TREND YA AFRICAN POLITICS. Historia Itajirudia Tanzania?


Ahsante sana kwa michango yako yote kwenye post hii,pia ahsante kwa huu mtizamo wako kuhusu Dr Slaa.
Lakini kwa swali langu la hapo juu nilipenda huyu Bi dada aje ajibu mwenyewe.....maana hahisi anakitu fulani
chini ya karpet
 

And at a given time of election ..the voting will only be made to the available candidates ... and*sometimes.. voters will select the party not the candidates!*
 


Kama ulivosema JG naona ni lugha gongana… kweli naona sikukupata in the lines ulikua unapita. Nimekupata pia why uko reluctant kwamba ni vigumu kuungana vyama… Uloongea yoote nimekupata na where it is coming from. Suggestion yangu ya vyama kuungana ni the simple fact kua Imagine kuna CCM katika kugombea Vs only one United Chama….. Naamini kua effect itakua kubwa na pana na kwamba itakonga mioyo ya Watanzania wengi with Great belief kua the VYama ni genuine…. Napenda pia nigusie hio ya Bishanga…. Kumbuka kua tukubali kwamba the Majority Tanzanians katika kuchagua Chama ni wachache ambao ni wajuvi enough to be interested in Knowing the IMANI, ITIKADI, MUONO & PROGRAME…. Wengi wapo more reliant na what is said by the Viongozi pale wanapokua Jukwaani na acha tu ile ya Siasa ya Kijiweni…. Sababu majority wanasema this is Good, then you regard it as good bila hata kujua what is so good about it…
 


AJ... I Love this post... its logic, its depth and the absolute Truth (IMO);
Na hio in Green... hio paragraph kwa yeyote ambae atasoma, atajua sasa
kua.. hio ndio inanifanya niwe alertively interested.... and thus this post.....
 
Asha,
Kwanza nakupongeza kwa mada moto na yenye changamoto.
Kutokana na mada yako, changamoto niionayo ni kwamba, katika muktadha wa siasa za Kiafrika nimeone kuna jambo moja linajirudia sana.
Ni lini tutajifunza na kuwa wa kweli? Ukiangalia nchi nyingi, kinachotokea ni "kupokezana vijiti" kwenye viti vya enzi.Hii inanifanya nijiulize maswali yafuatayo:
1. Je, nchi za kiafrika ziliwezaje kuwa na utawala wa kijadi wenye "maadili"? Najua machifu nao walikuwa na vimbwanga vyao.Lakini utawala uliheshimiwa, ulifuata miiko na kanuni hata kama kulikuwa na matabaka.
2. Je kulikuwa na ulazima kuiga mifumo ya utawala ya wageni? Ingekuwa vipi kama baada ya uhuru nchi hizi zingerudia ile mifumo ya kichifu hata kama ni kuifanyia "ukarabati" iweze kufit mazingira! Najua argument moja itakuwa -ukabila na kufanya nchi isitawalike. Still -this is food for thought.
3. Inakuwaje kila utawala unalaumiwa kwa maovu na hata pale mfumo na utawala mpya unapokuja mambo yanakuwa yaleyale- kama ni ufisadi unaendelea n.k
4. IS IT WORTHY to fight so hard kubadili viongozi/uongozi ilhali watakaokuja nao hawatakuwa na jipya?

Hayo maswali manne yananipelekea kuuliza SWALI MOJA LA JUMLA:
Je wananchi wanajua wanachokitaka? Kama wanajua, je wanajua namna ya kukipata?

Asha utanisamehe sana kwa kuongeza chumvi kwenye kidonda.
 

na hiyo ndo mistake ya waafrika
we are looking for heroes....wenzetu kwenye siasa na uchaguzi
they are not looking for heroes.they are looking for 'public servant'
akiweza haya,asipoweza ni kumtimua asap.....but sisi tuna ushabiki mno..
leo ukimwambia mtu kuhusu 'kukosoa wapinzani now kabla hawajaingia madarakani'
anafikiri uko chama tawala....they are not our heroes....
wapinzani watazamwe kama 'JOB SEEKERS' na sio WAKOMBOZI'
je watatufaa?wasipotufaa nguvu ya kuwatimua ,tumeiandaa?????
 
Mkuu AJ nimeitikia mwaliko wako bado nadadavua mada...!

