DOKEZO TRC, mtanitafuta kwa uchochezi au Mkurugenzi Mkuu Kadogosa utanishukuru mimi na JF? Treni imefungwa kwa waya!

DOKEZO TRC, mtanitafuta kwa uchochezi au Mkurugenzi Mkuu Kadogosa utanishukuru mimi na JF? Treni imefungwa kwa waya!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
So rais ndio kafunga hizo waya???au kawatuma kufunga hizo waya??acha kudhihaki na kutumia lugha ya matusi kwa mtu au taasisi ....Kama huna cha kuandika ni bora kuwa msomaji.
Yuko sahihi,Mama Samia bado hajakitende a kazi kiti chake mpk sasa amekua km mtu ambae mpk afikishiwe jambo lake ndo achukue hatua sasa treni km hilo liko barabaran na hamna mtu aliewajibika
 
Heshimu hicho kiti ndugu. Japo maisha ya watumiaji wa chombo hicho ni muhimu,kuna wahusika ambao kwa taarifa hiyo leo hadi ifike jioni hawatakuwa na kazi.
Kwa hii Serikali nan atakaewawajibisha hai wahusika,subir uone
 
Ingekuwa enzi za Magufuli saa hizi wangeshatumwa watu wakufuatilie na pangine Jamii Forum ingeshafunguliwa kesi.
Enzi hizo unazo sifia zilikuta mabehewa haya yakiwa mapya, yalinunuliwa na Kikwete toka Korea kusini, kwa bahati mbaya enzi hizo zilikuja na bana matumizi ya service. Bila huduma hakuna chombo kitakacho dumu.
Kuna mabehewa na vichwa vya treni vilinunuliwa enzi za mwalimu miaka ya sabini huko lkn mpaka 2007 kabla ya ubinafsishaji yalikuwa kama mapya kwakua yalikuwa yakipata service inavyotakiwa.
Inasikitisha sana kuona mabehewa mpya yanachakaa kiasi hicho kwa muda usiozidi maika 7
 
Nlkuwa nina hamu ya kupanda ayo matren lakini nlivoona ivo nmeishiwa na nguvu kabsaa 🙆🏻‍♂️🤕
Hapana mkuu usiogope take action nahisi kutokana na hii nadhani tayari watakuwa wanarekebisha.
 
Huo waya iliitishwa tenda na mzabuni aliyeshinda aliutoa ujerumani na ametukodishia kwa Milioni 400 za Kitanzania.

Kama unauona waya ni dhaifu ungetuma maombi ya tenda utuletee wa kwako. Ila kwa sasa huu waya ni salama. Kwanza hatuwezi amini picha hua zinaeditiwa.

I wish litoke hili jibu
Hahahhaha jamaa wa arse8 unazingua.
 
Natamani tungekuwa tunakodi viongozi wa Serikali kutoka kwingine, naamini hawa waliopo wangejifunza kitu. Ngoja tusubiri ajali, kuundwa kwa tume na mchezo kuishia hapo maisha yanaendelea.
 
Hivi huwa unamwabudu Mungu kweli mbona ha ni mabehewa ya mizigo ya zamani sana
Mkuu Mungu anaabudiwa mkuu, sema unataka kuzingua hapa, behewa gani za wanyama zina namba hizo?.

Tupia picha moja kwa uthibitisho.
 
NB:  Ndugu Kadogosa TRC natoa ushauri, kuna hizo behewa nasikia mnasema mpya wakati BiM Dr, SSH alisema tunaagiza kwanza used na mapya yatakuja mwakani.

Katika hizo mpya tunaomba route moja itakayokuwa ni Express kutoka Dar, Moshi na Arusha, badala ya masaa 20 Dar to Arusha itumie masaa machache as 8 au 10 kwa kutosimama vile vituo vidogovidogo.
Itatembea ktk reli hiyo huyo ya mjerumani au mtajengewa standard gauge
 
Nchi hii haishi vituko

Watu mpaka wasimamiwe,sasa hapo wa kulaumiwa nani

Ova
 
Kitaalamu hiyo naweza ita expansion joint ya behewa, kuruhusu contraction kati ya taili la behewa na shock absorber
Mkuu pale kuna vitu viwili kuna brake shoe iliyoshikwa na vertical lever na brake block ambayo ipo attached katika brake shoe kwa kuwekwa safety pin makosa ni ile wire ambayo ipo katika shoe haistaili pia brake block imepata crack si sahihi iwe vile.
 
Hii hapa chini ndiyo sijui wataalam wa wanasemaje kama break zikiwa katika hali hiyo, je treni inaweza kufanya kazi miezi mingapi na hakuna shida?

1671114816002.png

1671114870481.png

Hizi ni breki za treni jamani!!!!!

Kuna treni iliua sana kwa sababu mabehewa yalikuwa hayashiki breki hivyo kichwa kilizidiwa na likaanza kukimbia ovyo na kupinduka. Watu walikufa sana na kosa lilikuwa mfumo wa breki za mabehewa kutofanya kazi

Ilikuwa Igandu, mwaka 2002
1671115491123.png
 
Back
Top Bottom