TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

Wasipoweka USB na A/C itakula kwao! Haiwezekani nikajipepee kwa gazeti wakati nikiongeza elfu 10 kwenye hio nauli napanda chombo full A/C na kuchaji simu yangu bila wasiwasi.

Waboreshe kwanza Cabin za mabehewa ziwe comfortable. Watu wa wiring wamejaa VETA. Wawatumie hao kufanya interior designing za infotainment systems, upholstlery n.k ili ku keep pace na mabasi ya mkoani.

Wakiendeleza uzembe wa siti ngumu kama vigoda na uchafu ndani ya cabin anguko lao halitachukua muda.
December sio tu nauli zinapanda sana bali hata mabasi hayatoshi, hiyo elfu 10 unayosema wewe inaonyesha umekosa tu uelewa wa kuidadavua hii mada. Hayo unayoyasema yatawezekana tu kama watu wengi watakuwa wamesafiri na treni hivyo mtakaobaki ndiyo mtakaoweza ku enjoy hiyo nauli ya basi unayosema.
 
Kwenye kulala hapo nimeona vitanda vinne inamaana kila kitanda mnalipia au hio bei niyachumba kizima
Chumba kizima utalipia vitanda vyote mkuu, 39,000 x 4= ________

Jibu lake ndio litakupa chance ya wewe kufanya uasherati na mwenzio bila bugudha ya abiria wengine.
 
Watakuwa wajinga wa dunia basi, kununua USB switches na LED screens na kuzipachika kwa kila cabin sio jambo gumu. They have to do it to keep pace na wafanyabiashara wengine. Hata ikibidi first class pawe na hizo accessories plus A/C.

Sasa unapoita daraja la kwanza ukaweka viti vichache vyenye kitambaa, daraja la pili ukaweka viti vyenye ngozi what makes the difference ya madaraja? Si ni utoto huo.
Ni mabasi mangapi nchini yanawasha AC njia nzima, na ni mabasi mangapi nchini yana UBS? bingwa wa kupotosha wewe, hata kwenye ndege na boats za Azam sijaona UBS.
 
December sio tu nauli zinapanda sana bali hata mabasi hayatoshi, hiyo elfu 10 unayosema wewe inaonyesha umekosa tu uelewa wa kuidadavua hii mada. Hayo unayoyasema yatawezekana tu kama watu wengi watakuwa wamesafiri na treni hivyo mtakaobaki ndiyo mtakaoweza ku enjoy hiyo nauli ya basi unayosema.
Hahahaha basi itabidi nibaki huku tu mpaka Yesu azaliwe mkuu.
 
Ni mabasi mangapi nchini yanawasha AC njia nzima, na ni mabasi mangapi nchini yana UBS? bingwa wa kupotosha wewe, hata kwenye ndege na boats za Azam sijaona UBS.
Kwa kukusahihisha kwanza nianze na USB na sio UBS!

Swala la kuwepo ama kutokuwepo liko based kwenye ushindani zaidi.

Ukiangalia BM Coach, Marangu Coach, Dar Lux hawa ndio leading brands wenye premium trim ya mabasi kwa njia hio. Sasa unapotaka kuwahamisha watu lazma uwape sababu kwanini wahamie kwako.

Ni ngumu sana kumuhamisha mtu ati kisa umemjengea nyumba mpya ambayo kimsingi ina hadhi ya chini kuliko ile alieko nayo sasa kwa facilities na kila kitu. Kwa mfano, umtoe mtu Upanga umpeleke kwenye nyumba ya room mbili porini chanika au vikindu bila kumpa sababu za msingi au ushawishi. Lazma umshawishi na aone faida ya kuhamia Chanika against Upanga, kibiashara huwa iko hivyo. Cost ya nauli iko chini ni sawa ila je, nini faida ya ku compromise speed na comfort ya basi lenye nauli kubwa against treni yenye bei nafuu? Hio ni Logic thinking!

