TRC yasema Ajali ya treni ya abiria Juni 22, 2022 iliyosababisha vifo na majeruhi ni HUJUMA

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
0d9dde19-2ed0-4590-88a5-834ed23af327.jpg

Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea Juni 22, 2022 Mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi wengine kimetajwa kuwa ni hujuma.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuna kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa ili kisionekane kama kimeegeshwa.

Kadogosa amebainisha kuwa mwendo wa treni hiyo ulikuwa mdogo na kama ungekuwa wa kasi kubwa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa vifo na majeruhi.

"Eneo lililopata ajali treni hiyo lipo jirani na makazi ya watu na mara zote treni za abiria na mizigo huwa zinapita kwa mwendo wa pole," amesema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema bado wanaendelea kuhesabu waliofariki na majeruhi wa ajali hiyo.

Honoratha hakutaka kujibu kama waliofariki ni wanne au watatu akibainisha kuwa wanaendelea kuhesabu ingawa mmoja wa watumishi wa hospitali ya Kitete aliyeomba kuhifadhiwa ya jina lake amesema waliofariki ni zaidi ya wanane.

Chanzo: Mwananchi
 
Mama nae anahujumiwa?
Labda sio hujuma kwa nchi.

Au labda amemaanisha hujuma kampuni ionekane haifanyi ukaguzi wa miundombinu.

Auu....; Labda hujuma za wezi wa mali.

Yaani ni kama 'panya road' wafunge mtaa ili waibe..... basi hawa wanakuwa 'panya reli' yao sasa. Same concept😏.
 
Uchunguzi huru utathibitisha hilo na sio hisia binafsi.
 
Tabora. Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea leo Jumatano Juni 21,2022 mjini Tabora na kusababisha vifo na majeruhi kimetajwa kuwa ni hujuma.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuna kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa ili kisionekane kama kimeegeshwa.

Kadogosa amebainisha kuwa mwendo wa treni hiyo ulikuwa mdogo na kama ungekuwa wa kasi kubwa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa vifo na majeruhi.

"Eneo lililopata ajali treni hiyo lipo jirani na makazi ya watu na mara zote treni za abiria na mizigo huwa zinapita kwa mwendo wa pole," amesema.

Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema bado wanaendelea kuhesabu waliofariki na majeruhi wa ajali hiyo na

Honoratha hakutaka kujibu kama waliofariki ni wanne au watatu akibainisha kuwa wanaendelea kuhesabu ingawa mmoja wa watumishi wa hospitali ya Kitete aliyeomba kuhifadhiwa ya jina lake amesema waliofariki ni zaidi ya wanane.
 
Shutuma kali sana hizi bila mchanyato wa concrete evidence zinaleta taharuki...

Sasa hao wahujumu kama bado wapo sisi wasafiri mnatwambia nini ? Kwamba na kesho yanaweza tokea yaliyotokea leo ?
 
Nilikua naangalia habari apa watu wanne wamefariki, Uyo aliyekiegesha kipande iko ni nani?mbona case kubwa hii,na hivi huwa awafanyi ukaguzi jamani
 
Ajali leo na masaa kadhaa washatoa majibu yao bila kufanya uchunguzi wa kina ndio maana ajali za Treni zinaendelea kuwepo na watendaji wakitoa taarifa zisizo sahihi kwenye bus wangesema mwendo kasi wa dereva...
 
Kwa hiyo idadi kamili ya waliofariki haijulikani??
 
Tabora. Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea leo Jumatano Juni 21,2022 mjini Tabora na kusababisha vifo na majeruhi kimetajwa kuwa ni hujuma.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuna kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa ili kisionekane kama kimeegeshwa.

Kadogosa amebainisha kuwa mwendo wa treni hiyo ulikuwa mdogo na kama ungekuwa wa kasi kubwa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa vifo na majeruhi.

"Eneo lililopata ajali treni hiyo lipo jirani na makazi ya watu na mara zote treni za abiria na mizigo huwa zinapita kwa mwendo wa pole," amesema.

Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema bado wanaendelea kuhesabu waliofariki na majeruhi wa ajali hiyo na

Honoratha hakutaka kujibu kama waliofariki ni wanne au watatu akibainisha kuwa wanaendelea kuhesabu ingawa mmoja wa watumishi wa hospitali ya Kitete aliyeomba kuhifadhiwa ya jina lake amesema waliofariki ni zaidi ya wanane.
Hivi huyu kadogosa mzima kweli....he is not serious at all....
He is a failure...
 
Back
Top Bottom