TRC: Kulitokea hujuma katika Treni ya Mchongoko, baadhi ya waliohusika wamekamatwa

TRC: Kulitokea hujuma katika Treni ya Mchongoko, baadhi ya waliohusika wamekamatwa

Huyo/hao Wahujumu wenyewe mkiwajua mtawamudu au mtaishia tu kumuuliza "Mkuu hata wewe?".
 
Nilisema toka awali, Aboud na Shabibby washughulikiwe mapema, vinginevyo watatusa sana nchi hii. Route mbona zipo nyingi tu zina uhaba wa mabasi, si wapeleke huko?
Wamejisahau kwa upande wa Imani pia, kuwa riziki anatoa Mungu
Na kama hilo wameacha pia basi wajue duniani mambo hubadilika kwa maslahi ya nchi
 
Hao waliokamwatwa tutansubiri kuwaona wakipelekwa mahakamani .
 
Nilisema toka awali, Aboud na Shabibby washughulikiwe mapema, vinginevyo watatusa sana nchi hii. Route mbona zipo nyingi tu zina uhaba wa mabasi, si wapeleke huko?
Avoid naming people for severe accusations ambazo huwezi kutolea ushahidi.
 

TAARIFA KWA UMMA UZUSHI KUHUSU TRENI MCHONGOKO

Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba 2024.

Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa na watu mbalimbali kuhusu kusimama kwa Treni za EMU - Electric Multiple Unit, (Mchongoko) na changamoto za umeme.

Ukweli ni kwamba tangu kuanza kwa safari ya kwanza ya treni zinazotumia nishati ya umeme Juni 14, 2024 hakujawahi kuwa na changamoto ya umeme, tunawashukuru wenzetu wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa.

Aidha, kilichotokea Novemba 3, 2024 na kusababisha kusimama kwa treni ya EMU kwa takribani Saa 6 ni hujuma kutokana na kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.

Shirika la Reli Tanzania linauhakikishia umma kuwa hakuna treni ya Mchongoko iliyopata hitilafu ya kiufundi.
Tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa na hatua stahiki dhidi yao zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo husika.

Shirika linawakumbusha wananchi kuwa bado tuko kwenye kipindi cha mwaka mmoja cha matazamio, na kama changomoto zozote zinajitokeza, TRC itaujulisha umma kwa uwazi kama siku zote tunavyofanya, na taarifa rasmi mtazipata kwenye vyanzo vyetu rasmi na si vinginevyo.

TRC inawashukuru abiria kwa uvumilivu kipindi cha changamoto.

Fredy Mwanjala
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Uongo huo.

Majina Yao yako wapi??????

Wahujumu reli kwa maslahi Gani?????
 
Avoid naming people for severe accusations ambazo huwezi kutolea ushahidi.
Nini wewe, wachunguzwe hao.., hivi unanunuaje mabasi mapya 200 just a few weeks kabla ya kuanza SGR kwenye route hiyo hiyo ya kwake? Means alishajipanga..
 
Back
Top Bottom