Treni Mchongoko yawasili nchini

Treni Mchongoko yawasili nchini

Tunataka na miundombinu iliyobora, treni haipendezi kupita maporini hatuoni kwa wenzetu
 
Sawa mmetuletea mchongoko na kwa kutuliwaza mmeandika hapo pembeni "NYERERE EXPRESS" ikimaanisha hiyo itakuwa na mwendo wa uhakika, labda tuseme 180kph!.

Kuna mdau kaniambia kwa kuning'oneza kuwa unaweza kukuta ni ile ile ila wamebadiri uso na muonekano ili kuturubuni.

Nimemjibu, subiri tuone mwendo wake hapo ndipo tutaanza kumshukuru mzazi wetu kama ilivyo hada, 😃!.
 
Kuna mdau kaniambia kwa kuning'oneza kuwa unaweza kukuta ni ile ile ila wamebadiri uso na muonekano ili kuturubuni.
Kwani hata msiporubunika mtawafanya nini?
 
Kuna mdau kaniambia kwa kuning'oneza kuwa unaweza kukuta ni ile ile ila wamebadiri uso na muonekano ili kuturubuni.

Nimemjibu, subiri tuone mwendo wake hapo ndipo tutaanza kumshukuru mzazi wetu kama ilivyo hada, 😃!.
Afu baada ya mda kuna chawa atajisahau na kuropoka kuwa wameipimp.
 
TU WEPESI KWENYE KUANZISHA VITU
WAGUMU NA HATUWEZI KUSIMAMIA.
REJEA SIMULIZI YA MABASI YA MWENDOKASI
NDANI YA MIAKA 5 IJAYO ATATAFUTWA MWEKEZAJI,
PENGIONE NI HAO HAO DP WORLD
 
Kuna mdau kaniambia kwa kuning'oneza kuwa unaweza kukuta ni ile ile ila wamebadiri uso na muonekano ili kuturubuni.

Nimemjibu, subiri tuone mwendo wake hapo ndipo tutaanza kumshukuru mzazi wetu kama ilivyo hada, 😃!.
Tumshukuru samia kwa mchongoko
 
Treni oli iitwe ya mwendokasi lazima ikimbie kuanzia 200km/hr ma kuendelea.Hii ya 160km/hr ipo kundi gani? Tena umeme?
 
Treni oli iitwe ya mwendokasi lazima ikimbie kuanzia 200km/hr ma kuendelea.Hii ya 160km/hr ipo kundi gani? Tena umeme?
Kuna mahali wamesema still ni hatua za mwanzoni kwanza, lakini treninis capable of 200km/h +. Just miundo mbinu bado
 
Hongera wote mliohusika na ujenzi, Railway na watanzania ambao kodi zenu zimetumika na zitatumika kulipa mikopo.
Serikali ipunguze gharama za safari ili watanzania wengi watumie usafiri huo
 
Seti ya kwanza ya EMU
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa ya kuwasili katika Bandari ya Dar es salaam kwa seti ya kwanza ya Treni ya kisasa ya EMU, Vichwa vitano vya umeme na Mabehewa matatu ya Abiria ( iliyowasili ni seti moja ambayo kikawaida hufungwa behewa nane na vichwa viwili kimoja mbele na kimoja nyuma).

Taarifa iliyotolewa leo April 03,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano- TRC, Jamila Mbarouk imeeleza yafuatayo ——— > “Kupitia TRC ilifanya manunuzi ya seti kumi (10) za Treni za kisasa zijulikanazo kama Electric Multiple Unit (EMU) kutoka kwa Watengenezaji kampuni ya Hyundai Rotem ya Korea Kusini, seti moja ya EMU ina uwezo wa kubeba Abiria 589 na kutembea kilomita 160 kwa saa, EMU ni treni iliyoundwa kwa teknolojia ya kisasa inayomuwezesha Abiria kupata huduma kama Wi-FI, sehemu za kukaa Watu wenye mahitaji maalum n.k”

“Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania imepokea jumla ya Mabehewa 65 ya Abiria, Vichwa 9 vya umeme na seti moja ya EMU, seti nyingine za EMU zitaendelea kuwasili kila mwezi hadi Oktoba 2024, kuwasili kwa vitendea kazi kunaifanya TRC kuwa tayari kuanza huduma za usafirishaji Abiria katika reli ya kiwango cha kimataifa”

“Maendeleo ya mradi wa SGR awamu ya kwanza yamefikia asilimia 98.90 kwa kipande cha Dar es salaam - Morogoro (KM 300), asilimia 96.51 kipande cha Morogoro - Makutupora, asilimia 13.98 kipande cha Makutupora - Tabora, asilimia 5.44 kipande cha Tabora - Isaka, asilimia 54.01 kipande cha Mwanza - Isaka
View attachment 2953191
Pamoja na hayo sisi tunaomba muweke nauli rafiki kwa kulingana na usawa
 
Back
Top Bottom