Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limevunja mkataba na kampuni ya Eurowagon ya nchini Uturuki baada ya kushindwa kukamilisha ujenzi wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria.
Kwa mujibu wa mkataba huo, vifaa hivyo vilitakiwa kukamilika Novemba 2021 lakini kwa kuwa Eurowagon ilishindwa kutimiza matakwa ya mkataba na kipande cha kwanza Dar es Salaam mpaka Morogoro kikiwa hatua ya mwisho ya ujenzi, TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25,2022.
Hayo yamesemwa Juni 15, 2022 na mkuu wa kitengo cha uhusiano TRC, Jamila Mbarouk wakati akitoa taarifa ya vyombo vya habari kuhusu hatua mbalimbali zinazoendelea katika ujenzi wa reli ya kisasa SGR.
Amesema vifaa hivyo vya majaribio vilitakiwa kukamilika mapema katika kuhakikisha uendeshaji wa awali unaanza baada ya majaribio mara baada ya ujenzi kukamilika.
“TRC ilisaini mkataba wa vifaa vichache wa muda mfupi wa ununuzi wa vichwa vya treni ya umeme viwili na behewa 30 za abiria vitakavyofanyiwa ukarabati kutoka kampuni ya Eurowagon ya nchini Uturuki."
“Vifaa vilitakiwa kukamilika Novemba 2021, TRC iliamua kusitisha mkataba na kuwajulisha kwa barua Februari 25, 2025 na iliendelea na jukumu la kumalizia ukarabati bila gharama na vifaa vinatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti mwaka huu,” amesema Jamila.
Amesisitiza kuwa TRC haina mgogoro wa kimapato na kampuni ya Eurowagon kwani ilitimiza matakwa ya kimkataba ya kulipa asilimia 35 na kwa kutimiza masharti ya umiliki wa vichwa vya treni vya umeme viwili na behewa 30 vilishahamia kwa TRC.
“Mkataba unatoa haki kwa TRC kuchukua majukumu ya kumalizia ukarabati mara pale mzabuni anaposhindwa kutimiza masharti ya mkataba,” amesema Jamila.
Kaimu mkurugenzi miundombinu ya reli, Machibya Masanja akizungumzia mkwamo uliopo sasa amesema uchelewaji wa mabehewa ya abiria pamoja na vichwa vya treni vipya umetokana na athari za Uviko19.
“Sisi si kisiwa tunahusiana na nchi nyingine mabehewa yanakozalishwa kumekuwa na changamoto na athari mojawapo ilienda kwenye uzalishaji wa mabehewa, juhudi mbalimbali zinafanyika kuwasiliana na mzabuni ili kufikia Agosti mabehewa hayo yawe yamewasili nchini,” amesema Masanja.
Wakati ujenzi ukiendelea TRC inafanya manunuzi ya behewa za mizigo, behewa za abiria, seti za treni za kisasa na vichwa vya treni ya umeme.
Shirika hilo lilisaini mikataba ya manunuzi ya behewa mpya 1430 ya mizigo kutoka kampuni ya CRRC ya nchini China, behewa mpya za abiria 59 kutoka kampuni ya Sung Shin Rolling Stock Technology Limited ya Korea Kusini, seti 10 mpya za treni za kisasa zenye behewa 80 na vichwa 17 vya umeme vipya kutoka Hyundai Rotem ya Korea Kusini vyenye thamani ya Sh 1.18 Trilioni.
Hapa ninachokisoma na kinachokanushwa ni vitu viwili tofauti, kwanza Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweliMADAI
Mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi).
Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria ambao ulitegemewa kukamilika ifikapo Novemba 2021.
TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25, 2022 kwa madai kwamba EUROWAGON wamechelewesha kazi na mazungumzo hayajawahi kuendelea. Kampuni ya RINA ilipewa kazi ya kuthibitisha kazi ya ukarabati na utiaji nakshi mabehewa hayo na kuthibitisha kwamba kazi hiyo imekamilika kwa 50%.
Hivyo EUROWAGON Railways Limited wanataka malipo ya Sh. 10 bilioni, ambayo ni 15% ya kazi iliyothibishwa na RINA kwamba kazi ya ukarabati na utiaji nakshi ilifanyika kwa 50% na malipo ya Sh. 23 bilioni ni kwa ajili ya 35% ya kazi hiyo. Malipo haya yalifanyika Desemba 14, 2020
Baada ya kuvunja mkataba huo Februari 25, 2022 na EUROWAGON, TRC wakaingia mkataba na kampuni nyingine kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa na kutia nakshi. Kampuni hizo ni Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany)
EUROWAGON kupitia Mwanasheria Duygu Seda, wakamuandikia barua Mkurugenzi wa TRC kwamba Tanzania Railways Corporation (TRC) wamevunja mkataba kwa njia ambazo siyo halali. TRC walivunja mkataba kwa kigezo cha EUROWAGON kushindwa kuwasilisha Dhamana ya Utendaji (performance Bond)
Mwanasheria wa EUROWAGON, Duygu Seda katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa TRC amemueleza kwamba kutokana na sheria za EU, Germany, Turkey na Austria na makubaliano kati ya EU na Turkey, TRC hawaruhusiwi kufika yalipo mabehewa na vichwa vya SGR wala kusafirisha isipokuwa EUROWAGON.
TRC hawakununua vichwa na mabehewa mapya kwa ajili ya SGR, isipokuwa, EUROWAGON waliopewa zabuni walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC
Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalcin Aydemir anasema kwamba TRC walimpa kazi bila dhamana ya Utendaji (Bank/performance guarantee) lakini ghafla TRC wakabadili gia angani na kuidai. Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa anasema EUROWAGON wanatapatapa tu hawana hoja.
TRC June 17, 2022 ilisema imesitisha mkataba na kampuni ya EUROWAGON, iliyokuwa ikitengeneza mabehewa hayo baada ya kushindwa kukamilisha ukarabati vichwa 2 na mabehewa 30 ya abiria, kwa ajili ya majaribio hayo, ni kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk
Vifaa hivyo kutoka EUROWAGON vilitakiwa kukamilika Novemba, 2021, TRC ilisitisha mkataba na kuwataarifu kwa barua Februari 25, 2022 na kuendelea na kazi ya kukamilisha ukarabati unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2022,” alisema mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk
Kwa mujibu wa Tanzania Railways Corporation, taarifa waliyoeleza kwa waandishi wa habari June 15, 2022, walisema Mkataba kati yao na EUROWAGON unaipa TRC haki ya kuchukua jukumu la kukamilisha ukarabati iwapo mzabuni atashindwa kuzingatia masharti ya mkataba.
View attachment 2424063
1. Taarifa ya TRC inasema vichwa vipya na mabehewa mapya, lakini ukweli ni kuwa ni vichwa mitumba na mabehewa mitumba ya mwaka '1947'!.
2. Mkataba ni wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa mitumba!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!.
3. Hakuna ubaya nchi kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, kitu muhimu ni Watanzania tuelezwe ukweli!.
4. Jee hivyo vichwa viliundwa lini, wapi na vimetumika muda gani kabla sisi hatujauziwa?.
5. Mitumba hiyo imenunuliwa kwa bei gani na inakarabatiwa kwa bei gharama gani?.
5. Tufanyiwe comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua mitumba hiyo?.
6. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila maintance cost ni ndogo, unaweza kununua mitumba kwa bei poa kumbe ni mitumba choka mbaya, hivyo maintenance cost ikawa juu.
7. Sii wengi wanajua kazi ya CAG sio kutoa tuu zile ripoti za hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, ufhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, jee kulifanyika tathmini yoyote rail worthness report ya vichwa mabehewa hayo mitumba kabla hayajanunuliwa?. Then CAG atufanyie value for money audit, msikute mitumba hiyo tumepewa bure, huku watu wakipiga kubwa tunauziwa kwa bei ya mapya!.
8. Ukiingia mkataba wa manunuzi, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.
9. Tulivinja mkataba wa Dowans, watu wakajiapisha "over my dead body", tulishitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa tukasema hatulipi!, ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa!.
10. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe mitambo ile, Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo mitumba!.
11. Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans tuliovunja, kwa gharama zile zile na tukawalipa!.
12. JPM alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule, huku nyuma, sio tuu tumelipa, bali pia tumeinunua ile mitambo kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni mtumba hatununui, sasa ni mali yetu na malipo yote yaliisha fanyika chap chap!, ila Watanzania hatuambiwi!.
Tuambiwe tuu ukweli!.
P