TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

kwani mkijibu nini kinapungua? maana naona mnakwepakwepa tu.
 
kwani mkijibu nini kinapungua? maana naona mnakwepakwepa tu.
Sio kila swali linastahili majibu ya moja kwa moja. Hii reli ya kwenda Moshi ni ile ya kizamani sana, hivyo hutegemei speed yake iwe sawa na basi. Kwa vyovyote vile basi litakwenda haraka kuliko treni ya aina hii. Piga hesabu mwenye speed ya 30-40KM/h safari itakuwa ya masaa mangapi? lazima ujiongeze mkuu. Uzuri wake nyiani haitakutana na matuta wala tochi za barabarani wala foleni za mjini.
 
Hapo kwenye kulala sijaelewa ....
kwa hivyo unaweza kununua kiji room kabisa!?
Kwenye treni kuna vyumba vya binafsi, watu wanne na jumuia, pia kuna baa ina kaunta na stuli na meza za wanywaji pia kuna sehemu ya chakula kama hoteli vile.
Kuchimba dawa mpaka ukamwambie dereva.
 
Siku hizi ni sawa Kwa wote. Tren itaondoka saa 12.00 Joni. Na kuwalaumu saa 01.00/02,00.asubui
 
... acha hizo stori; ni nini cha ajabu kilichopo along the railway kwa mazingira ya Tanzania? Zaidi ya makazi duni na vibanda vya ajabu ajabu kuna nini cha kufanya utalii? And by the way, zaidi ya 60% ya railway Dar-Moshi iko parallel na barabara so hakuna kipya maana scene ni ileile ukitumia usafiri wa barabara!
 
Marangu Luxiury Coach iko poa sana
 
Hapo kwenye kukaa, ni mkao wa chaimaharage au wote mnatazams upande mmoja! Kuna waume za watu!
 
Wameboresha kwa sasa inatembea kwa speed yA 70km/hr sasa sijajua hadi Moshi ina cover KM ngapi ukujua hapo unafanya zile hesabu za velocity unapata masaa
 
Hii treni itakuwa poa sana ila changamoto itakuwa kwenye booking na ticketing...TRC wawekeze kwenye mfumo ambao utakuwa unamruhusu mtu kukata ticket mtandaoni, kwa mfano mfumo wa shabiby na Darlux, mtu unachagua seat, unabook na kulipia kwa simu na system inakutumia ticket yako kwenye email instantly...wakazi wa hiyo mikoa hustle za kwenda mpaka stesheni kukata ticket zitawashinda.

Mfumo huu unaweza kutoa hata ajira kwa agents kuwakatia ticket wale wasioelewa namna ya kufanya mambo mtandaoni
 
Wakata tiketi watakosa dili za kulangua tiketi (tiketi za dili). Pia waboreshe wahudumu kwenye treni isije kuwa sawa na Air Tambarare
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…