DOKEZO TRC, mtanitafuta kwa uchochezi au Mkurugenzi Mkuu Kadogosa utanishukuru mimi na JF? Treni imefungwa kwa waya!

DOKEZO TRC, mtanitafuta kwa uchochezi au Mkurugenzi Mkuu Kadogosa utanishukuru mimi na JF? Treni imefungwa kwa waya!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Ninavyofahamu kwenye usafiri wa mabasi kuna wakaguzi kama maofisa wa kitengo cha usalama barabarani.

Sasa kwenu nyie shirika la reli TRC ya ndg Kadogosa sijui nani anawakagua mwanzo, katikati ya safari au mwisho.

Pichani ni treni mnaita deluxe inayotoka Dar Es Salaam kwenda Arusha na hizo namba ni mabehewa yenye hizo kasoro.
IMG_20221215_080444.jpg
IMG_20221213_094646.jpg


Hii hapa chini ndiyo sijui wataalam wa wanasemaje kama break zikiwa katika hali hiyo, je treni inaweza kufanya kazi miezi mingapi na hakuna shida?
IMG_20221215_080953.jpg
IMG_20221213_094403.jpg


Nawasilisha.
 
Ninavyofahamu kwenye usafiri wa mabasi kuna wakaguzi kama maofisa wa kitengo cha usalama barabarani.

Sasa kwenu nyie shirika la reli TRC ya ndg kadogosa sijui nani anawakagua mwanzo, katikati ya safari au mwisho...
Heeee ilitakiwa Mkurugenzi ajiuzulu ASAP hii kitu ni hatari kwa watumiaji wa treni no way huu ni uzembe mkubwa sana
 
NB:  Ndugu Kadogosa TRC natoa ushauri, kuna hizo behewa nasikia mnasema mpya wakati BiM Dr, SSH alisema tunaagiza kwanza used na mapya yatakuja mwakani.

Katika hizo mpya tunaomba route moja itakayokuwa ni Express kutoka Dar, Moshi na Arusha, badala ya masaa 20 Dar to Arusha itumie masaa machache as 8 au 10 kwa kutosimama vile vituo vidogovidogo.
 
Huo waya iliitishwa tenda na mzabuni aliyeshinda aliutoa ujerumani na ametukodishia kwa Milioni 400 za Kitanzania.

Kama unauona waya ni dhaifu ungetuma maombi ya tenda utuletee wa kwako. Ila kwa sasa huu waya ni salama. Kwanza hatuwezi amini picha hua zinaeditiwa.

I wish litoke hili jibu
 
Ninavyofahamu kwenye usafiri wa mabasi kuna wakaguzi kama maofisa wa kitengo cha usalama barabarani...
Vitu vya kifala sana hivi..halafu mamlaka kimyaaaa..

Mimi ningekuwa kiongozi hakika watu wangejinyea, mambo ya kipumbavu kama haya lazima nizae na mtu...
Hivi kwa nini watu hawana huruma na maisha ya watu aisee?
Duh...
 
Back
Top Bottom