Treni yenye Watalii 60 yatoka Afrika Kusini hadi Tanzania

Treni yenye Watalii 60 yatoka Afrika Kusini hadi Tanzania

Nyie ccm ni waongo, hakuna reli ya kutoka South Africa kuja Tanzania labda kama ipo Zambia to South inawezekana kuja hadi Tanzania kupitia TAZARA.
Sasa wewe Kwa akili Yako fupi unadhani hakuna interconnectivity ya reli Hadi South Africa?

Kwa taarifa Yako unaweza Toka Angola Hadi Dar Kwa train hii hii ya Ravos
 
Kwahiyo kwa asilimia kubwa nchi za Kiafrika zimeunganishwa na reli, si ndiyo? Sisi wengine hatuna exposure ya kusafiri nje ya Tanzania

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Point yako ni unakataa au ? Sjasema nchi zote za africa zimeunganishwa na reli ila unaweza kutoka dar mpk SA congo angola kwa reli
 
Mkuu reli ya TAZARA inaunga mpaka South kwa Madiba kitaalamu wanaita Cape Gauge ni tofauti kidogo na Standard Gauge inayojengwa Bongo
Turekebishe kidogo mkuu.

Utofauti kidogo ni kwa meter gauge kwasababu upo sawa umeiita cape gauge ina kipimo cha 1067mm na meter gauge ni 1000mm. Utofauti kidogo pia ni aina ya sleepers zinazotumika cape ni zage na meter ni chuma.

Standard gauge ni 1435mm.

Pia kama ulivyosema cape gauge inafika hadi S.A
 
Kama nawaona marasta uchwara walivyozagaa zagaa hapo station kuona kama wataambulia ambulia kibibi
🤣🤣

Kwa upande wa Tanzania wengi ni wanahofu

Rovos isimame matabeleland-ZW 🤣🙌
Kuna binadamu wamejitoa mhanga kwa ngozi nyeupe.🙌
 
Kama nawaona marasta uchwara walivyozagaa zagaa hapo station kuona kama wataambulia ambulia kibibi

🤣🤣

Kwa upande wa Tanzania wengi ni wanahofu

Rovos isimame matabeleland-ZW 🤣🙌
Kuna binadamu wamejitoa mhanga kwa ngozi nyeupe.🙌
 
TRENI YA WATALII YA ROVOS YAPOKELEWA

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), imepokea treni ya Kitalii Kampuni ya ROVOS yenye Watalii 60 kutoka nchini Afrika Kusini.

Treni hiyo ilianza safari yake mwezi Juni 30, 2023 na imepita katika nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na kuhitimisha nchini Tanzania.

Afisa Utalii Mkuu Bi. Alistidia Karaze amesema kuwa Bodi ya Utalii Tanzania Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea Watalii 60 waliotoka Mataifa ya, Denmark, Canada, Australia, Malaysia, Marekani na Afrika Kusini.

"Watalii hawa wamekuja na treni ya ROVOS alionza safari kutoka Afrika Kusini, wakiwa nchini watapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar" amesema Karaze

Ameongeza kuwa tukio hilo ni kutokana na juhidi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan Suluhu kupitia filamu ya " The Royal Tour" kutangaza utalii duniani.

Mtalii Andrew Saimon kutoka Marekani amefurahishwa na mapokezi makubwa kutoka Tanzania na kuwapongeza watanzania Kwa kuwa watu wakarimu na wenye upendo.

View attachment 2689015View attachment 2689016View attachment 2689017View attachment 2689018
Royal tour oyee
 
Back
Top Bottom