba yenu kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafirishaji abilia, hadi mlipoamua kupachika hii banner ni mmejiridhisha sawasawa.

Mmetoa muda wa kutoka Dar saa kumi na mbili asubuhi ambao kwa maoni yangu mlipaswa kuanza mapema zaidi ya hapo.

Na kutoka Morogoro mlipaswa kuweka train nyingine kwa muda huo huo zikiwa zinapishana, kuepusha delaying hapo kati.

Au ndiyo mnaanza hivyo mnasoma upepo ila kama mmeanza jumla basi inabidi kuweka usafiri wa usiku kama kwenye mabasi huko.

MABASI; kwa upande wenu wenye makampuni nawashauri Starting Point yenu badala Dar Es Salaam, sasa ianzie Morogoro, hii ni kwa basi zinazokwenda mikoa ya kanda ya kati, kanda ya ziwa, magharibi nk.

Hapo mtakuwa mmesave muda na pesa kwa kipande cha Dar - Moro, 4hrs ni muda mrefu sana kwa basi hivyo abilia wenu mkiwachukulia Moro mkasonga mbele hapo mtakuwa mnaneemeka.
 
TRC, tafadhali fanyeni hivi, train ikinyanyuka Dar kwenda Morogoro,muda huo huo nyingine inyanyuke Morogoro kwenda Dar.

Kila ikitoka upande Moja wa nchi nyingine itoke upande meingine kwa muda ule ule.

Ninashauri ticket zikatwe online, na anayekata tiketi za tarehe za mbali apate discount automatic.

Iwepo pia train ya express kwenda na kurudi moro
 
Yaani wewe washauri watu wa treni, mabasi hamna ushauri umewapa hapo. Mabasi kila starting point yake ina basi kwa muda husika. Anayepanda basi dodoma saa 12 muda huohuo wa dar anapanda pia.
 
Haya sasa muda wa maafisa masoko na ushauri wa trc kumwaga nondo.
 
Nahisi Kuna njia Moja tu ambayo hawaezi kupishana
Wamejenga njia moja tu kama zamani dunia ya sasa? BTW kama ni hivyo, bado wanaweza kupishana katikatika kwa kutumia reli za mchepuko mradi timing iwepo. Ila uendeshaji wa namna hii ni changamoto kwani treni moja ikichelewa inabidi nyingine isubiri.
 
Kwahiyo wa Chalinze watembee kwa mguu huku wa Dar Mwanza utawalipia wewe nauli mpaka Moro!
Uko baa gani nije tushauriane.
Tatizo utoto nao unachangia akili kuwaza maziwa tu!.

Umesoma wapi nimeandika 'mabasi yote lazima yaanzie' au hujui maana ya 'ushauri' na nani kakwambia usafiri wa Dar - Moro kwa njia ya bus hautakuwepo?.
 
Mnaosema train moja itoke Moro ingine Dar
Watapishana vipi hapo kati na rail iko moja em tujuzeni sisi washamba
Zinapishana stesheni. Mfano Inayotoka Dar saa 0700 inahskikisha saa 0745 iko Soga, na inayotoka Moro saa 0715 inahakikisha saa 0745 iko Soga.

Hapo ndio zinapishana kila mmoja anaendelea.

Kifupi zinapisha kwenye stesheni. Watu wa logistics and signals wanapanga kila kitu.

Mtu wa signal akizungua zinapigana mzinga.
 
Zinapishana stesheni. Mfano Inayotoka Dar saa 0700 inahskikisha saa 0745 iko Soga, na inayotoka Moro saa 0715 inahakikisha saa 0745 iko Soga.

Hapo ndio zinapishana kila mmoja anaendelea.

Kifupi zinapisha kwenye stesheni. Watu wa logistics and signals wanapanga kila kitu.

Mtu wa signal akizungua zinapigana mzinga.
Ooh kumbe ni kama matreni mengine haya tuliozea
 
Back
Top Bottom