Treni yaleta ‘kilio’ usafiri wa mabasi Dar - Moshi

Treni yaleta ‘kilio’ usafiri wa mabasi Dar - Moshi

Hesabu zako aziko sawa hebu piga upya
Abiria 450×trip 3 = 1350 abiria kwa wiki

Abiria 1350 × wiki 4 = 5400 abiria kwa mwezi.

Idadi hiyo 5400 ni sawa na mabasi mangapi?
Linganisha hapo alafu uje na hitimisho
hayo ni mabasi 100 ni sawa na safari ya siku moja tu ya mabasi ya arusha!
bado haiwez athiri mfumo! maana wao pia huwa wanakodi coaster tarehe zikifka! watagawana mbao
 
Kweli mmeshikwa pabaya, Kwanza mlisema hapandi mtu, watu wa Moshi wanauwezo na wana magari yao, baadae mkasema usafiri wa kishamba Nani asafiri usiku kucha, sasa hivi wenye magari wanalalamika abiria sio kama miaka iliyopita wewe unasema train haitoshi, sio kweli Wana mabehewa ya kutosha abiria wakiongezeka na wao wataongeza mabehewa, nitakubaliana na wewe ukisema kwamba hawa abiria ni wa.msimu

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanza nikuambie tu mimi siishi huko nafikiria ukisoma vizuri utanielewa
La pili population yenu ni zaidi ya 50m
Unafikiri trains hizo zinatosha?
Na je mabasi hayo yanakidhi usafiri?
Bado sana mkuu Hebu tembea uone dunia jinsi watu walivyowekeza kwenye usafiri
Hakuna neno msimu kwenye usafiri


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
hayo ni mabasi 100 ni sawa na safari ya siku moja tu ya mabasi ya arusha!
bado haiwez athiri mfumo! maana wao pia huwa wanakodi coaster tarehe zikifka! watagawana mbao
Kwahiyo Dar- Arusha ina mabasi 100 yanayofanya safari?
 
Kwahiyo Dar- Arusha ina mabasi 100 yanayofanya safari?
yanafika bana kuna kampuni zaidi ya 25 nwa wastani wa gari tatu au 4 kwa kila kampuni

mfano Dar exp, Dar lux, Hai, Happy nation, serengeti, buffalo, ngorika, machame, esther, marangu, BM, na wengine wengiii
 
Sasa kama treni inabeba abiria 150 tu tija ya uwekezaji iko wapi? Au wameamua kufanya huduma tu?

Abiria 150 si ni makadirio ya mabasi matatu tu ya kawaida? Behewa moja linachukua abiria wangapi? Na hiyo treni ina mabehewa mangapi?
 
Yaani treni inaenda Moshi mara 3 kwa week, trip moja inabeba watu 150 kwa hiyo hadi mwezi uishe itakuwa imebebeba abiria kama 2000 tu ndiyo imeua biashara ya mabasi msimu wa Christmas?

Get outta here.
Daaa mkuu hata kwa akili ndogo tu haiwezekani yaani mabehewa yote yabebe watu 150? Kama level seat ni 100 ya behewa moja bado watakao simama kwa third class iweje behewa 14 zibebe watu 150

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda mimi ndio sielewi hapa
Usafiri bado sana huko hata kama wataweka train tatu naona bado mabasi yatapata wasafiri tu
Train moja tu tena safari moja wanalalamika
Hapa nilipo watu ni 60m na usafiri wa train upo wa chini ya ardhi na upo wa juu na ni nyingi sana
Lakini pia mabasi yapo ya nje ya mji na yote yanajaa full
Katika usafiri bado sana na wasafiri ni wengi bado


Sent from my iPhone using Tapatalk
Nakubaliana na wewe kabisa.Hizo treni ni hatua ya maendeleo lakini haziwezi kuuwa biashara ya mabasi kwa sababu kila usafiri una sifa na kasoro zake na abiria wana sababu tofauti za kusafiri.Wengine ni wafanyabiashara wanapenda walale kwenye treni asubuhi wafike waendako na wengine ni wagonjwa au wanafunzi wanataka asubuhi mapema wawe wa mwanzo kufika sehemu husika sio saa mbili linapofika treni hata kuoga bado.
Tukiendelea na sababu za kusafiri,wengine ni watalii wanapenda wasafiri na kufaidi mandhari ya mazingira wanamopita ili kujifunza hili na lile.Kwa upande wangu huku niliko usafiri wa treni una nguvu sana na treni zimeunganishwa na miji yote ya nchi lakini pia mabasi ni mengi sana.Vituo vingi vya treni vinapendeza na vimepangiliwa kuliko hata uwanja wetu wa JK uliopo Dar es salaam.Treni zinaingia na kuondoka takriba kila baada ya robo saa sio usiku usiku au jioni jioni .Zaidi ni njia za mabasi hakuna kupishana mpaka unafika unakokwenda.Sehemu zinapokutana barabara iwe ni ya treni au mabasi basi moja inapita juu na nyengine chini yake.Katika hali kama hiyo mabasi yanjaa na matreni pia.
 
Nimecheka sana ....tena sana... 🤣🤣🤣🤣!!

Ndugu zangu tupunguze kebehi , Behewa moja linabeba abiria zaidi ya 65 wa basi.... na treni tunakuta inabehewa 15 mpaka 30!!! Leo mtu anatwambia treni inabeba watu sawa na behewa 2 tu!!!!

Mnaweza kusema hakuna athari yeyote maana kwamba kila abiria ana aina ya usafiri apendayo..... lakini ukweli unabaki kuwa TRENI IMELETA UKOMBOZI WA SAFARI KANDA YA KASKAZINI KUANZIA SIKU HIZI ZA SIKUKUU NA SIKU ZIJAZO,

WENYE MABASI WANAJUA JINSI GANI ZAIDI YA ABIRIA 5,000 WAKIONDOKA KWENYE MZUNGUKO WAO,

SISI WENGINE TUBAKI WATAZAMAJI WAKATI TANZANIA INAANZA KUAMKA TENA!!!
 
yanafika bana kuna kampuni zaidi ya 25 nwa wastani wa gari tatu au 4 kwa kila kampuni

mfano Dar exp, Dar lux, Hai, Happy nation, serengeti, buffalo, ngorika, machame, esther, marangu, BM, na wengine wengiii

Kila siku Ubungo yanatoka wastani wa mabasi 400 kwenda mikoa yote nchini


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwahiyo siku 4 za wiki zilizobaki watu hawasafiri wanasubiri treni?
 
Back
Top Bottom