I wrote this somewhere.
Albert Fish - Gray Man, Werewolf of Wysteria
Edward Budd aliweka tangazo kwenye gazeti kua anatafuta kazi. Akataja anwani aliyopo na kwamba yupo radhi kufanya kazi kokote. Baada ya muda wakapokea mgeni, Albert Fish.
Muonekano wa kitajiri, umri umesogea kidogo, nywele zenye mvi, nadhifu na alitembea na pesa nyingi mfukoni. Usingeweza wazia kingine.
Akakaribishwa ndani akaeleza kua ameona tangazo na amekuja kukutana na kijana mwenyewe, Edward akaitwa, akaja ila alikua na kijana mwingine, Willie. Albert akasema amependa kama angeweza kuondoka nao wote.
Akakubaliwa.
Wakawa wamekaa wanapiga stori akiwaelezea maisha ya mjini. Stori zikiwa zinaendelea akaingia binti wa miaka 10, ilikua Jumapili Gracie alikua akitokea kanisani. Kumuona tu Albert akatoa pesa na kumtania "Hesabu nikuone" Gracie akahesabu na kumtajia kiasi sahihi, Albert akampa pesa akamwambia akanunue pipi.
Kisha akawapa pesa kidogo Edward na Willie. Akaomba udhuru kwa wazazi wao akisema anaenda kwenye birthday ya mtoto wa dada yake siyo mbali na hapo, sherehe ikiisha angewapitia Edward na Willie na kuondoka nao.
Wazazi wakakubali.
Albert akapendekeza aende na Gracie.
Wazazi wakakubali.
Wakataka wambadilishe nguo angalau akalingane na wenzake huko kwenye sherehe. Albert akasema yupo sawa hivyo alivyo wasitie shaka hivyo wao wanaenda.
Grace Budd
Wakaondoka. Muda ukayoyoma si Albert wala Gracie aliyerudi. Wakaifuata anwani aliyowatajia hawakukuta jengo na ilkua ni anwani feki, badala yake walikuta pagale.
Kwa maelezo ya Albert ni kwamba huo muda alimpotezesha fahamu Gracie kisha akamficha humo yeye akaenda matembezini akitarajia arudi usiku aondoke naye.
Lakini waliomtafuta Gracie pengine walikua na kihoro hata hawakuingia kwenye lile pagale.
Hiyo ikawa Jumapili ya mwisho ya wazazi, na kaka zake Willie na Edward kumuona Gracie. Hawakuweza muona hata akiwa mfu kwakua Albert alimla Gracie.
Familia ya Gracie ikapokea barua. Barua ilitoka kwa Albert Fish, safari hii alitaja jina lake la kweli na akaelezea tukio zima kuanzia kumuacha Gracie kwenye pagale kumrudia usiku na kwenda naye kwake. Hakuacha kitu. Alielezea ni jinsi gani alimkata vipande vidogo vidogo kumpika na kumla, anadai alikula mwili wa Gracie kwa zaidi ya siku 10.
Hii barua ikafikishwa polisi. Ikaanza kufuatiliwa ilipotokea, ikaja kukutwa orijin yake ni huko mjini wakajikuta ana kwa ana na kijana wa kiume ambaye akakiri kua ni kweli ile anwani ni yake lakini hajawahi kuandika barua na kuituma kwenda kwa anwani ya Budd.
Hii inamaanisha ili kumkamata ilitakiwa atume tena barua ila safari hii ofisi za posta ziwe na maafisa watakaokua wakiangalia kila anayetuma barua. Tatizo likawa vipi kama asipotuma tena? Ingekua anwani ni ya kweli wangeweza kumtumia na yeye ili aijibu ila haiko hivyo, so what next?
Kitu kimoja kuhusu serial killers hua wanajihisi wao ni miungu, wanatamani kusujudiwa, kuonyeshwa kua umuhimu wao ni mkubwa. Hivyo ukiweza kucheza na akili ya muuaji wa aina hii una % nzuri za kumkamata.
Maaskari wakaipublish barua kwenye gazeti kisha wakasema kila kilichokua mule ni uongo mtupu, wakasema kua rangi ya gauni iliyotajwa mule ni uongo, ni uongo pia kwamba Albert Fish alikua ndiye kinara wa mazungumzo ile siku yupo kwa Kina Gracie. Wakasema alikua ni mzee muoga, dhaifu ambaye hakuonyesha kuana nguvu.
Kilichofuata ITV? Albert akatuma tena barua, tena safari hii akawatumia na polisi, shenzi kabisa mnasema mi muongo? Hahaha hiyo sehemu ya tusi nimetunga.
Albert chini ya ulinzi
Anyway, akawa amejitia kitanzini. Ile barua ya kwanza na ya pili ilielezea mauaji kinaga ubaga kiasi ilikua na details ambazo ni muuaji tu angeweza kuzijua.
Mahakamani Albert alikutwa na hatia na akahukumiwa kifo. Adhabu yake ya kifo ilitekelezwa kwa kutumia kiti cha umeme na huo ukawa mwisho wa Albert Fish.
Siku ya hukumu