Treni yenye Watalii 60 yatoka Afrika Kusini hadi Tanzania

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
TRENI YA WATALII YA ROVOS YAPOKELEWA

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), imepokea treni ya Kitalii Kampuni ya ROVOS yenye Watalii 60 kutoka nchini Afrika Kusini.

Treni hiyo ilianza safari yake mwezi Juni 30, 2023 na imepita katika nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na kuhitimisha nchini Tanzania.

Afisa Utalii Mkuu Bi. Alistidia Karaze amesema kuwa Bodi ya Utalii Tanzania Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea Watalii 60 waliotoka Mataifa ya, Denmark, Canada, Australia, Malaysia, Marekani na Afrika Kusini.

"Watalii hawa wamekuja na treni ya ROVOS alionza safari kutoka Afrika Kusini, wakiwa nchini watapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar" amesema Karaze

Ameongeza kuwa tukio hilo ni kutokana na juhidi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan Suluhu kupitia filamu ya " The Royal Tour" kutangaza utalii duniani.

Mtalii Andrew Saimon kutoka Marekani amefurahishwa na mapokezi makubwa kutoka Tanzania na kuwapongeza watanzania Kwa kuwa watu wakarimu na wenye upendo.

IMG-20230715-WA0006(1).jpg
IMG-20230715-WA0007(1).jpg
IMG-20230715-WA0008(1).jpg
IMG-20230715-WA0005(1).jpg
 
Huenda hayo mapokezi yamecost robo tatu ya kilichopatikana / kilichoingizwa..., Hizi Political Mileage zinatutoa kwenye Reli hizo Juhudi / Matangazo wayapeleke huko wanakotoka au wawape moyo wenyeji ili hospitality iwe nzuri through word of mouth hawa wadau warudi tena

(huku kitaa sisi sio walengwa na kama motive ni kuonyesha mnafanya vyema ili kwenye debe mchaguliwe nadhani there are more effective ways za kufanya - Na Matozo na Kupandisha Makodi kila kukicha is not one of them)
 
TRENI YA WATALII YA ROVOS YAPOKELEWA

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), imepokea treni ya Kitalii Kampuni ya ROVOS yenye Watalii 60 kutoka nchini Afrika Kusini.

Treni hiyo ilianza safari yake mwezi Juni 30, 2023 na imepita katika nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na kuhitimisha nchini Tanzania.

Afisa Utalii Mkuu Bi. Alistidia Karaze amesema kuwa Bodi ya Utalii Tanzania Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea Watalii 60 waliotoka Mataifa ya, Denmark, Canada, Australia, Malaysia, Marekani na Afrika Kusini.

"Watalii hawa wamekuja na treni ya ROVOS alionza safari kutoka Afrika Kusini, wakiwa nchini watapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar" amesema Karaze

Ameongeza kuwa tukio hilo ni kutokana na juhidi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan Suluhu kupitia filamu ya " The Royal Tour" kutangaza utalii duniani.

Mtalii Andrew Saimon kutoka Marekani amefurahishwa na mapokezi makubwa kutoka Tanzania na kuwapongeza watanzania Kwa kuwa watu wakarimu na wenye upendo.

View attachment 2689015View attachment 2689016View attachment 2689017View attachment 2689018
Safi sana
 
Nyie ccm ni waongo, hakuna reli ya kutoka South Africa kuja Tanzania labda kama ipo Zambia to South inawezekana kuja hadi Tanzania kupitia TAZARA.
 
Wazungu inawezekana wanajua serengeti na kilimanjaro tu hawajui hata Rais nani
Kwani umeambiwa wamekuja kuitikia wito wa raisi au kushughulikia habari zake?!!!!! Mbona haters hadi 2030 mtawehuka si kitoto!!!!

Go mama Samia gooooooooo!!!
 
Back
Top Bottom