A
Anonymous
Guest
Habari wanabodi
Hapo awali treni ya SGR Morogoro - Dar inayochukua abiria takribani 900 ilikuwa inajaa siku 1 au 2 kabla ya safari. Ukiingia mtandaoni hupati tiketi.
Utafiti wangu nilioufanya kwa siku kadhaa kupitia mfumo wa mauzo ya tiketi na kuuhitimisha tarehe 25 Sept 2024, dakika 25 kabla safari (ikumbukwe zikibaki dk 20 kabla ya safari zoezi la ukataji tiketi hufungwa), nimebaini yafuatayo;
1. Ukijaribu kukata tiketi ya Dar-Moro, unakuta kati ya siti 900, siti zaidi ya 500 ziko wazi kutoka Dar kwenda Moro. Hii ina maana kwamba abiria takribani 400 kasoro ndio watakao anzia safari Dar. Hii haijalishi watashukia wapi.
2. TRC wanaweza sema wengine watapandia vituo vya njiani, lakini dakika hiyo hiyo ukirudia kukata ticket ya Soga-Moro unakuta nafasi zaidi karibia 600 kasoro. Hii maana yake ni kwamba; wanaopandia njiani si wengi zaidi ya wanaoshukia njiani, hivyo treni inatoka Dar hadi Moro ikiwa na abiria pungufu zaidi nusu.
Hali hii inatokea pia kwa safari za Moro-Dar.
Kwa kuzingatia hilo tutafakari yafuatayo kwa pamoja;
1. Abiria hawafurahii huduma hivyo wameisusa treni?
2. Mwanzo ilikuwa ni ushamba tu kwa hiyo hata asiyekuwa na safari aliiunda ghafla?
3. Ni hujuma ya abiria kukata tiketi za njiani huku wanafika mwisho wa safari?
4. Je, ukiingia ndani ya treni viti viko wazi kweli kusadifu mauzo hafifu ya tiketi au ndio tiketi haziuziki ila treni imejaa?
5. Kuna hujuma ya baadhi watumishi wa TRC kuingiza abiria bila ticket?
Ikumbukwe kuwa, mwezi Agosti 2024 mwanaJF aliripoti kuhusu ulanguzi wa tiketi, TRC wakaweka utaratibu wa vitambulisho. Ukaguzi wa vitambulisho wakati wa kuingia kwenye treni
umesaidia sana.
Baadae ikaripotiwa na TAKUKURU Morogoro kuwa baadhi ya abiria wanakata tiketi za Pugu huku wanakwenda Moro. TRC walitoa taarifa kuwa wameanza ukaguzi wa kieletroniki mwisho wa safari, kwamba abiria aliyepitiliza kituo, geti la kutokea stesheni halitofunguka. Hili si kweli, hadi sasa hilo halifanyiki. Abiria hukaguliwa mwanzo tu, hata ndani ya treni wakati wa safari hakuna ukaguzi wowote. Sijui kwanini TRC waliamua kudanganya.
Mapendekezo:
1. TRC na vyombo husika wachunguze kama kuna hujuma au abiria wamesusa. Kama ni hilo la pili waangalie abiria wanakwazwa na nini. Kuwe na platform rahisi ya kukusanya maoni ya abiria ikiwemo
kitufe cha maoni kwenye website ya booking.
2. Kama mifumo ya ukaguzi ya mageti ya kutokea stesheni haifanyi kazi, basi wakague mara kadhaa manually ndani ya treni. Mhudumu kila baada ya kituo kimoja au viwili akague abiria wake kama wana tiketi za kuwafanya wawepo walipo.
Hii tusione kama ni usumbufu kwa abiria, ndio jamii tuliyonayo inahitaji hilo. Bado tujajifunza ustaarabu polepole.
Nawasilisha
Dar-Moro
Moro-Dar