A
Anonymous
Guest
Sababu ya kwanza ambayo nimeisikia na imekuwa ikitajwa ni kuwa reli ilikuwa inafanyiwa marekebisho ya hapa na pale.
Pili baada ya kukamilika marekebisho hayo, treni ilifanya kazi siku mbili, kilichofuata baada ya kunyesha kwa mvua mfululizo Bwawa la nyumba ya Mungu lililopo Moshi Mkoani kilimanjaro likajaa maji na hivyo kusababisha maji kutiririka na kujaa katika njia za reli.
Hali hiyo ikachangia usafiri wa Treni usitishwe kwa muda hadi hali itakapokaa ndipo usafiri wa treni utarudi tena.
Baadhi ya sisi abiria wa Arusha, Moshi na Tanga ambao tunatumia usafiri huo tumefika mara kadhaa zilipo ofisi za reli kuulizia ili kupata taratibu za safari lakini hakuna majibu ya kueleweka.
Kibaya zaidi hata tunapoenda kuulizia palepale kwenue ofisi zao, wahudumu wao nao hawajui kama ilivyo kwa abiria wengine, wanaenda ofisini wanakaa siku nzima bila kazi, wanasaini kisha wanarudi home na mwisho wa mwezi mshahara unaingia kama kawaida.
Naomba kama ni Serikali, mamlaka inayohusika kutoa taarifa juu ya nini kinachoendelea, kwani Treni mbali na kubeba abiria tunaitumia kusafirisha mizigo yetu mizito na mikubwa, kwa sasa tunalazimika kutumia njia mbadala wakati tumeshazoea Treni.
============
Ratiba ya awali ilivyokuwa