Treni yenye Watalii 60 yatoka Afrika Kusini hadi Tanzania

Hao waliunga unga wakafika Zambia, then Zambia to Tz via tazara railway. Hakuna tren ya Dar to South Afrika, labda reli ya ccm.
 
Jinsi unavyowona barabara zilivyo za kuunga hadi unafika Nchi zingine,na reli nazo hivyo hivyo unauunga hadi unafika Misiri! Kama hapo unaona Watu wametoka South na reli ya South kupitia Zimbabwe hadi kuingia Zambia, Zambia wakala reli ya Tazara hadi Tanzania!!
 
Hongera mbabe wetu wa Royal Tour.

1689474746591.png
 
TRENI YA WATALII YA ROVOS YAPOKELEWA

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), imepokea treni ya Kitalii Kampuni ya ROVOS yenye Watalii 60 kutoka nchini Afrika Kusini.

Treni hiyo ilianza safari yake mwezi Juni 30, 2023 na imepita katika nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na kuhitimisha nchini Tanzania.

Afisa Utalii Mkuu Bi. Alistidia Karaze amesema kuwa Bodi ya Utalii Tanzania Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea Watalii 60 waliotoka Mataifa ya, Denmark, Canada, Australia, Malaysia, Marekani na Afrika Kusini.

"Watalii hawa wamekuja na treni ya ROVOS alionza safari kutoka Afrika Kusini, wakiwa nchini watapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar" amesema Karaze

Ameongeza kuwa tukio hilo ni kutokana na juhidi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan Suluhu kupitia filamu ya " The Royal Tour" kutangaza utalii duniani.

Mtalii Andrew Saimon kutoka Marekani amefurahishwa na mapokezi makubwa kutoka Tanzania na kuwapongeza watanzania Kwa kuwa watu wakarimu na wenye upendo.

View attachment 2689015View attachment 2689016View attachment 2689017View attachment 2689018
Zamani tuliyaita makaburu sasa hivi tunayaita matalii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
niliwaona bagamoyo siku ya jumatano.wakipanda kiboti kidogo wakielekea zanzibar.
 
Hao waliunga unga wakafika Zambia, then Zambia to Tz via tazara railway. Hakuna tren ya Dar to South Afrika, labda reli ya ccm.
Tazara inaishia Zambia sawa lakini pale reli inaendelea mpaka South africa kupitia Botswana na Zimbabwe reli ni hii hii sasa nyinyi mnafikiri hiyo treni huwa wanaibeba kuihamishia reli ya tazara

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Kama hujui uwe unakaa kimya hiyo treni ya kitalii ina kuja karibia kila mwaka toka South africa moja kwa moja!...tazara kama tazara inaishia Zambia ila pale reli inaendelea mpaka South africa

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Tazara inaishia Zambia sawa lakini pale reli inaendelea mpaka South africa kupitia Botswana na Zimbabwe reli ni hii hii sasa nyinyi mnafikiri hiyo treni huwa wanaibeba kuihamishia reli ya tazara

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Mimi hilo sijui ninalojua Tazara mwisho Zambia. Kama wametengeza kiungo pale Zambia sawa
 
Natamani Tanzania ingefanya vitu kama hivi, ikaweka reli safi kwa ajili ya utalii`: Dar to Kigoma round trip labda siku 10.

Inasimama katika maeneo muhimu watu wanatoka kidogo halafu wanaendelea na safari.

Siyo hii beba beba lakini iwe kama hiyo ya South Africa.
 
TRENI YA WATALII YA ROVOS YAPOKELEWA

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), imepokea treni ya Kitalii Kampuni ya ROVOS yenye Watalii 60 kutoka nchini Afrika Kusini.

Treni hiyo ilianza safari yake mwezi Juni 30, 2023 na imepita katika nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na kuhitimisha nchini Tanzania.

Afisa Utalii Mkuu Bi. Alistidia Karaze amesema kuwa Bodi ya Utalii Tanzania Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea Watalii 60 waliotoka Mataifa ya, Denmark, Canada, Australia, Malaysia, Marekani na Afrika Kusini.

"Watalii hawa wamekuja na treni ya ROVOS alionza safari kutoka Afrika Kusini, wakiwa nchini watapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar" amesema Karaze

Ameongeza kuwa tukio hilo ni kutokana na juhidi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan Suluhu kupitia filamu ya " The Royal Tour" kutangaza utalii duniani.

Mtalii Andrew Saimon kutoka Marekani amefurahishwa na mapokezi makubwa kutoka Tanzania na kuwapongeza watanzania Kwa kuwa watu wakarimu na wenye upendo.

View attachment 2689015View attachment 2689016View attachment 2689017View attachment 2689018
Hii treni iko toka siku nyingi karibu miaka saba sasa na ilianza na Trans africa kwa hiyo usidanganye watu hii ipo kitambo sana.
 
Back
Top Bottom