TRC yasema Ajali ya treni ya abiria Juni 22, 2022 iliyosababisha vifo na majeruhi ni HUJUMA

TRC yasema Ajali ya treni ya abiria Juni 22, 2022 iliyosababisha vifo na majeruhi ni HUJUMA

Huyu mkurugenzi ni mwongo mwongo. Reli Kipande cha tabora kigoma ni mbovu mbovu, treni huwa na mawimbi sana
 
Serikali wamezoea kuongea uongo hata haifahamiki ni saa ngapi wanaongea ukweli.
Halafu "wamekitoa na kukirudisha kwa kukiegesha ili kisionekane kama kimeegeshwa" ila yeye bado ameshaona!

Amtaje sasa huyo mtu maana inaonekana ana taarifa naye vizuri sana.
 
Halafu "wamekitoa na kukirudisha kwa kukiegesha ili kisionekane kama kimeegeshwa" ila yeye bado ameshaona!

Amtaje sasa huyo mtu maana inaonekana ana taarifa naye vizuri sana.

Sababu za uongo ili kuficha ubovu au uzembe wa usafiri wao.
 
Bora mtuambie wanaohujumu bwawa la Mwalimu Nyerere ni Kina nani.

Maana sarakasi zimekuwa nyingi na mradi haukamiliki.
 
Mama nae anahujumiwa?
Majuzi nilikuwa naenda Kigoma na AIFOLA EXPRESS BUS na nikapata muda mzuri tuu wa kuiona hiyo reli kwa kipande kutoka Tabora to Kigoma, tumepita maeneo kama Nguruka na mengineyo. Jamani ukweli usemwe hii reli kwa jinsi ilivyochoka mpaka unajiuliza mara mbili mbili treni inaruhusiwaje kupita? Yaani hata vile vijumba vya kukaa wafanyakazi wanaokagua reli (wanaita Gang) vina hali mbaya, vimebomoka na viko hoi bin taabani. Niliwahi pia kusafiri kwenda Moshi baada ya kufufua usafiri wa treni mwaka jana, kiukweli bado reli kwa nilivyoona mmhh haiko vizuri kwa maana ya uimara wa tuta, mataruma na reli yenyewe. Sasa tukirudi kwenye uchunguzi baada ya ajali kwa maoni yangu si sahihi kwa TRC kuruhusiwa kufanya uchunguzi wao wenyewe kwa sababu ikitokea ni uzembe wao lazima watafunika kombe mwanaharamu apite. Kuna kipindi huwa naangalia kwenye hizi discovery Channels Au geographical channels (Azam) ambapo huonyesha matukio ya ajali mbalimbali kubwa, kama ndege au treni zao inapotokea wao wana chombo maalum cha professionals mbalimbali ndiyo wanapewa hiyo kazi ya kuchunguza na kuja na recommendations ikiwemo kuwachukulia hatua wazembe wote waliosababisha ajali na pia kuweka mifumo mipya ya kuzuia ajali kama hiyo in future.
 
Tabora. Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea leo Jumatano Juni 21,2022 mjini Tabora na kusababisha vifo na majeruhi kimetajwa kuwa ni hujuma.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuna kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa ili kisionekane kama kimeegeshwa.

Kadogosa amebainisha kuwa mwendo wa treni hiyo ulikuwa mdogo na kama ungekuwa wa kasi kubwa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa vifo na majeruhi.

"Eneo lililopata ajali treni hiyo lipo jirani na makazi ya watu na mara zote treni za abiria na mizigo huwa zinapita kwa mwendo wa pole," amesema.

Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema bado wanaendelea kuhesabu waliofariki na majeruhi wa ajali hiyo na

Honoratha hakutaka kujibu kama waliofariki ni wanne au watatu akibainisha kuwa wanaendelea kuhesabu ingawa mmoja wa watumishi wa hospitali ya Kitete aliyeomba kuhifadhiwa ya jina lake amesema waliofariki ni zaidi ya wanane.
Who can prove this?? What if anajitetea kulinda ugali wake??
 
Guy's let's go to basic, au tuwarudishe wakoloni waje kututawala tena?,treni hasa ya abiria kabla haija move from station A to B ni LAZIMA kiberenge kipite kwa ukaguzi!!na hii ni main principle..kenge...why hatujifunzi why?,miaka kadhaa ya nyuma hili la ukaguzi halikufanyika ,kumbe daraja limezolewa na maji ya mafuriko na reli ikawa hewani, treni ya abiria ilipopita pale...ule uchungu upo mpaka leo, sasa my trc ceo anakurupuka na ushenzi huu kw kutuona watanzania ni mazuzu, awajibike atuachie ofisi.
 
  • Thanks
Reactions: Pep

Reli yenyewe ni mbovu na muundo wake ni wa kizamani, ni rahisi mtu kuifungua, ni vigumu kusikia reli za SGR imehujumiwa kutokana na muundo wake.

Hata kama inakaguliwa na kiberenge sio rahisi kiberenge na treni ziongozane kwa muda mmoja, kiberenge hua kinakagua kwa muda wake na treni ya abiria inapita muda tofauti, dakika kumi tu zinamtosha mtu kuifungua reli hizi za kizamani.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Na kwwnini ilianza kuanguka behewa LA mwisho badala ya injini?
Kuna vitu viwili vya kumtilia maanani. 1. engine inavuta mabehewa hivyo traction force yake ni tofauti na behewa linalovutwa. 2. Uzito wa engine ni constant ( Unabadilika kidogo kutokana na kupungua kwa dezel na kuongeza) Lakini uzito wa behewa ni variable kuna wakati watu wanakuwa wengi sana. (overloaded) Pamoja na mizigo hivyo kuifanya kuwa unstable. Kwa sababu hizo inawezekana engine ikapita sehemu salama na behewa LA abiria likashindwa hivyo likaanguka.
 
  • Thanks
Reactions: Pep

Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea Juni 22, 2022 Mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi wengine kimetajwa kuwa ni hujuma.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuna kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa ili kisionekane kama kimeegeshwa.

Kadogosa amebainisha kuwa mwendo wa treni hiyo ulikuwa mdogo na kama ungekuwa wa kasi kubwa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa vifo na majeruhi.

"Eneo lililopata ajali treni hiyo lipo jirani na makazi ya watu na mara zote treni za abiria na mizigo huwa zinapita kwa mwendo wa pole," amesema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema bado wanaendelea kuhesabu waliofariki na majeruhi wa ajali hiyo.

Honoratha hakutaka kujibu kama waliofariki ni wanne au watatu akibainisha kuwa wanaendelea kuhesabu ingawa mmoja wa watumishi wa hospitali ya Kitete aliyeomba kuhifadhiwa ya jina lake amesema waliofariki ni zaidi ya wanane.

Chanzo: Mwananchi
Waache uzembe, zaman ilikuwa lazma kiberenge kipite kifanye survey ndipo tren ipite. Karibia kila station ilikuwa na kiberenge chake.
 
Mtu ahujumu reli ili apate nini?
Huwezi jua labda kuna Mtu ana Malori yake na anaona hayapati kazi,Sasa wanaamua ku hujumu ili mizigo inayosafirishwa na treni hiyo ije kwao kwenye Malori! Vita ya Uchumi ni ngumu sana, maana rafiki yako anaweza kua adui wako wa sirini kisa Uchumi tu!!
 
Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea Juni 22, 2022 Mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi wengine kimetajwa kuwa ni hujuma.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuna kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa ili kisionekane kama kimeegeshwa.

Kadogosa amebainisha kuwa mwendo wa treni hiyo ulikuwa mdogo na kama ungekuwa wa kasi kubwa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa vifo na majeruhi.

"Eneo lililopata ajali treni hiyo lipo jirani na makazi ya watu na mara zote treni za abiria na mizigo huwa zinapita kwa mwendo wa pole," amesema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema bado wanaendelea kuhesabu waliofariki na majeruhi wa ajali hiyo.

Honoratha hakutaka kujibu kama waliofariki ni wanne au watatu akibainisha kuwa wanaendelea kuhesabu ingawa mmoja wa watumishi wa hospitali ya Kitete aliyeomba kuhifadhiwa ya jina lake amesema waliofariki ni zaidi ya wanane.

Chanzo: Mwananchi
Hujuma inawezekana, lakini uzembe unaweza kuwa ndio sababu. Anzeni na wafanyakazi wa reli kama kulikuwa na matengenezo eneo hilo kabla ya ajali. Pili kama ajali imetokea eneo la makazi ya watu, mtaa,kitongoji au Kijiji ilipotokea ajali, ufanyike uchunguzi wa kina.🤔
 
Labda sio hujuma kwa nchi.

Au labda amemaanisha hujuma kampuni ionekane haifanyi ukaguzi wa miundombinu.

Auu....; Labda hujuma za wezi wa mali.

Yaani ni kama 'panya road' wafunge mtaa ili waibe..... basi hawa wanakuwa 'panya reli' yao sasa. Same concept😏.
Panya reli ha ha ha!
 
Back
Top Bottom