Ni kichaa pekee ambaye atakubali kuhama katika mazingira kama hayo, isitoshe ni biashara. Sasa hili lina uhusiano wa moja kwa moja na hao mabwana Reli.
 
Kaka maelendeleo kwaajili ya umma hayatoi kipaumbele kwa maendeleo na haki ya mtu mmojammoja. Fidia ya mtu mmoja haiwezi kupambana na mahitaji ya watu wengi (umma). Mfano, mgahawa wako unaweza kufungwa au hata kubomolewa wakati wa mlipuko wa kipindupindu kama njia ya kunusuru watu dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu. Fidia utapewa hapo hapo au hata baadae ili mradi usicheleweshwe na wewe mtu mmoja.
Hiyo ni kwa mujibu wa sheria au hisia zako? Mimi nijuavyo, haki ni haki hata kama ya mtu mmoja. Justification ya watu 6 kumchinja na kumla nyama mtoto mdogo kwa kuwa hana misuli ya kujitetea kwa kisingizio cha kuogopa kufa na njaa ndio mfano unaofanana na haya unayonisimulia hapa. Nikukumbushe tena nazungumzia MTU KUFIDIWA na sio KUTOKA AU KUBAKI.
 
Shirika la Reli Tanzania, TRC linawatangazia watu wote kuwa safari za treni la biria kutoka Dar kuelekea Moshi zitarejea rasmi mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka 2019

Nauli Dar - Moshi inategemewa kuwa ifuatavyo:
- Daraja la tatu Tsh. 16,500
- Daraja la pili kukaa Tsh. 23,500
- Daraja la pili kulala Tsh. 39,100

================================

Dar es Salaam. Ikiwa tunaelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019, abiria wa Kanda ya Kaskazini watakuwa na kicheko kwao baada ya treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi itaanza Desemba.

Tayari Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa tangazo la kuanza kwa usafiri huo na kuthibitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaac Kamwele.

Waziri Kamwele amesema kama Serikali imefurahi kufikia hatua hiyo ukizingatia treni hiyo ilikuwa ianze tangu Septemba 2019.

Hata hivyo, amesema kutokana na changamoto za kunyesha mvua na kusababisha baadhi ya miundombinu ikiwemo ya reli kuharibika katika ukanda huo wa Kaskazini ndio maana kukawepo na uchelewaji wa kuanza kwake.

“Sasa ile tabia ya wafanyabiashara pale stendi ya ubungo kulangua abiria tiketi wakati watu wakienda kula sikukuu na ndugu zao itakoma, kwani hata mimi ilishanikuta na kama Serikali tulikuwa tunahangaika kutafuta njia ya kukomesha vitendo hivyo na ujio wa treni hii ya abiria utasaidia,” amesema

Kuhusu nauli, Waziri Kamwele amesema wameacha ileile iliyokuwa ikitumiwa tangu kusitishwa kwa usafiri huo na ndio maana hawakuitisha hata kikao cha wadau kuhitaji maoni ya nauli.

Wakati kuhusu uwezo wa kusafirisha abiria, amesema itategemea na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) itakavyowapangia japokuwa uwezo wa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kimoja cha treni kikiwa na uwezo wa kubeba mabehewa 20.

“Katika idadi ya abiria tutakaobeba tutasubiri Latra watuambie kwa kuwa wenyewe ndiyo wataalam wa usafiri lakini uwezo wetu kwa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kikiwa na nguvu ya kubeba mabehewa 20,”amesema.

Treni hiyo itakayopita Korogwe mkoani Tanga, TRC imetangaza nauli zake ambapo Dar es Salaam hadi Korogwe daraja la tatu itakuwa Sh10,700, daraja la pili kukaa Sh15,300 na daraja la pili kulala Sh25,400.

Wakati kwa abiria watakaotoka Dar es Salaam kwenda Moshi daraja la tatu itakuwa Sh16,500, daraja la pili kukaa Sh23,500 na daraja la pili kulala Sh39,100.
View attachment 1267371
Wanavizia jamaa wanavoenda kuhesabiwa
 
Back
Top Bottom