DOKEZO TRC, mtanitafuta kwa uchochezi au Mkurugenzi Mkuu Kadogosa utanishukuru mimi na JF? Treni imefungwa kwa waya!

DOKEZO TRC, mtanitafuta kwa uchochezi au Mkurugenzi Mkuu Kadogosa utanishukuru mimi na JF? Treni imefungwa kwa waya!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ninavyofahamu kwenye usafiri wa mabasi kuna wakaguzi kama maofisa wa kitengo cha usalama barabarani.

Sasa kwenu nyie shirika la reli TRC ya ndg Kadogosa sijui nani anawakagua mwanzo, katikati ya safari au mwisho.

Pichani ni treni mnaita deluxe inayotoka Dar Es Salaam kwenda Arusha na hizo namba ni mabehewa yenye hizo kasoro.
View attachment 2447266View attachment 2447267

Hii hapa chini ndiyo sijui wataalam wa wanasemaje kama break zikiwa katika hali hiyo, je treni inaweza kufanya kazi miezi mingapi na hakuna shida?
View attachment 2447268View attachment 2447270

Nawasilisha.
Nchi ngumu sana hii mabillion ya hela za Spea yashaibiwa apo😅
 
Malaika mlinzi amekuongoza vyema.

Sasa utasikia DPP anaanza kumsumbua Maxence Melo amtaje member aliyetoa taarifa hii.

Na kwa kuficha uozo utaona taarifa ya kuzuia kupiga picha vituo vyote vya treni wakisingizia tishio la usalama.

Bravo mkuu
CAG achunguze TRC pia
 
Kwanza hapo umeokoa maisha ya watu kibao...
Maana ajali za treni mziki wake unajulikana

Ova
 
Sasa mkuu mimi mtu mdogo hadi DPP anitafute kweli?.

Alafu wakituzuia tusipige picha kwa simu inabidi wakati wa kulipanda hilo dubwana pale kwenye milango awepo askali anakusanya simu, ukifika mwisho wa safari yako ndipo unapewa phone yako.

Vinginevyo hatutakuwa tunaishi dunia hii ya binadamu, maybe tupo sayari nyingine kabisa.
Pale ferry kuna madudu kibao. Wamezuia kupiga picha ili isije kuvuja kwa wakubwa huko mauzembe yao
 
Serikaki haipaswi wala haiwezi kufanya biashara kabisa. Biashara wawachiwe wafanya biashara.
 
Huyu mkurugenzi sijui ana kimzizi, mwenzake huko Wakala wa ndege za serikali kachinjiwa baharini lakini yeye kaponea chupuchupu, eti imevinjwa bodi peke yake daaah...
 
Mkuu acha uchochezi wewee. Mungu yupo!
Acha ujinga mkuu, Kama yeye ameiona kasoro ulitaka anyamaze ili watanzania wafe ndio viongozi waje na matamko? Mangapi yanafikishwa katika vyombo husika na hayafanyiwi kazi mpaka consequences related to the situation itokee?! Mwendo ni huu huu wa kuanika wazi ili wananchi wajue na wapige kelele kwa ujumla wao. Inamaana mpaka Sasa baada ya miaka yote hii hujui Kuna kufumbiana macho na wanaoumia ni raia? Litakapokuja kugusa familia yako kwa uzembe wa mamlaka ndio utaelewa kwanini watu wanaweka wazi Mambo kama haya.
 
Ajabu kweli mkuu
Huyu mkurugenzi sijui ana kimzizi, mwenzake huko Wakala wa ndege za serikali kachinjiwa baharini lakini yeye kaponea chupuchupu, eti imevinjwa bodi peke yake daaah...
 
Mpaka inakera na kufikirisha sana. Wenye uwezo na nia thabiti wapo ila wajitokezapo wanapotezwa dah. Nini hasa kifanyike kama wananchi wenyewe tumekubaliana na hali?!
Linnchi lina watu wazembe kupitiliza.
 
Pale ferry kuna madudu kibao. Wamezuia kupiga picha ili isije kuvuja kwa wakubwa huko mauzembe yao
Tafuta upenyo mkuu piga picha na tupia hapa, hatuna na inaonekana nchi yetu hairuhusu Investigation Journalist.
 
Huyu mkurugenzi sijui ana kimzizi, mwenzake huko Wakala wa ndege za serikali kachinjiwa baharini lakini yeye kaponea chupuchupu, eti imevinjwa bodi peke yake daaah...
Bodi ivunjwe manake na mkurugenzi atoke ofisini Hawa wazee mbona ving'ang'anizi
 
Back
Top Bottom