Kama hutojali na kutokana na kazi unayoifanya ya kilimo Cha mpunga ungepata pawatila Siam Kubota. Kwa upande wa trekta usijali kikubwa angalia spea/ vipuli zake zinaingiliana na kampuni gani na upatikanaji wake upoje. Baadhi ya trekta likizingua unageuza kichanja hata Kama unahela, na nyingine huwa zinaharibika Mara Kwa Mara hasa pampu.
Trekta ukinunua Kwa keshi itakua poa Sana kuliko kukopa. Mfano Efta ilikua ukikopa marejesho ni Kila mwezi Kwa miaka mitatu na Kuna vigezo vya shamba na kiingilio lakini ukifeli marejesho hata Kama umebakiza miezi miwili liwe lako wanabeba.
Ukinunua pia utatakiwa kununua majembe na rota na angalau trela kwaajili ya kubebea mizigo wakati wa kiangazi au uwe unakodi.
Kuhusu pawatila utapata Kwa milioni 12 ikiwa complete na Kama ukiwa na pesa za kutosha unaweza kununua mbili. Ukiwa nazo mbili hapo mwenye trekta mnakula league na unaweza kumzidi kidoogo kutokana na wewe kutumia mafuta kidogo na PAWATILA kufanya kazi hata maeneo mapya au yasiyofikika Kwa trekta.
Kwa trekta roho ya paka ni New Holland, masey Ferguson, valtra, Kubota, ford na nyingine nyingi ambazo spa zake zinapatikana.
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app