Leo nimepata muda wa kukusoma AshaDii pamoja na wachangiaji wengine na kutambua kwamba sii kwamba wananchi hawafahamu matatizo yetu bali ni sawa na wafungwa walioko magereza wakijaribu kutafuta uhuru ndani ya gereza..hawa siku zote hadithi, nyimbo na ngonjela husaidia kuwapa tumaini jipya lakini haiwapunguzi kifungo chao...
Watanzania wenzangu swala la kutafuta coalition between vyama haliwezekani, na haiwezekani kwa sababu vyama kama vyama havina matatizo isipokuwa WATU wenyewe ndio hatuaminiani na kama hakuna trust hutuwezi kuweka UMOJA wa aina yoyote ile. Hii ndio athari kubwa ya Ukoloni, na hii ndio atahri kubwa ya Utumwa kwa mtu mweusi kiasi kwamba tumeondoa utamaduni wa kuaminiwa kama kigezo cha mafanikio.
Hili sii swala la wanasiasa pekee bali ni ahat sisi wananchi, leo hii kumpata mtu wa kumwamini Tanzania ni sawa na kuokota lulu.. kuna rafiki yangu mmoja alinambia ukimpata mtu wa kuaminika ukamtaka awe mshirika wako, atakuuliza -Nitakwaminije?.. kwa nini afanye kazi na wewe ikiwa wewe upo ktk fungu la kutoaminika?.
Na kweli, historia inajirudia kuonyesha jinsi sisi waafrika tusivyoweza kutoaminika..Ni sisi tuliodanganywa kwa shanga wazungu na waarabu wakaendesha biashara ya Utumwa, tukatawaliwa na hata Machief wetu kukubali kufanya kazi na wakoloni wakipewa wadhifa mdogo sana ili wakoloni waweze kutu control...Hawa walikuwa wenzetu waliotuuza tukatawaliwa, na baina yao Machief wenyewe hawakuaminiana, leo hii mchezo ni ule ule tunashindwa kumwamini Dr.Slaa au Lipumba kuwa mmoja wao anaweza kuleta mabadiliko isipokuwa kwa kutokana na kabila au dini yake (kutoaminiana). Alitazamwa hivyo Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK na hata viongozi wote wa kiafrika mtihani wao mkubwa ulikuwa kabila na imani zao za dini kuwa kigezo kikubwa cha utawala wao. Kwa maana hiyo itikadi asili ya mwafrika ni mila na desturi sio hizi siasa za Kushoto na Kulia.
Binafsi naamini kabisa kwamba mabadiliko tusiyategemee kutoka kwa vyama vyetu bali sisi wenyewe tutakapo weza kuweka imani zetu ktk mabadiliko tunayoyataka. Kama tunataka CCM iondoke madarakani tunatakiwa kupima ni chama gani chenye uwekezano mkubwa wa kumwondoa CCM na tukiunge mkono. Leo hii ni Chadema, nashindwa kuelewa mtu anapokiunga mkono CUF au NCCR wakati anajua fika kwamba vyama hivi haviwezi kushinda uchaguzi na lengo ni kumwondoa CCM madarakani. Why vote for them na wengine bado wameweka tumaini kwa CCM kama sii kutoaminiana.
Na maadam hatuaminiani siwezi kushawishika na mtu yeyote anayesema Dr.Slaa haaminiki wakati hatuna utamaduni wa kuamini mtu mwenye mila na desturi tofauti na zetu.. Na tumekumbatia utamaduni huo kwa sababu sisi wenyewe hatuaminiki toka enzi za utumwa, ukoloni na tunaendeleza libeneke. Viongozi wetu ambao kwa asili walikuwa maskini, hawakupitia mafunzo ya Uzalendo, Utaifa wanapopata mwanya wa kuliongoza taifa lisilo kuwa na waaminifu hujikuta akiharibu zaidi kwa sababu sisi wenyewe tulishaweka malengo ya uchaguzi wetu.
JK alishinda uchaguzi kwa kuaminiwa na watu wasioanika! na matokeo yake ndio UFISADI ukapata nafasi kushamiri lakini kama tungejifunza toka wakati wa Mwinyi hadi Mkapa kwamba CCM ilipoteza dira, ilitupa mbali misingi ya Ujenzi wa Taifa letu kuutukuza UTU na bado tukaendelea kukichagua chama hicho kwa dhana dhaifu ya kwamba bora ya Zimwi likujualo, hatutaweza jifunza kwa lolote jingine isipokuwa sisi wenyewe kurudisha imani zetu na TRUST hata kama sisi wenyewe hatuaminiki...
- Sijui kama nimeeleweka!