TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza tena kwa safari ya treni ya Dar - Tanga - Moshi.

Safari hizo zinatarajiwa kuanza mapema mwezi Desemba. Hii italeta chachu katika sekta ya usafiri wa Kaskazini hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya. Hongereni TRC kwa kufufua reli hii ya Kaskazini.

Nauli Dar - Moshi inategemewa kuwa ifuatavyo:
- Daraja la tatu Tsh. 16,500
- Daraja la pili kukaa Tsh. 23,500
- Daraja la pili kulala Tsh. 39,100

Ndugu zangu wakina, Mushi, Mollel, Mshana, Massawe, Mbise, Laizer na wote wa Kaskazini ni wakati wenu sasa kuchangamkia fursa.
20191120_143746.jpeg
20191120_143610.jpeg
20191120_143521.jpeg
20191120_143700.jpeg
 
Kilimanjaro itakua kama mbezi,kutakua na muingiliano wa makabila mengi kama dar angalau hata wadada wa kule watachangamka kitandani waanze nao kukata viuno,nami ntakua naenda kila wiki kula nyapu zangu ambazo zipo kiporo kule
 
Itatumia masaa mangapi dar to moshi?
Shida hapa sio muda wa kufika bali uhakika wa kufika kwa BEI nafuu na kuepusha watu kukodi daladala kwenda Moshi. Kama wewe unajali muda basi panda Air Tanzania, Precision Air, KQ au Euric Air. Vinginevyo tumia gari lako binafsi.

Kusafiri kwa treni ni raha hasa kwa kufanya utalii wa ndani ya nchi unapopita maeneo ya madaraja, mbuga, na mapori ambayo treni inapita. Hata mimi nilitoka Michigani kwenda Chicago kwa treni ili kufanya utalii tu sio kwa kukosa hela ya basi au ndege.
 
Kwl kabisa mkuu nami panapomajaliwa nitalionja natumai Mombo stesheni napo patakua panafanya kazi kwahiyo kwa Korogwe sio lazima wote tushukie Korogwe mjini kwa sisi wa Mombo nandugu zangu wa Lushoto watashukia mombo nakupanda gari zakupandisha (weita ushoto,mlalo,vugha bazo ,bumbui,shambaai,Mtae.. ni iwe du)
du umenikumbusha mbai mosie iwe. Hata wale wa mashewa, magoma, usangi, mwanga, nk treni hii ni yenu pia. Wacha wenye mabasi wakohoe kikohozi kikavu safari hii, na hata zile hoteli zao za bei mbaya mule njiani zitashusha bei walahi.

Nijuavyo mimi hata watalii wangependa kupanda treni iliyo salama na nafuu kuliko kukodi magari ya gharama kubwa.

Hata wazazi wangependa watoto wao shule zikifungwa wasafiri kwa treni ya serikali kuliko mabasi.

Chamsingi tu hapa ni kununua mabehewa nadhifu yasiyo na kunguni na makondacta (TT) nadhifu waliosomea customer care.
 
daraja la tatu mnakaa wengi kwenye behewa kama vile kwenye basi na huduma nyingine chache. Lakini kuna viti pia, madirisha, choo nk. Tofauti ni idadi ya watu kwa chumba na huduma zingine za kulala na kupunzika na misosi
Ok nikajua kusimama
 
Back
Top Bottom