Sheriff Hood
Member
- May 3, 2018
- 89
- 131
Wakuu nasumbuliwa na maumivu makali upande mmoja wa uso kwenye shavu karibu na sikio. Maumivu haya yanakuja kila baada ya kupita muda fulani inaweza ikawa nusu saa, lisaa au masaa kadhaa, yakija yanadumu kwa sekunde kadhaa then yanatoweka, maumivu mithili ya shoti kali ya umeme, au kama mtu anakuchoma na kitu chenye ncha kali, maumivu yanakuja ghafla bila kuwa na dalili yoyote.
Kiukweli yananipa shida yananifanya niishi kwa wasiwasi sana.
Nilitumia vidonge vya kutuliza maumivu ya neva, ikatulia ila baada ya miezi mitatu yamerudi tena.
Naomba wataalam mnipe ufafanuzi jinsi ya kupata utatuzi wa kudumu wa tatizo hili. Hospitali ipi naweza kutibiwa na gharama zake zikoje.
Asante