Treni yaleta ‘kilio’ usafiri wa mabasi Dar - Moshi

Mkuu, asante kwa taarifa.

Hapa tunazungumzia nchi ya ulimwengu wa tatu, kwa abiria (hasa mnyonge) kuchagua usafiri anaoutaka na kwa kadri anavyomudu gharama za usafiri ni jambo la kimaendeleo. Pia kuna suala la usalama ambapo mtu anasafiri toka upande/sehemu moja ya nchi hadi nyingine kwa amani na utulivu huku akifurahia safari yake.

Kwa mtu/mwananchi (hasa wakazi wa mikoa ya kaskazini) anayefurahia haya atasema chochote kuelezea furaha yake. Kwa hilo tutasikia mengi. Pia tunafahamu kuwa wapo wasiopenda uwepo wa jambo hili. Tunawapa pole. VIVA TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kigoma Kuna treni na mabasi yanajaa tu....hao waboreshe huduma,wajue n wapi wamekwama

Sent using Jamii Forums mobile app
Unalinganisha mabasi yanayokwenda kigoma na yanayokwenda kaskazini kwa Tanzania ? Unaota ndoto ya asubuhi mkuu.ili kujua Hali halisi na kwa vitendo kuwa train imevuruga mabasi na wamiliki wake njoo stand ya mkoa muda huu Niko hapa , mabasi yapo hakuna abiria na yaliyoondoka hayakujaa. Hali sio Shari na wapigadebe nawaona kukizurura tu na kupiga kelele.wengi wameanza kuhamia stand ya dodoma na morogoro ili kujipatia mlo wa siku.
 
Kwa hiyo usafiri wa trani uzuiliwe?

No way out. Ni kutafuta njia mbadala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa hata mama kimario muuza vitumbua anauhakika wa kwenda moshi krismasi kula na kunywa mbege na watoto.
Hivi bado wachaga mna kadi za chadema
 
Hali tete,dogo aliyeuza Maori 300 na mabus ni yupi tena
 
Nadhan hapa tajir na timu yake watabidi warekebishe nauli na baadhi ya changamoto zinazolalamikiwa na abiria. Hapo wapanda tren watakuwepo na wapanda mabasi watakuwepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani nimesoma huu uzi asee nimebaki nacheka 16/12/2019 nimetoka dar kuja chuggah pale shekilango Kilimanjaro ametoa gari 10 zinazoenda arusha na Moshi na kwenda dar hivyo hivyo na gari zote zipo level seat na wengine wamepakiwa njiani wakakaa pale pembeni ya derava juu ya engine sasa kusema biashara ya bus itakufa nakataa na ninapinga

Hii ni Korogwe Kilimanjaro fast food vyuma vikepaki mapumziko ya dk 30 za chakula


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ingekuwa ni hivyo hiyo biashara ingekufa kwa Mbeya na Mwanza ambako treni zipo!!

Usisikilize kauli za masikini na washamba!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda Mabasi ya 3rd Class. Yale First class yamejaza Hadi 26 Dec. Nenda pale Shekilango yalipo Dar Exp, Dar Lux,KLM, Kidia, Tilisho,Esta hata Kwa Laki hupati. Nafasi Zimejaa Booked ana paid.
 
Labda Mabasi ya 3rd Class. Yale First class yamejaza Hadi 26 Dec. Nenda pale Shekilango yalipo Dar Exp, Dar Lux,KLM, Kidia, Tilisho,Esta hata Kwa Laki hupati. Nafasi Zimejaa Booked ana paid.

Ndio maana nasema bado nchi inahitaji mabasi na train pia


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…