Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
TAARIFA KWA UMMA
HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE
Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.
Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme
Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.
Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Jamila Mbarouk
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO