TRC: Seti ya Kwanza ya Treni ya Kisasa ya EMU, Vichwa Vitano vya Umeme na Mabehewa Matatu ya Abiria imewasili

Kwamba seti ya kwanza ya vichwa vitano vya treni na mabehewa matatu ya abiria yamewasili na kwamba seti moja ina uwezo wa kubeba abiria 589. Ina maana hiyo seti moja iliyofika yenye mabehewa matatu ndiyo ina uwezo wa kubeba idadi yote hiyo ya abiria 589? Mbona ni idadi kubwa sana au mimi ndiye sijaelewa.
 
Rangi za vichwa na mabehewa hazi-reflect alama yoyote ya Tanzania, wameshindwa hata kupaka rangi mojawapo iliyopo kwenye bendera ya taifa , nembo ya taifa au hata mlima Kilimanjaro.

Vv
 
Ile treni ya kisasa ya Umeme aliyotuahidi Shujaa Magufuli akiiita Mjusi imefikishwa bandarini DSM

Vimewasili vichwa 5 Vya Umeme na mabehewa 3 ya Abiria

Source: Ayo TV
 
Kwa nauli haiwezi kuwa Sawa na Mabasi na nauli itakuwa juu kuliko basi kaa mkao wa kula
 
Sawa hongereni kwa kuleta treni.

Ila sasa huu umeme ambao bwawa likijaa maji wanazima mitambo na bwawa likikosa maji wanazima pia tutafika kweli??
 
Serikali kazi yake iwe kujenga reli, treni zinunuliwe na kuendeshwa na makampuni na watu binafsi ndio tutaona ufanisi
 
Wacha basi na wewe! Dar to Shy kilomita 500?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…