Mkuu nakusoma,*

Pia Mimi niko kwenye tafakari .. kuna kitu hakijanikalia vizuri. Nilifikiri utafumbua. Naona kama kuna ukweli fulani usiopingika kirahisi kuwa bila kujali Chama, bila kujali Nchi ... Kwenye bara letu kuna kasoro amabazo zinajirudia. Kama mada ilivyokaa ina mifano ambayo inaliwakilisha jambo hili na kulifanya lieleweke ... Kazi ni jinsi ya kulipatia ufumbuzi Tatizo hili.

Nikiangalia CCM itanfanya nini kujiweka sawa hadi kunusuru vipengele muhimu vya UTU kama HAKI, USAWA na AMANI ya kila mwanachi kwa hali ilivyo sasa ndani ya chama hicho sipati picha ya haraka kufikia hapo.

Challenge inakuja ..Je wapinzani wakiwa na fursa ya Kutwaa madaraka .. Katika hali ya ukweli KABISA ... Watafanyia nini Tatizo la Kuvunjwa misingi ya UTU wa Taifa ... kama ilivyoainishwa kwenye katiba ...au kama tulivyoongolea kule!!?

Wataanza wapi kuwachukulia HATUA wale wote wanaodhaniwa kuwa walifanya makosa ya dhati kabisa ... haswa kwenye Ufisadi wa dhahiri kabisa... Kwenye post moja nimesema CCM wadhubutu ... kuchukua maamuzi magumiu ... Wajisafishe ... Mhh ..Sijui. Lakini kwa upande wa pili Hivi Hawa Chama cha upinzani kikichukua madaraka ...Watakuwa na uwezo wa kudhubutu kwa dhati kabisa kutekeleza hilo ..? Na kwa kiasi gani kweli kwenye hali hiyohiyo wanaweza kuwa tofauti na hao waliondoka madarakani..? .. Bado natafakari...
 
Nimeipitia kwa makini hii thread kuna mambo mengi ya msingi kwa siasa zetu za Afrika, kwanza nakupa pongezi AshaDII.
Tuna safari ndefu sana wakati mwingine mtu unafikiri huu mfumo wa Demokrasia kwa Afrika hautufai labda tuwe na mfumo mwingine kwanza, tunatakiwa tupate viongozi wazalendo
 

Ahsante sana kwa michango yako yote kwenye post hii,pia ahsante kwa huu mtizamo wako kuhusu Dr Slaa.
Lakini kwa swali langu la hapo juu nilipenda huyu Bi dada aje ajibu mwenyewe.....maana hahisi anakitu fulani chini ya karpet


Mshiakachuma... Naomba utanisamehe na tuliache pending... Only that nakushukuru kwa kugusia for did not fikiria kabisa kua kuna member atakua amenote hilo; Hivo basi naomba sana you understand kua yawezekana ni instict na we close on the subject. Natangulisha Shukrani.
 



The words in this post naona ipo kabisa in-conjuction with the reason behind the Thread it self.... Thank you for nimeikubali to the dot.... Haina maana kua yajulikana they have millions of money in cash and assets alafu waachiwe waendelee kuzitumia kifamilia bila ku retrieve!! Nonsense kwa kweli....
 

Ukizungumizia Coalition ya chama pinzani sasa i get... i thot Coalition kati ya CCM na CDM.... Thus concur the thought... In fact i support it all the way!! Kuhusu Banda... ndo maana nikasema ni a somehow lenient leader, for believe me you ingekua sio kifo cha Mwanawassa hata huo Uraisi asingeonja... hana leadership qualities....
 


WoS Asante for the acknowledgement na mchango ulotoa for Umegusia maswala ya muhimu na Msingi…. Nimependa kua umejaribu kuangalia wapi exactly tumetoka in terms of leadership na the way hao babu zetu walikua na nidhamu dhidi ya uongozi… I am taking questions 1, 2, 3 as Rhetorical and sticking to number 4 which to me has really touched me.

Hio number four ni muhimu mno kuweza li observe for hio ndi ime rise my whole interest. Na ndio maana nilichukua inchi jirani zetu as Mifano halisi and in a way ka vile a Case study. Narudi pale DRC… Sababu kubwa ya wananchi kuweza M-support Kabila Snr nguvu zake shidi ya Kumng'oa Mobutu ilikua kujilimbikizia kwa mali kwa Mobutu na wale wake wa karibu alokua anawa favour…. But Kabaila Snr alipoingia Uongozi alivunja ahadi zoote (kama vile kuwepo kwa uchaguzi wa huru na haki na kuhakikisha mwanachi wa kawaida anakula matunda ya nchi yake); Badala yake alidiriki tamka "His years of struggle were like applying fertilizer to the field and thus it was time to Harvest" No wonder kifo kikamkuta!!

Hivo basi kama incase CCM wakatolewa na CDM ama chama kingine kikaja jua kua itakua haina maana kabisa kama everything from governance to all its systems zitakua vile vile….

WoS the chumvi kwenye Kidonda was worth it.... THANK YOU....
 
Leo nimepata muda wa kukusoma AshaDii pamoja na wachangiaji wengine na kutambua kwamba sii kwamba wananchi hawafahamu matatizo yetu bali ni sawa na wafungwa walioko magereza wakijaribu kutafuta uhuru ndani ya gereza..hawa siku zote hadithi, nyimbo na ngonjela husaidia kuwapa tumaini jipya lakini haiwapunguzi kifungo chao...

Watanzania wenzangu swala la kutafuta coalition between vyama haliwezekani, na haiwezekani kwa sababu vyama kama vyama havina matatizo isipokuwa WATU wenyewe ndio hatuaminiani na kama hakuna trust hutuwezi kuweka UMOJA wa aina yoyote ile. Hii ndio athari kubwa ya Ukoloni, na hii ndio atahri kubwa ya Utumwa kwa mtu mweusi kiasi kwamba tumeondoa utamaduni wa kuaminiwa kama kigezo cha mafanikio.

Hili sii swala la wanasiasa pekee bali ni ahat sisi wananchi, leo hii kumpata mtu wa kumwamini Tanzania ni sawa na kuokota lulu.. kuna rafiki yangu mmoja alinambia ukimpata mtu wa kuaminika ukamtaka awe mshirika wako, atakuuliza -Nitakwaminije?.. kwa nini afanye kazi na wewe ikiwa wewe upo ktk fungu la kutoaminika?.

Na kweli, historia inajirudia kuonyesha jinsi sisi waafrika tusivyoweza kutoaminika..Ni sisi tuliodanganywa kwa shanga wazungu na waarabu wakaendesha biashara ya Utumwa, tukatawaliwa na hata Machief wetu kukubali kufanya kazi na wakoloni wakipewa wadhifa mdogo sana ili wakoloni waweze kutu control...Hawa walikuwa wenzetu waliotuuza tukatawaliwa, na baina yao Machief wenyewe hawakuaminiana, leo hii mchezo ni ule ule tunashindwa kumwamini Dr.Slaa au Lipumba kuwa mmoja wao anaweza kuleta mabadiliko isipokuwa kwa kutokana na kabila au dini yake (kutoaminiana). Alitazamwa hivyo Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK na hata viongozi wote wa kiafrika mtihani wao mkubwa ulikuwa kabila na imani zao za dini kuwa kigezo kikubwa cha utawala wao. Kwa maana hiyo itikadi asili ya mwafrika ni mila na desturi sio hizi siasa za Kushoto na Kulia.

Binafsi naamini kabisa kwamba mabadiliko tusiyategemee kutoka kwa vyama vyetu bali sisi wenyewe tutakapo weza kuweka imani zetu ktk mabadiliko tunayoyataka. Kama tunataka CCM iondoke madarakani tunatakiwa kupima ni chama gani chenye uwekezano mkubwa wa kumwondoa CCM na tukiunge mkono. Leo hii ni Chadema, nashindwa kuelewa mtu anapokiunga mkono CUF au NCCR wakati anajua fika kwamba vyama hivi haviwezi kushinda uchaguzi na lengo ni kumwondoa CCM madarakani. Why vote for them na wengine bado wameweka tumaini kwa CCM kama sii kutoaminiana.

Na maadam hatuaminiani siwezi kushawishika na mtu yeyote anayesema Dr.Slaa haaminiki wakati hatuna utamaduni wa kuamini mtu mwenye mila na desturi tofauti na zetu.. Na tumekumbatia utamaduni huo kwa sababu sisi wenyewe hatuaminiki toka enzi za utumwa, ukoloni na tunaendeleza libeneke. Viongozi wetu ambao kwa asili walikuwa maskini, hawakupitia mafunzo ya Uzalendo, Utaifa wanapopata mwanya wa kuliongoza taifa lisilo kuwa na waaminifu hujikuta akiharibu zaidi kwa sababu sisi wenyewe tulishaweka malengo ya uchaguzi wetu.

JK alishinda uchaguzi kwa kuaminiwa na watu wasioanika! na matokeo yake ndio UFISADI ukapata nafasi kushamiri lakini kama tungejifunza toka wakati wa Mwinyi hadi Mkapa kwamba CCM ilipoteza dira, ilitupa mbali misingi ya Ujenzi wa Taifa letu kuutukuza UTU na bado tukaendelea kukichagua chama hicho kwa dhana dhaifu ya kwamba bora ya Zimwi likujualo, hatutaweza jifunza kwa lolote jingine isipokuwa sisi wenyewe kurudisha imani zetu na TRUST hata kama sisi wenyewe hatuaminiki...

- Sijui kama nimeeleweka!
 
Well said Mkandara......umeeleweka vizuri sana! yaani hakuna ulichobakiza kwenye upembuzi wako huu!
Ubarikiwe sana na usiku mwema! ALL EYEZ ON IGUNGA NOW.....hakuna kulala hadi kieleweke.
 

...*Hivo basi kama incase CCM wakatolewa na CDM ama chama kingine kikaja jua kua itakua haina maana kabisa kama everything from governance to all its systems zitakua vile vile....

... *Nimeipitia kwa makini hii thread kuna mambo mengi ya msingi kwa siasa zetu za Afrika ...
Tuna safari ndefu sana wakati mwingine mtu unafikiri huu mfumo wa Demokrasia kwa Afrika hautufai labda tuwe na mfumo mwingine *...


.... IS IT WORTHY to fight so hard kubadili viongozi/uongozi ilhali watakaokuja nao hawatakuwa na jipya?*SWALI MOJA LA JUMLA:*Je wananchi wanajua wanachokitaka? Kama wanajua, je wanajua namna ya kukipata?*

Tatizo la msingi ndio hilli! Kama lilivyogusiwa na memebers mabalimbali!!!!*

Kwamba Tunahitaji mabadilko ? Jibu ni ndio! Tanazania kwa sasa ni kweli imefikia mahali nilazima mabadiliko ya uongozi yafanyike ... Bado Jibu ni ndio. Kwa ujumla Sioni mtu anayeona kuwamabadaliko hayahitajiki.*

DILEMMA au niseme KIGUGUMIZI kilipo, kwenye kutekeleza MABADILIKO tumesha kiona.

SASA INAKUWAJE? ... Nafikiri hapa tusaidiane ..!

1. Tubakie hapa tulipo, yaani tusitishe mabadiliko yote?

2. Tufumbe macho na kusema tunakubaliana na kitakachokuja mbele ya safari.

3. AU kwa sababu ni lazima kwa wakati wowote kuwa na Uongozi, na ili kufikia Uongozi uliotukuka ni MCHAKATO ... na kwa namna yeyote ..Hautafikiwa Leo au kesho .. Basi Tukabaliane kuwa kila mara kwenye uchaguzi tuwakubali wenye afadhali KWA WAKATI HUO ... tukisubiri ... Miaka mingi ijayo kwa mchakato kutuletea Kile amabacho kinahitajika... yaani the change we need!!
 
Kwanza nianze na lengo la mtoa mada: Nikijaribu kuweka kwa maneno machache nini kimemsukuma mtoa mada kuleta mada hii ni kwamba:- Kutokana na historia ya mabadiliko ya uongozi wa kisiasa kwenye nchi kadhaa za kiafrika kutoleta mabadiliko yaliyotarajiwa (kama mapambano dhidi ya rushwa na uboreshaji wa maisha ya raia wake), Je kuna haja ya kufanya mabadiliko/kuweka matumaini kwenye mabadiliko hayo hapa kwetu? Jibu ni ndiyo tunahitaji mabadiliko.

Kabla sijaeleza kwanini tunahitaji mabadiliko, ningependa kuelezea masuala kadhaa, kwanza ni kwa kurudi kwenye historia yenyewe na kugusia kidogo mifano uliyotoa; Ukiangalia historia ya Afrika kabla ya uhuru,wakati wa kutafuta uhuru na baada ya Uhuru kuna mshabihiano(kufanana) wa karibu sana. Hoja yetu hapa imejikita kwenye historia ya Afrika baada ya Uhuru.

Sasa ukiyatazama mataifa ya Afrika mara tu baada ya Uhuru yalikua na kazi kubwa mbili;
  1. Kujenga Utaifa - hii inatokana na historia ya mataifa ya Afrika kuwa na mikusanyiko ya makabila mbalimbali
  2. Kujenga Mifumo ya Uongozi na Demokrasia - Hapa masuala ya ni siasa za aina gani (ideology) zifuatwe
Bila kugusia mambo mengi tunaona kuwa mwanzoni nchi nyingi za kiafrika zilikumbatia mfumo wa chama kimoja cha Siasa ili kuleta Umoja na mshikamano miongoni mwa watu wao hivyo kujenga UTAIFA. Mwishoni mwa miaka ya 80 vuguvugu la kushinikiza mfumo wa vyama vingi lilianza na nchi nyingi za Afrika zikaanza ku "adapt" mfumo huu.

Sasa hapa something very interesting kinajitokeza: Kumbuka tuna vyama vilivyodai uhuru kama UNIP - Zambia, KANU - Kenya, TANU/CCM - Tanzania na ZANU-PF Zimbabwe, vyama hivi viliwapa tumaini kubwa sana wananchi wake kuwa baada ya uhuru maisha yao yataboreshwa kwa kiwango kikubwa lakini matokeo yake ni kunyume chake.

Miaka takribani 20 baada ya uhuru mfumo wa vyama vingi unaingia Zambia na Kenya tunashuhudia mabadiliko ya uongozi wa kisiasa ila hakuna kinachobadilika kwa upande wa kero za wananchi au mabadiliko yapo ila si ktk kiwango kilichotarajiwa, kwanini? hilo nitaliacha kwasasa..... Ila narudi kwenye suala la mabadiliko..Je tunayahitaji? jibu ni NDIO

Kwanini?
  1. Tuliukubali wenyewe mfumo wa vyama vingi ili tuwe na uchaguzi kwamba chama kimojawapo kituongoze hasa pale kilichopo madarakani kinaposhindwa kutimiza matarajio yetu - CCM imeshindwa kufikia matarajio yetu hivyo tunahitaji mabadiliko ya Uongozi
  2. Kuondoa dhana ya Uhodhi wa madaraka (monopoly) kwa CCM ili kujenga utamaduni wa kupokezana madaraka ya nchi baina ya vyama - hapa ndipo utaona kuwa wenzetu Kenya na Zambia wamefanikiwa katika hili na hapa ndipo ukomavu wa demokrasia hii ya vyama vingi tuliyojichagulia wenyewe unapopatikana.
Sasa swali la WOS "IS IT WORTHY to fight so hard kubadili viongozi/uongozi ilhali watakaokuja nao hawatakuwa na jipya?" Hivi how do we know exactly kama hao watakaokuja hawatakuwa na jipya? If a scenario is true in Kenya/Zambia is it necessarily true in Tanzania? Lazima tuwe na imani (kama alivyosema Mkandara) na uthubutu wa kufanya mabadiliko kwa maana vyama hivi ni vyetu tumevilea kwa kodi zetu kupitia ruzuku wanazopata hivyo tuvitumie kutupatia Uongozi mbadala.
 
It's the constitution!! There's no check and balance.
The notion that ministers should be MPs is outdated and the Parliament needs to confirm Ministers, Deputy Ministers,PS, RC..... etc.
The judiciary,especially Supreme court justices needs to be confirmed by the Parliament too.
This will help in getting rid of the scandalous politicians and put technocrats where they belong.
Otherwise, CDM,CUF,NCCR..they are just the same under this constitution. Let the "people" get more involved.
 


Mkandara na MawazoMatatu, Nimewasoma!!

Kuwa ninachokiita Dilemma kina utatuzi ... na utatuzi huo ni IMANI! Kwa sasa nisubiri kabla ya kulijadili jambo hili! Nikitegemea kutakuwa na mawazo na mitizamo mingine mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…