Treni ya SGR yazimika tena Morogoro!


20240802_072438.jpg

20240802_072441.jpg
 
TRC ifanye Kazi na sekta binafsi, wenye uwezo wa kuleta vichwa na mabehewa Kwa standard za TRC waluhusiwe na Wao kuleta wapewe utaratibu, hii itaondoa hisia za kuwa matajiri wa Mabus wanahujumu reli!
Wameishaambiwa wanakaribishwa kuwekeza vichwa na mabehewa harafu watalipia tozo za miundo mbinu
 
I told you guys, Nchi maskini ku opt expensive project using high technology tena za kusubiria mfundishwe na Wazungu haya ndio madhara yake.

Kama tungekuwa tumejenga Barabara km 6,000 Sasa hivi tungekuwa tumevuna Uchumi mkubwa sana ambao ungewezesha kusomesha watu Wetu na kujenga Sgr bila pressure yeyote kuanzia mwaka 2030 huko.

Hela zimepotea na ki sgr chenu kitaendelea kusumbua Hadi mkome

View: https://twitter.com/Mwanahalisitz/status/1819110185480474692?t=_qVsO48V6sF8D4m2t00mgA&s=19

Hakuna wa kuzuia legacy
images.jpeg-190.jpg
 
Kuna taarifa sisizo rasmi kuwa

Treni ya umeme Dom-Dar yadaiwa kupata hitilafu, yakwama kwa muda.​

Je, ni bundi na Ngedere imesababisha hiyo hitilafu Tena?​


***
Treni ya reli ya umeme (SGR) kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam imedaiwa kukwama kwa muda mkoani Morogoro usiku wa Alhamisi Agosti 1, 2024.

Treni hiyo iliyokuwa imebeba abiria na wageni mbalimbali waliotoka kwenye uzinduzi wa huduma za SGR zilizofanyika mkoani Dodoma jana.

Mmoja wa abiria aliyekuwa katika chombo hicho ameiambia Mwananchi Digital kuwa safari ilianza bila changamoto mishale ya saa 2 usiku.

"Tumetoka vizuri tu Dodoma," anaeleza. "Lakini tulipofika katikati ya Stesheni ya Mkata na Moro ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."


Abiria Peter Nyanje, ambaye ni mhariri aliyeshiriki uzinduzi Dodoma, ameripoti changamoto hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiandika:

"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."

Mwananchi haijathibitisha chanzo cha changamoto hiyo, wala idadi ya abiria waliokuwa kwenye treni kutoka kwa mamlaka husika.

Tunaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuutafuta uongozi ama msemaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kupata undani zaidi wa kilichojiri.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa abiria zinaonesha saa 5:35 usiku, treni hiyo ilifanikiwa kuendelea na safari yake mpaka Morogoro, kabla ya kuendelea kuelekea Dar es Salaam.

Hii haikuwa treni pekee iliyorejea Dar es Salaam jana ikiwa na wageni kutoka katika uzinduzi Dodoma.

Treni nyingine ya awali iliyoondoka Dodoma saa 1 usiku ikiwa na viongozi, wasanii na wadau mbalimbali, ilifanikiwa kufika Dar es Salaam bila changamoto.

"Tulitoka Dodoma saa 1 usiku tukasimama kushusha watu kwenye stesheni za Kilosa, Morogoro, Ngerengere na Pugu, tukaingia Dar es Salaam saa 5.32 usiku," anaeleza abiria aliyekuwa kwenye treni hiyo.

Anaeleza, "hakukuwa na changamoto zozote. Tulisubiri tu kwa dakika 25 hivi hapo Pugu ili kuipisha treni ya Dar-Dodoma."

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
yale yale ya Mwendokasi...... na hapo bado sana, hiyo ni cha mtoto. Subiri mpinduke kama tunavyosikiaga India , Bangladeshi na kwingineko kwenye kundi sawa kama sisi
 
View attachment 3059049
Rais Samia akiwasalimia wananchi katika uzinduzi wa treni Agosti 1, 2024

Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi amezindua rasmi huduma za usafiri wa reli ya kisasa (SGR), treni iliyokuwa imebeba wageni walioshiriki uzinduzi huo wakiwamo mabalozi na viongozi mbalimbali wa kiserikali kutokea mkoani Dodoma, imepata tena hitilafu karibu na Stesheni ya Morogoro kwa zaidi saa moja sasa.

Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Mmoja wa abiria aliyemo kwenye treni hiyo amesema:"Tumetoka vizuri tu Dodoma lakini tulipofika katikati ya Mkata na Moro stesheni ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla hadi na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."

Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje katika ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."

Hata hivyo, ilipofika saa 5:35 usiku, treni hiyo ilianza safari.

Juhudi za kuupata uongozi wa Shikika la Reli Tanzania (TRC) zinaendelea.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku mbili baada shirika hilo kuomba radhi kwa treni yake iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete mkoani Morogoro juzi tarehe 30 Julai 2024.

Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

“Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system),” amesema.

Mwananchi
View attachment 3059048
1722573476868.jpeg




During the four years he spent in black Africa as the bureau chief for the Los Angeles Times, David Lamb traveled through almost every country south of the Sahara, logging more than 300,000 miles. He talked to presidents and guerrilla leaders, university professors and witch doctors. He bounced from wars to coups oceans apart, catching midnight flights to little-known countries where supposedly decent people were doing unspeakable things to one another. In the tradition of John Gunther's Inside Africa, The Africans is an extraordinary combination of analysis and adventure. Part travelogue, part contemporary history, it is a portrait of a continent that sometimes seems hell-bent on destroying itself, and of people who are as courageous as they are long-suffering.


Report an issue with this product or seller
 
Hiyo miradi ilikuwa ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli, hayupo tena

Sasa sijui niseme au sijui niishie tu hapa?
 
Kama tulishindwa kuendesha zile treni za zamani, tukashindwa kuendesha mwendokasi, hata hii SGR kwa 100% tutashindwa kuendesha.
Tatizo kuna washenz wachache wanafanya hujuma
Inanyike intelligence ya maana kama ya Mossad iwabaini hao wahuni mapema sana na kuwanyoosha
 
Back
Top Bottom