kwani mkijibu nini kinapungua? maana naona mnakwepakwepa tu.
Shida hapa sio muda wa kufika bali uhakika wa kufika kwa BEI nafuu na kuepusha watu kukodi daladala kwenda Moshi. Kama wewe unajali muda basi panda Air Tanzania, Precision Air, KQ au Euric Air. Vinginevyo tumia gari lako binafsi.
Kusafiri kwa treni ni raha hasa kwa kufanya utalii wa ndani ya nchi unapopita maeneo ya madaraja, mbuga, na mapori ambayo treni inapita. Hata mimi nilitoka Michigani kwenda Chicago kwa treni ili kufanya utalii tu sio kwa kukosa hela ya basi au ndege.