TRC yasema Ajali ya treni ya abiria Juni 22, 2022 iliyosababisha vifo na majeruhi ni HUJUMA

ukiangalia report za air crash investigation mwanzo mwisho unaweza fika robo tu ukadhani hii ndio sababu ya crash, kumbe sio, huwezi kutumia akili za Kadogosa (papara) kufanya uchunguzi wa ajali yoyote
 
Wale wafanyakazi wa Railway walioondolewa miaka ya nyuma walieudishwa?

Wale walikuwa wanafanya kazi na kuishi pembezoni mwa reli
Masaa yote walikuwa wanarekebisha na hata kuinulia reli Kokoto kila wakati

Ila mwisho wangu kupanda trein unaona mpaka miti na majani yameota sana pembeni ya reli

Hii sio hujuma wasikurupuke kwa majibu ya kubuni tu
Uchunguzi bado Kwanini watoe maamuzi?
 

Hakuna behewa la abiria linaweza kuwa zito kuliko kile kichwa mkuu.... bado Trc wanatakiwa wawe wa kweli barabara ni mbovu na hawa madereva mmeanza kuwazingua kwakutokuwapa posho zao stahiki watayabinua mpaka akili ziwakae sawa
 
Ajali leo na masaa kadhaa washatoa majibu yao bila kufanya uchunguzi wa kina ndio maana ajali za Treni zinaendelea kuwepo na watendaji wakitoa taarifa zisizo sahihi kwenye bus wangesema mwendo kasi wa dereva...
Maajabu haya! Ana uthibitisho gani kuwa kipande hicho cha reli kilikatika kabla ya ajali na si baada ya ajali? Maanake treni ikianguka si ajabu reli kupinda au kukatika.
 
Maajabu haya! Ana uthibitisho gani kuwa kipande hicho cha reli kilikatika kabla ya ajali na si baada ya ajali? Maanake treni ikianguka si ajabu reli kupinda au kukatika.
Wanatoa majibu mepesi kwenye ishu inayohusu maisha ya watu na kesho watu wapande tena hilo treni kwa majibu hayo...chuma kinawaka kwenye ajali kama karatasi tuu
 
Vile viberenge vinavyopita kukagua barabara kabla treni haijapita siku hizi havipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…