TRC: Seti ya Kwanza ya Treni ya Kisasa ya EMU, Vichwa Vitano vya Umeme na Mabehewa Matatu ya Abiria imewasili

TRC: Seti ya Kwanza ya Treni ya Kisasa ya EMU, Vichwa Vitano vya Umeme na Mabehewa Matatu ya Abiria imewasili

Kwamba seti ya kwanza ya vichwa vitano vya treni na mabehewa matatu ya abiria yamewasili na kwamba seti moja ina uwezo wa kubeba abiria 589. Ina maana hiyo seti moja iliyofika yenye mabehewa matatu ndiyo ina uwezo wa kubeba idadi yote hiyo ya abiria 589? Mbona ni idadi kubwa sana au mimi ndiye sijaelewa.
Mkuu nadhani inawezekana! Kila behewa litabeba abiria karibia 200!
 
Walau baadhi ya vichwa vinavyoletwa safari hii vinafanana kidogo na treni halisi za umeme za wenzetu.

Ila siyo kile kichwa cha majaribio kutoka Dar kwenda Morogoro ile siku ya majaribio!
Maana hakina tofauti na ile treni kimeo ya dizeli ya Kenya, waliyobambikwa na Wachina. Halafu wakaambiwa eti ni SGR!!
Ni lazima kile kichwa cha majaribio kipite kwenye kila reli mpya, ninyi ambao mliyokimbia sayansi, kwanza kina uzito tofauti kwa ajili ya kupima uimara wa reli, na umadhubuti, hivyo vinavyokuja huwa vya kazi na si vizito sana.
 
Ahsante kwa maelezo mkuu,natumaini safari zitarahisishwa kiliko mabasi au unamtazamo gani juu ya hili
 
Ahsante kwa maelezo mkuu,natumaini safari zitarahisishwa kiliko mabasi au unamtazamo gani juu ya hili
Ni kweli safari zitarahisishwa sana, hasa baada ya kumalizia mtandao mzima wa SGR, tukumbuke treni hizi engine zinamfumo wa motor!, hata mfumo wa speed yake ni wa ku engage, yaani unachagua unataka ikimbiaje 80km/h-100km/h-120km/h160km/h-180km/h.
#Kisayansi nadhani unafahamu utendaji kazi wa motor!
 
Atleast kichwa hata kimoja wangekiita Magufuli express, Daaah yule mwamba naye anamchango mkubwa sana kwenye hii project. Watu makatiliii😬
Halafu Dar moro railway inaurefu wa 300Kms, na train inaspeed ya 160Km/h, automatically hiyo chuma dar moro ni masaa mawili na nusu hadi matatu ukiongeza dakika za kushusha na kupakia
 
TAARIFA KWA UMMA
KUWASILI KWA SETI YA KWANZA YA TRENI YA KISASA EMU

Dar es Salaam, Tarehe 03 Aprili 2024
Shirika la Reli Tanzania TRC linautaarifu umma kuwa Seti ya kwanza ya treni ya kisasa ya EMU, vichwa vitano vya umeme na mabehewa matatu ya abiria yamewasili katika bandari ya Dar es Salaam.

Serikali kupitia TRC ilifanya manunuzi ya Seti kumi (10) za treni za kisasa zijulikanazo kama Electric Multiple Unit kutoka kwa watengenezaji kampuni ya Hyundai Rotem ya nchini Korea Kusini.

Seti moja ya EMU ina uwezo wa kubeba abiria 589 na kutembea kwa kasi wa kilomita 160 kwa saa. EMU ni treni iliyoundwa kwa teknolojia ya kisasa inayomuwezesha abiria kupata huduma muhimu ikiwemo huduma ya mtandao (Wi-FI), sehemu za kukaa watu wenye mahitaji maalum, mifumo ubaridi na kamera za usalama (CCTV Camera).

Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania imepokea jumla ya mabehewa 65 ya abiria, vichwa 9 vya umeme na Seti moja ya EMU. Seti zingine za EMU zitaendelea kuwasili kila mwezi hadi Oktoba 2024.

