TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

Wameweka mabehewa ya aina gani?
Je safari itatumia masaa mangapi?
HAWA JAMAA ZETU HUWA WANAJALI SANA UBORA,SIO SAWA NA WALE WANAOSAFIRI NA MAJIKO YAO NA KUANZA KUPIKIA HUMO HUMO.
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Wanaojali ubora ni wale wenye Range Rover na VX-R zao ambazo zitatembelea full tank mwezi mzima wa sikukuu huku wakisubiria Yesu azaliwe na kusheherekea kupunguza mwaka mmoja wa Al-Haji Jiwe madarakani.

Hao wanaowaza kupanda mabasi ni wale kajamba nani wenzetu. Hivyo hata wakitumia daraja la tatu kusimama mradi wafike panapofuka Moshi.
 
🀣
Hahaa kwamba wanataka waanze kuoanisha speed yahiyo treni na speed ya KILIMANJARO COACH ..
Hahaa duh najikuta nacheka sana hapa nikikumbuka ile kauli ya mkulu aliyosema kama unataka speed kapande ndege ya jeshi
🀣🀣🀣🀣🀣 lini hiyo mbona sijawahi kuisikia mangi?
 
Hapo kwenye kulala sijaelewa ....
kwa hivyo unaweza kununua kiji room kabisa!?
Nop unanunua upande wa kitanda, sema nashauri wasisahau kutuwekea USB port. Lasivyo utakuwa upumbavu kukaa kwenye treni af simu inakuzimia chaji njianiπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Labda nipande kwa utalii wa ndani lakini kwa aina ya mabus luxury mapya yanayofanya safari kwenda Dar-Moshi-Arusha kwa bei ya 35-40 sioni sababu ya kupanda treni ya enzi za mkoloni.
 
Unauelewa gani kuhusu neno "UBORA"...?
 
Labda nipande kwa utalii wa ndani lakini kwa aina ya mabus luxury mapya yanayofanya safari kwenda Dar-Moshi-Arusha kwa bei ya 35-40 sioni sababu ya kupanda treni ya enzi za mkoloni.
Wasipoweka USB na A/C itakula kwao! Haiwezekani nikajipepee kwa gazeti wakati nikiongeza elfu 10 kwenye hio nauli napanda chombo full A/C na kuchaji simu yangu bila wasiwasi.

Waboreshe kwanza Cabin za mabehewa ziwe comfortable. Watu wa wiring wamejaa VETA. Wawatumie hao kufanya interior designing za infotainment systems, upholstlery n.k ili ku keep pace na mabasi ya mkoani.

Wakiendeleza uzembe wa siti ngumu kama vigoda na uchafu ndani ya cabin anguko lao halitachukua muda.
 
Kaka maelendeleo kwaajili ya umma hayatoi kipaumbele kwa maendeleo na haki ya mtu mmojammoja. Fidia ya mtu mmoja haiwezi kupambana na mahitaji ya watu wengi (umma). Mfano, mgahawa wako unaweza kufungwa au hata kubomolewa wakati wa mlipuko wa kipindupindu kama njia ya kunusuru watu dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu. Fidia utapewa hapo hapo au hata baadae ili mradi usicheleweshwe na wewe mtu mmoja.
 
Sidhan kama waliwaza hayo. TRC wawe na USB & full AC njia nzima? I doubt
 
Nop unanunua upande wa kitanda, sema nashauri wasisahau kutuwekea USB port. Lasivyo utakuwa upumbavu kukaa kwenye treni af simu inakuzimia chaji njianiπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Watawauzia Na Power bank njian
 
Sidhan kama waliwaza hayo. TRC wawe na USB & full AC njia nzima? I doubt
Watakuwa wajinga wa dunia basi, kununua USB switches na LED screens na kuzipachika kwa kila cabin sio jambo gumu. They have to do it to keep pace na wafanyabiashara wengine. Hata ikibidi first class pawe na hizo accessories plus A/C.

Sasa unapoita daraja la kwanza ukaweka viti vichache vyenye kitambaa, daraja la pili ukaweka viti vyenye ngozi what makes the difference ya madaraja? Si ni utoto huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…