bongodili tele
JF-Expert Member
- Jun 8, 2024
- 1,520
- 3,022
Kuweka uzio ni jambo jema lengo ni kulinda uhai.
Lakini kuweka uzio hakukuzingatia athari za kiuchumi kwa wakaazi wa maeneo husika baada ya kuwatenganisha pande mbili ili waweze kuwasiliana ni lazima wafate kivuko ambavyo navyo sio rafiki.
Mfano ili uvuke upande wa pili ni lazima ufate kivuko kilometers moja ukavuka daraja lenye urefu wa mita 500 then urudi tena kilometers moja ulipotoka awali baada ya kuvuka so itakulazimu utembee kilometers tatu sawa na dakika 45 tofauti na zamani kabla ya uzio ambapo ulitumia dakika moja kuvuka upande wa pili ambao ni mita 30.
Hii imeathiri biashara zote za mafrem, mahoteli,bar,nk zilizotegemea mapitio ya watu kabla ya uzio.
Kuanzia vingunguti, airport, majumba sita, Ukonga,gongo la mboto ni kilio kwa kwenda mbele biashara zimekufa watu wanalazimishwa wakapite juu ya madaraja ambayo sio rafiki utadhani kila mtza ana miliki gari.Mfano airport pale ni lango la nchi kimataifa thus pana watz waliwekeza kujenga mahoteli pana hotel kama tano hivi zenye ghorofa zaidi ya nne zote zinaenda kufa kwa sababu ya njia zimefungwa ili ufike kwenye hizo hotel ni mzunguko wake sio wa kitoto.
Achilia biashara zingine kumbuka hawa ni walipa kodi na biashara ni watu na watu ni njia sasa ukifunga njia umeua biashara uchumi utazungukaje ajira ngapi zimekufa.
Check vingunguti ni eneo la viwanda pana malori yanatakiwa yaingie viwandani daraja lipo lakini ni one-way halina sehemu ya malori kukunja ni labda ukaingilie buguruni ucheze na vumbi mwambao wa reli hadi vingunguti inaathiri mda pia barabara sio rafiki.
Halafu sijui nani kawashauri wajenge madaraja vichunguu mjini kuchafua sura ya jiji na kuzuia maji tutegemee vilio vya maji kujaa kwenye majumba ya watu pembeni mwa madaraja sababu wameblock njia za maji bila kuacha matoleo upande wa pili.
Madaraja vichunguu ndo wajenga uhasibu na chang'ombe ukiangalia gharama za kujaza vifusi yaani huo mlima ni gharama za kujenga nguzo kama za daraja la Tazara tofauti yake ni ndogo sana.Madaraja vichunguu ujengwa maporini huko na sio mijini daraja ni kama lile la Tazara chini liwe wazi maisha yaendelee chini na sio unblock upande wa pili,ni aibu kwa mainjia wenzao wakitoka nje ya nchi.
Sijawahi ona madaraja vichunguu katikati ya mji yanachafua mazingira ya mji,daraja linatakiwa liwe kivutio kama sehemu ya utaliie pia.
Ilitakiwa nguzo ziende hadi Pugu ili chini maisha yaendelee kama kawaida ,watu wapite bila vizuizi.Kama gharama za nguzo ni kubwa ilitakiwa treni ianzie Pugu huku nguzo zikijengwa mdogo mdogo kuja mjini.
La imeshindikana ilitakiwa wainue tuta la reli juu mita 6 sehemu zote za vivuko vyenye watu wengi waweke karavati box la urefu wa mita tano kwa tano watu,pikipiki,toroli vipite chini ya reli magari yakapite juu ya hayo madaraja hii isingeathiri biashara za watu kwa kukosa watu.
Mbona mashambani na maporini wamewawekea wanyamapori na mifugo hizo karavati box kupita chini ya reli.
Hata wao TRC wameathirika kimapato kwa kuweka uzio umewazuia abiria upande wa pili wasiweze kupanda hii treni daladala ya Pugu gerezani haijai kama zamani kwa maana ya wengi wamezuiwa na uzio ili ukapande treni daladala ni lazima ukavuke hizo kilometers kufata daraja ambao ni sawa na kupita zaidi ya vituo vitatu vya daladala hivyo hauna uchaguzi zaidi ya kupanda daladala tu labda ujio wa BRT mwendokasi utawaokoa watu walioupande wa pili ya reli.Treni daladala siku hizi halijazi sana kama zamani kabla hawajaweka uzio so ni hasara kwa TRC.
Pana huduma za kijamii na kiroho mfano makanisa,shule,mahospitali masoko nk upande wa pili wameathirika.
Ushauri kwa mikoani ambapo mradi unaendelea wajaribu kutoathiri shughuli za kiuchumi kwa kuugawa mji pande mbili ni mateso kwa wakazi husika inauwa biashara inaharibu sura ya mji inapunguza mapato kwa biashara kufa na Kodi zinakosekana.
Bila hivyo Mwanza,Shinyanga,Tabora nk jiandaeni na vilio kama wanavyolia waliowekewa uzio.
Somo kwa mainjia wetu tunapodesign miundombinu jaribuni kukaa na wakazi husika muangalie faida na hasara ya hio design kabla ya ujenzi.
Msichore tu design kwa sababu mnakaa bunju,masaki, mbezi kwa sababu nyie sio wakazi wa maeneo husika,mngekuwa mnaishi maeneo hayo mngejali maisha ya wengine kwani maisha sio reli tu na maisha mengine inapaswa yaendelee.
Mliangali treni tu na sio athari za kiuchumi kwa wakaazi husika baada ya maamuzi yenu.