Treni ya SGR Dar-Moro kuanza kutoa huduma Januari 2024

Treni ya SGR Dar-Moro kuanza kutoa huduma Januari 2024

IMG-20240131-WA0052.jpg
 
Wanaweza wakaleta pia Train la hivyo la kizamani na likawa linasimama kila Kituo ila hazitakuwa na tofauti sana na Train La sasa la Diesel. Train za hivyo kwa sasa wanataka kuziacha na kubaki wanabebea Mizigo tu na abiria kidogo kwa sababu siyo Economical kabisa. Pia yanakuwa mazito sana na hayawezi speed kubwa.

Hata Aerodynamic yake ni dhaifu na hivyo kupunguza speed.

Ndiyo maana Highspeed zote zinazokwenda zaidi ya 300km/hr ni hizi Bullet Train. Train Kama TGV ya Mfaransa, Shikansen ya Mjapan, Maglev (hii ni Train ta sumaku ambayo nadhani ni Mchina na Mjapan wanaitumia na inaelea bila kugusa chini) zote zipo muundo huo.

Kwa ukubwa wa Tanzania tulitakiwa tuweke TRAIN za umeme Mjini tu labda hadi pembezoni hadi Kibaha. Baada ya hapo mnaweka ya Diesel kwani kwa umbali mrefu, hailipi kutumia Umeme.
Ndiyo maana nchi zote kubwa Kama USA, Canada, Australia nk kwa Train za mbali, wanatumia Diesel Engine peke yake.
Anyway, mengine ni maamuzi ya Wakubwa, huwezi kuwahoji.

Tungeliweza pia kuweka LNG Train au CNG kwani tuna Gas 😂😂
Cha muhimu tumeanza.

Nina wazee wako TRC pale kina Kippaya.
Wamesema kuna mabehewa yatakua ya ordinary kabisa ambayo ni sawa na mabehewa yanayotumiwa katika MGR ya third seat deluxe.
Ambayo yatatumiwa na electric lokomotives na hayo ya kuungwa yatatumika na Electro multiple Unit.
Yani kutakua kuna engine mbili za umeme.
 
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema mwishoni mwa Januari, 2024 treni ya abiria ya reli ya kisasa (SGR) itaanza kutoa huduma kati ya Dar es Salaam na Morogoro.

Huenda kauli ya Profesa Mbarawa ikawa habari njema kwa Watanzania, baada ya wiki hii kushuhudiwa kichwa cha treni hiyo kikifanya majaribio kwenye reli hiyo.

Awali zilitolewa ahadi kadhaa kuhusu majaribio hayo, lakini hazikutekelezeka.

Novemba 19, 2020, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea mradi wa SGR Morogoro na akaeleza kuridhishwa na ujenzi wa kipande hicho, wakati huo ujenzi ukiwa asilimia 90 na aliwaahidi Watanzania kwamba njia hiyo ingepitisha treni ya kwanza Aprili 2021.

Machi 15, 2021 aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho, akiwa Morogoro, alisema treni ya kisasa ingeanza kufanya kazi Agosti mwaka huo.

Aprili 20, 2021, Waziri Mkuu alitangaza tarehe nyingine, akisema treni hiyo ya kisasa ingeanza kufanya majaribio Agosti mwaka huo.

Akizungumza jana katika kikao cha mawaziri saba wa Sekta ya uchukuzi wa Umoja wa Ushoroba wa Kati (CCTTFA), Profesa Mbarawa alisema huduma itaanza kutolewa kuanzia mwishoni mwa Januari, mwakani.

“Jambo la kufurahisha mwishoni mwa Januari, 2024 tutaanza rasmi kutumia usafiri wetu wa SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa ajili ya abiria si mizigo,” alisema.

Mkutano wa mawaziri

Mkutano wa jana uliwajumuisha mawaziri saba wa sekta za uchukuzi wa mataifa ya Tanzania, Uganda, Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi.

Profesa Mbarawa alisema mkutano huo umekuwa wa mafanikio na wamekubaliana masuala mbalimbali ili ushoroba huo upige hatua.

Katika kikao hicho, mataifa ya Zambia na Malawi yalikubaliwa kujiunga na umoja huo na kufikisha idadi ya nchi saba kutoka tano za awali.

Alisema ushoroba huo unaunganishwa kwa miundombinu, ikiwamo ya reli, maziwa na barabara na kwamba, baadhi ya mataifa yanajenga reli za kisasa, ikiwamo Tanzania.

Mawaziri wa sekta za uchukuzi wa Zambia na Malawi waliwashukuru wenzao wa umoja huo kwa kufanikisha mataifa hayo kuingia katika mpango.
Mpaka sasa imeshafanya safari ngapi?
 
Back
Top Bottom