JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
KUWASILI KWA SETI YA KWANZA YA TRENI YA KISASA EMU
Dar es Salaam, Tarehe 03 Aprili 2024
Shirika la Reli Tanzania TRC linautaarifu umma kuwa Seti ya kwanza ya treni ya kisasa ya EMU, vichwa vitano vya umeme na mabehewa matatu ya abiria yamewasili katika bandari ya Dar es Salaam.
Serikali kupitia TRC ilifanya manunuzi ya Seti kumi (10) za treni za kisasa zijulikanazo kama Electric Multiple Unit kutoka kwa watengenezaji kampuni ya Hyundai Rotem ya nchini Korea Kusini.
Seti moja ya EMU ina uwezo wa kubeba abiria 589 na kutembea kwa kasi wa kilomita 160 kwa saa. EMU ni treni iliyoundwa kwa teknolojia ya kisasa inayomuwezesha abiria kupata huduma muhimu ikiwemo huduma ya mtandao (Wi-FI), sehemu za kukaa watu wenye mahitaji maalum, mifumo ubaridi na kamera za usalama (CCTV Camera).
Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania imepokea jumla ya mabehewa 65 ya abiria, vichwa 9 vya umeme na Seti moja ya EMU. Seti zingine za EMU zitaendelea kuwasili kila mwezi hadi Oktoba 2024.
Kuwasili kwa vitendea kazi kunaifanya TRC kuwa tayari kuanza huduma za usafirishaji abiria katika reli ya kiwango cha kimataifa
Maendeleo ya Mradi wa SGR awamu ya kwanza yamefikia asilimia 98.90 kwa kipande cha Dar es salaam Morogoro (KM 300), asilimia 96.51 kipande cha Morogoro Makutupora, asilimia 13.98 kipande cha Makutupora - Tabora, asilimia 5.44 kipande cha Tabora - Isaka, asilimia 54.01 kipande cha Mwanza - Isaka.
Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano