Treni ya Abiria imepata ajali kwa kugongwa na Lori maeneo ya Tabora leo Mei 28, 2025

Treni ya Abiria imepata ajali kwa kugongwa na Lori maeneo ya Tabora leo Mei 28, 2025

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
WhatsApp Image 2025-05-28 at 16.12.05_661fc361.jpg
Inadaiwa kuna Treni ya Abiria imepata ajali kwa kugongwa na Gari maeneo ya Tabora huko, wenye taarifa zaidi watujuze.

=============================


Abiria wa Gari Moshi wamenusurika kifo kufatia ajali ya lori la mizigo lenye trela Namba T 933 DMF lililokuwa likitokea Tabora kuelekea Wilayani Urambo kuigonga treni hiyo iliyokuwa ikitoka Kigoma kuelekea Dar es salaam katika barabara kuu ya Urambo - Tabora kwenye maeneo ya Kata ya Mbugani, mkoani Tabora hali ilisababisha kukwama kwa safari kwa muda pamoja na uharibifu wa vyombo hivyo.

Ajali hiyo imetokea Leo Mei 28,2025 ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni uzembe wa dereva wa lori kwani hakuzingatia sheria za barabarani kwenye maeneo ya makutano ya barabara hizo, kwamba hata alivyopigiwa honi na treni hakusimama.

Abiria hao wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwatafutia njia mbadala ya usafiri ili waweze kuendelea na safari.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora SACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuainisha hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu na kwamba wanaendelea kufanya utaratibu wa kuwawezesha abiria hao kuendelea na safari.
 
Back
Top Bottom