Kuwasili kwa vitendea kazi kunaifanya TRC kuwa tayari kuanza huduma za usafirishaji abiria katika reli ya kiwango cha kimataifa

Maendeleo ya Mradi wa SGR awamu ya kwanza yamefikia asilimia 98.90 kwa kipande cha Dar es salaam Morogoro (KM 300), asilimia 96.51 kipande cha Morogoro Makutupora, asilimia 13.98 kipande cha Makutupora - Tabora, asilimia 5.44 kipande cha Tabora - Isaka, asilimia 54.01 kipande cha Mwanza - Isaka.

Ni jambo zuri kwa maendeleo yetu sote, hii ni ya mchongoko iko vizuri, subira yafuta heri ni kinyume na maneno ya watu.
 
na lile likichwa la yutong walilitoa wapi au tusingesanuka wangetuletea mandonga ya dizain ile
Nadhani kilikuwa cha majaribio tu, sema binadamu ni wazushi sana, walikuzusha hata mimi nikawaamini, ila ukweli ndio umedhihirika nimeona kwa macho yangu mwenyewe, kitu mchongoko kama nyoka, tuwasamehewe tu.
 
Mmmmmhh 500km/h yaan dar to shinyanga kwa dakika 60 au.....huyu mama akifanikiwa hz kitu zikafanya kazi na bei ikawa kama ile ya mabus au chini kidogo afu kwa spid hata ya 130km/h atakuwa kafanikiwa sana. Cha muhim ahakikishe sgr na bwawa la Mwal. nyerere yanafanya kazi kwa ubora hasa.
Mama gani akifanikiwa? Upumbavu mwingine!!!!
 
Reli za train kuanzia speed 300+ sio hizi, mkuu, zile gurudumu la chuma linajishika kwa kui lock reli.
Reli hizi sio za kisasa kwa ulimwengu ulipofikia, hizi rail wenzetu huko ngambo ni za miaka ya 50s-70s ndipo zilipamba moto, LAKINI RELI HIZI ZA SGR ZILIBUNIWA RASMI 12-NOV - 1922,WAKATI BABA WA TAIFA ANAZALIWA!.
Ilibuniwa na vijana saba, waliokuwa wakufundisha science, Butler University!, 1922.
Ahsante kwa taarifa.
Aisee tupo nyuma, ndio nasikia kila kona hii project inapigiwa pambio na chapuo kumbe ni tech za 1960's.

Ila sasa wakaze basi tufike hata 220 hapo dah!
 
Mmmmmhh 500km/h yaan dar to shinyanga kwa dakika 60 au.....huyu mama akifanikiwa hz kitu zikafanya kazi na bei ikawa kama ile ya mabus au chini kidogo afu kwa spid hata ya 130km/h atakuwa kafanikiwa sana. Cha muhim ahakikishe sgr na bwawa la Mwal. nyerere yanafanya kazi kwa ubora hasa.
Hivi unawajua unawasikia, utasikia sgr imeibiwa. Tupo hapa.
 
Ahsante kwa taarifa.
Aisee tupo nyuma, ndio nasikia kila kona hii project inapigiwa pambio na chapuo kumbe ni tech za 1960's.

Ila sasa wakaze basi tufike hata 220 hapo dah!
Hatuwezi kukwepa hatua za makuzi, ni stage kwa stage mkuu.
 
Hatuwezi kukwepa hatua za makuzi, ni stage kwa stage mkuu.
Inabidi tujitutumue kuendana na kasi ya maendeleo ya dunia mbona simu hamtumii za 2001? Mbona network hamtumii gprs bali mnatumia 4G na 5G.

Kingine huwezi nishauri leo nifike dukani ninunue tv la chogo kisa inapaswa niendane na hatua za makuzi, mbona ndege hawanunui za 1970's .

Aisee walete za mwendokasi.
 
Back
Top Bottom